Madhara ya chama kimoja kukaa madarakani muda mrefu ndio haya. Wenye nchi chukueni hatua

NAMBA MOJA AJAYE NCHINI

JF-Expert Member
Oct 29, 2019
8,520
17,426
Kushika hatamu kwa chama kimoja kwa muda mrefu huleta mazoea na uzembe wa kutowajibika ndio huleta kudumaa kwa maendeleo ya nchi na kukosa fikra mbadala za kisukuma gurudumu la maendeleo nchini.

Vitendo kama ufisadi hutamalaki na ubwanyenye wa kubweteka hii inatokana na wenye chama kupata muda mrefu wa kuratibu uchafu wao ndani ya serikali na kujimilikisha Mali za umma kama miungu watu.

Leo nchi yetu inalizwa na ufisadi uliofanywa na viongozi wa umma kwasababu tulilea ufisadi sisi wenyewe kwa kuruhusu kikundi cha aina moja kukaa madarakani kwa muda mrefu Sana na kupata muda wa kutosha wa kufanya ufisadi huo kea kutunza sheria lege lege zinazowabeba wao kushika hatamu.

Kama tungeshtuka mapema vitendo vya kifisadi visingekua na mizizi mrefu kiasi hiki!kwasababu wanasiasa wasingekua na uhakika wa chama gani kitashika Dola uchaguzi ujao Baada ya kilichopo kuangushwa wasingekua na mipango ya muda mrefu ya kipigaji.

Ukanda,mauaji,chuki za kiitikadi za vyama ni matokeo ya kuruhusu chama kimoja kushika hatamu kea muda mrefu!!Tumetengeneza kundi la watu au Koo Fulani ambazo hazidhani kama zitakua hai bila madaraka!zinadhani madaraka ni haki yao ya asili na sio haki ya watanzania wengine.

Tatizo hilo limetokana na kukosa watu wenye maono ya mbali Sana kwenye Taifa letu!!Inawezekana wenye maamuzi ya nchi yetu walishiba vya kutosha na kutiwa upofu na raha wanazopata kwa kula keki ya Taifa peke yao.

Kuna haja ya taasisi za kijasusi za nchi yetu kuratibu siasa za nchi yetu kea manufaa na maono kuliko kuwaachia wanasiasa hasa wa chama tawala kuamua hatma ya siasa zetu!!!Aina hii ya siasa ndio umefanya ufisadi na umungu watu kuzidi nchini kwetu.

Kiukweli kabisa kama wenye nchi wangekua na maono wangebadili chama ambacho kingetwaa madaraka hapo 2015 Baada ya kelele za ufisadi kwa awamu ya nne!!pia wangeratibu na aina ya mgombea ambaye wangetaka ashinde uchaguzi ule!!Lakini kosa kubwa waliwaachia wanasiasa waamue hatma yetu ambayo ndio hii imeleta ukakasi na ombwe na wingu la chuki na uadui lenye kuhitaji Mabadiliko makubwa ya uongozi yenye maumivu Sana na kujikuta hakuna namna zaidi ya kuyakumbatiamaumivu yao.

Vuta picha kama hayati jpm angeshinda uraisi hapo 2015 kwa kupitia CHADEMA chini ya uratibu wa wenye nchi unadhani teka teka ile,ua ua Ile na potea potea ile ingetokea???sidhani kama angewatesa wanachama wake wapya kwa kesi zile zisizoisha!!hata kama kwa chama hata cha CUF au nccr mambo yasingekua hivi leo.

Nadhani wenye nchi Wana la kujifunza kwamba Zama za kuacha chama kimoja kitawale kwa miaka 20 na zaidi zimepitwa na wakati!!sasa ni Zama za kuwa na siasa zisizo tabirika na kiutafiti na za kisayansi!!wakati umefika wa kutengeneza watu nje ya mfumo wa kisiasa na chama na kuwaingiza pole pole kwenye vyama ili washinde uraisi kuwa chama chochote na kuwa na siasa zisizo tabirika.

Sote tunajua demokrasia ni kuhalalisha ushindi wa kiongozi aliechaguliwa na wachache kwa Njia ya uchaguzi kama tufanyavyo kea miaka mingi!Muda umefika wa kutumia mwanya huo kuanzisha siasa na chaguzi zisizo tabirika.

Ukweli ni kwamba siasa za chama kimoja kushika madaraka kea muda mrefu zimeacha majeraha,makovu na maumivu yasiyovumilika nchini kwetu vuteni picha ya idadi ya nguvukazi na walipa kodi tuliowapoteza kwa siasa za aina hii tulizoziendekeza kwa miaka mingi.

Pigeni hesabu make na takwimu hapa jamvini.

Wenye nchi kuna haja ya kutubu kwa dhambi hii ya kukosa maono kwa nchi yetu!!Bandiko hili mkatoe kopi na kuwekwa mlangoni mwa ofisi zenu za siri kama ukumbusho wa toba wa dhambi hii kubwa.

