Madhara ya chama kimoja kukaa madarakani muda mrefu ndio haya. Wenye nchi chukueni hatua

Muda wa kukaa na kuandika haupo nitakuwa bize Sana!!majukumu ya kifamilia yananiandama na najitahidi kuwa Baba Bora kabisa kwa wangu!!
 
Waafrika sio watu wa kuweza kuendelea chini ya tawala za kiimla, ingekuwa hivyo basi Afrika ndio ingekuwa bara iliyoendelea kuliko zote duniani.

Tunahitaji mabadiliko ya mara kwa mara katika uongozi wetu wa juu ili kuleta fikra kinzani ambayo ndio inaweza ikachochea maendeleo ya nchi.

Lakini kwa huu utaratibu wa chama fulani kung'ang'ania madaraka pasipo ridhaa ya wananchi maana yake ni kwamba tutaendelea tu kuchoma mahindi 🌽
 
Leo nchi yetu inalizwa na ufisadi uliofanywa na viongozi wa umma kwasababu tulilea ufisadi sisi wenyewe kwa kuruhusu kikundi cha aina moja kukaa madarakani kwa muda mrefu Sana na kupata muda wa kutosha wa kufanya ufisadi huo kea kutunza sheria lege lege zinazowabeba wao kushika hatamu
 
Usituletee uchuro hayo mambo hatujazoea sisi...Nchi yetu tutaibadili kwa amani na bila vurugu yeyote. Jeshi letu limekuwa na nidhamu ya hali ya juu kwa Jamuhuri ya Muungano usiliingize kwenye mambo maovu kama haya...Haijalishi kama unapenda au unauvhukia kila uongozi watoka kwa Mungu na anakuwa na sababu zake kwanini uwe huo...Mungu ameumba wema na ubaya kwa matumizi yake binafsi
Huu wa sasa ndio UCHURO wenyewe. Nchi imejaa washetani yaliyo katika mashindano ya kubambikiza watu kesi, kula kwa urefu wa kamba, mazingaombwe ya karibuni ya akina Betina na wenzie huko bungeni
 
Leo nchi yetu inalizwa na ufisadi uliofanywa na viongozi wa umma kwasababu tulilea ufisadi sisi wenyewe kwa kuruhusu kikundi cha aina moja kukaa madarakani kwa muda mrefu Sana na kupata muda wa kutosha wa kufanya ufisadi huo kea kutunza sheria lege lege zinazowabeba wao kushika hatamu
Mshanar kama mshanar yaani!!umequote pisi kali mno kwenye Uzi!!
 
Kikwazo kikubwa kwenye nchi zetu za Africa ni majeshi, kama yangeamua kusimama na wananchi nadhani Africa ingekuwa vizuri sana
 
Kushika hatamu kwa chama kimoja kwa muda mrefu huleta mazoea na uzembe wa kutowajibika ndio huleta kudumaa kwa maendeleo ya nchi na kukosa fikra mbadala za kisukuma gurudumu la maendeleo nchini.

Vitendo kama ufisadi hutamalaki na ubwanyenye wa kubweteka hii inatokana na wenye chama kupata muda mrefu wa kuratibu uchafu wao ndani ya serikali na kujimilikisha Mali za umma kama miungu watu.

Leo nchi yetu inalizwa na ufisadi uliofanywa na viongozi wa umma kwasababu tulilea ufisadi sisi wenyewe kwa kuruhusu kikundi cha aina moja kukaa madarakani kwa muda mrefu Sana na kupata muda wa kutosha wa kufanya ufisadi huo kea kutunza sheria lege lege zinazowabeba wao kushika hatamu.

Kama tungeshtuka mapema vitendo vya kifisadi visingekua na mizizi mrefu kiasi hiki!kwasababu wanasiasa wasingekua na uhakika wa chama gani kitashika Dola uchaguzi ujao Baada ya kilichopo kuangushwa wasingekua na mipango ya muda mrefu ya kipigaji.

Ukanda,mauaji,chuki za kiitikadi za vyama ni matokeo ya kuruhusu chama kimoja kushika hatamu kea muda mrefu!!Tumetengeneza kundi la watu au Koo Fulani ambazo hazidhani kama zitakua hai bila madaraka!zinadhani madaraka ni haki yao ya asili na sio haki ya watanzania wengine.

Tatizo hilo limetokana na kukosa watu wenye maono ya mbali Sana kwenye Taifa letu!!Inawezekana wenye maamuzi ya nchi yetu walishiba vya kutosha na kutiwa upofu na raha wanazopata kwa kula keki ya Taifa peke yao.

Kuna haja ya taasisi za kijasusi za nchi yetu kuratibu siasa za nchi yetu kea manufaa na maono kuliko kuwaachia wanasiasa hasa wa chama tawala kuamua hatma ya siasa zetu!!!Aina hii ya siasa ndio umefanya ufisadi na umungu watu kuzidi nchini kwetu.

Kiukweli kabisa kama wenye nchi wangekua na maono wangebadili chama ambacho kingetwaa madaraka hapo 2015 Baada ya kelele za ufisadi kwa awamu ya nne!!pia wangeratibu na aina ya mgombea ambaye wangetaka ashinde uchaguzi ule!!Lakini kosa kubwa waliwaachia wanasiasa waamue hatma yetu ambayo ndio hii imeleta ukakasi na ombwe na wingu la chuki na uadui lenye kuhitaji Mabadiliko makubwa ya uongozi yenye maumivu Sana na kujikuta hakuna namna zaidi ya kuyakumbatiamaumivu yao.

Vuta picha kama hayati jpm angeshinda uraisi hapo 2015 kwa kupitia CHADEMA chini ya uratibu wa wenye nchi unadhani teka teka ile,ua ua Ile na potea potea ile ingetokea???sidhani kama angewatesa wanachama wake wapya kwa kesi zile zisizoisha!!hata kama kwa chama hata cha CUF au nccr mambo yasingekua hivi leo.

Nadhani wenye nchi Wana la kujifunza kwamba Zama za kuacha chama kimoja kitawale kwa miaka 20 na zaidi zimepitwa na wakati!!sasa ni Zama za kuwa na siasa zisizo tabirika na kiutafiti na za kisayansi!!wakati umefika wa kutengeneza watu nje ya mfumo wa kisiasa na chama na kuwaingiza pole pole kwenye vyama ili washinde uraisi kuwa chama chochote na kuwa na siasa zisizo tabirika.

Sote tunajua demokrasia ni kuhalalisha ushindi wa kiongozi aliechaguliwa na wachache kwa Njia ya uchaguzi kama tufanyavyo kea miaka mingi!Muda umefika wa kutumia mwanya huo kuanzisha siasa na chaguzi zisizo tabirika.

Ukweli ni kwamba siasa za chama kimoja kushika madaraka kea muda mrefu zimeacha majeraha,makovu na maumivu yasiyovumilika nchini kwetu vuteni picha ya idadi ya nguvukazi na walipa kodi tuliowapoteza kwa siasa za aina hii tulizoziendekeza kwa miaka mingi.

Pigeni hesabu make na takwimu hapa jamvini.

Wenye nchi kuna haja ya kutubu kwa dhambi hii ya kukosa maono kwa nchi yetu!!Bandiko hili mkatoe kopi na kuwekwa mlangoni mwa ofisi zenu za siri kama ukumbusho wa toba wa dhambi hii kubwa.

Wenye nchi someni halafu mchukue hatua!
Such a good thread. Me ndo naisoma Leo.

Kuzaliwa Kwa CCM kuliua TANU na TAA na Katiba mpya ilizaliwa.

Likewise, Haiwezekani kuandika KATIBA mpya bila kukiua chama kilichopo.

Kifo Cha CCM ni INEVITABLE baada ya Katiba mpya kupatikana.

Bado namba zinasoma vile vile kuwa, baada ya 2026 hapatakuwa na CCM.

Ameeeen.
 
Neno kea ni typing error ni kwa !!isomeke hivyo!!ni mimi mwenzenu ninaeamini utanzania wetu haupimwi kwa itikadi za vyama bali uzalendo binafsi!pia naamini chama kingine kikishika hatamu hautokuwa mwisho wa Tanzania yetu kama wanasiasa wanavo wadanganya!!mf:-eti ukichagua upinzani kutatokea vita!!!kauli mbovu kabisa kutamkwa uchaguzi 2015!!nilishangaa Sana kauli hii!!
Ni Kweli, pasingekalika maana mizizi ya CCM imeenda deep sana.
 
Such a good thread. Me ndo naisoma Leo.

Kuzaliwa Kwa CCM kuliua TANU na TAA na Katiba mpya ilizaliwa.

Likewise, Haiwezekani kuandika KATIBA mpya bila kukiua chama kilichopo.

Kifo Cha CCM ni INEVITABLE baada ya Katiba mpya kupatikana.

Bado namba zinasoma vile vile kuwa, baada ya 2026 hapatakuwa na CCM.

Ameeeen.
Umechelewa Sana mkuu,

Written!
 
Narudia tena, machafuko pekee ndio njia ya kuleta mabadiliko ya kweli kwenye nchi hIi. Subiri uone kitakachoendelea.
Mkuu

Hakuna haja ya machafuko Ili kupata mabadiliko KWA NCHI yangu Tanzania!

Kama Mwl nyerere aliaminiwa kusimamia transformation ya TANGANYIKA kujitawala toka KWA mkoloni,Basi tambua hata sasa kuna dalili naziona za transformation ya utawala MPYA Bila ya ccm hapo mbeleni!

Namuona mtu makini ameshaanza kutema cheche zitakazo zaa moto mkubwa wa mabadiliko ya kiuongozi na kiutawala!!

Trend ya yanayotokea,majibizano ya hoja za kuhoji uhalali wa kiutendaji wa kiti kikuu ni chachu ya mabadiliko Hayo!!!

Naiona Transformation MPYA ikakamilika MAPEMA Sana kabla hata ya uchaguzi mkuu ujao!

TUSUBIRI!
 
  • Thanks
Reactions: Ame
Back
Top Bottom