Wenye nchi someni halafu mchukue hatua!
 
Neno kea ni typing error ni kwa !!isomeke hivyo!!ni mimi mwenzenu ninaeamini utanzania wetu haupimwi kwa itikadi za vyama bali uzalendo binafsi!pia naamini chama kingine kikishika hatamu hautokuwa mwisho wa Tanzania yetu kama wanasiasa wanavo wadanganya!!mf:-eti ukichagua upinzani kutatokea vita!!!kauli mbovu kabisa kutamkwa uchaguzi 2015!!nilishangaa Sana kauli hii!!
 
Bilaa kutokea machafuko hiki unachosema hakiwezi kutokea. Sasa hivi wananchi hawatokei tena kupiga Kura maana hawaridhiki na ccm kuendelea madarakani, ila uchaguzi ukifanyika CCM wanatangazwa washindi kwa shuruti. Hapa ni jeshi kupindua tu na tutawaunga mkono.
 
Kama Mali
 
CCM ni takataka kabisa
 
Labda wachaga pori
Ubaguzi uchaggani upo kwenye DNA. Ona sasa umeanza kubagua mpaka Wachagga wenzako.

Huko uchaggani nyumba za tope nyingi tu, tena wengine wanajengra mbao kutoka chini mpaka juu
 
Neno kea ni typing error ni kwa !!isomeke hivyo!!ni mimi mwenzenu ninaeamini utanzania wetu haupimwi kwa itikadi za vyama bali uzalendo binafsi!pia naamini chama kingine kikishika hatamu hautokuwa mwisho wa Tanzania yetu kama wanasiasa wanavo wadanganya!!mf:-eti ukichagua upinzani kutatokea vita!!!kauli mbovu kabisa kutamkwa uchaguzi 2015!!nilishangaa Sana kauli hii!!
Mimi ni mwana CCM mpaka damu yangu lakini niliamini kabisa mwaka 2015 tungebadilisha mifumo yote ndani ya chama lakini ni kiri tu aliyejaribu kufanya hivyo alionekana mwenye dhamira ya kweli kabisa sijui sababu kubwa iliyomfanya akose confidence na kuwa na hofu kiasi kile chakuogopa hadi kivuli chake...Natamani siku moja nifahamu kwanini alitawaliwa na hofu ile kuu hadi kukosa rationality...

Naamini katika Mungu kwamba tupo kwenye right truck na future yetu ni bora sana sana...I wish you could see what I see!
 
Bilaa kutokea machafuko hiki unachosema hakiwezi kutokea. Sasa hivi wananchi hawatokei tena kupiga Kura maana hawaridhiki na ccm kuendelea madarakani, ila uchaguzi ukifanyika CCM wanatangazwa washindi kwa shuruti. Hapa ni jeshi kupindua tu na tutawaunga mkono.
Usituletee uchuro hayo mambo hatujazoea sisi...Nchi yetu tutaibadili kwa amani na bila vurugu yeyote. Jeshi letu limekuwa na nidhamu ya hali ya juu kwa Jamuhuri ya Muungano usiliingize kwenye mambo maovu kama haya...Haijalishi kama unapenda au unauchukia kila uongozi watoka kwa Mungu na anakuwa na sababu zake kwanini uwe huo...Mungu ameumba wema na ubaya kwa matumizi yake binafsi
 
Usituletee uchuro hayo mambo hatujazoea sisi...
Sidhani kama ni uchuro, Tindo anaeleza hali halisi itokanayo na aina ya uongozi kama huu tulio nao.

Hao waliokumbwa na mapinduzi ya kijeshi wengi hawakupenda ila kutokana na aina ya uongozi uliokuwepo kwenye hizo nchi ikatokea hivyo.

Hapa kwetu kama uongozi uliopo hautabadilika na kufanya mambo kwa weledi, usione ajabu mapinduzi kama hayo kutokea.
Haya mambo yanaenda kisayansi..hakuna uchuro hapa.
 
Bilaa kutokea machafuko hiki unachosema hakiwezi kutokea. Sasa hivi wananchi hawatokei tena kupiga Kura maana hawaridhiki na ccm kuendelea madarakani, ila uchaguzi ukifanyika CCM wanatangazwa washindi kwa shuruti. Hapa ni jeshi kupindua tu na tutawaunga mkono.
Mawazo ya kipepo kabisa haya yashindwe kwa jina la Yesu......

.....jitahidi kusali mara kwa mara ili usimpe shetani nafasi ya kutawala fikra zako.
 
Mkuu kwani wachaga ni wananchi wa nchi gani?? tulitengeneza taasisi imara kabisa hata tukiongozwa na kabila lolote hatutahofu chochote!!tutengeneze taasisi imara tu ili usiwaogope wachaga!!!kuwaogopa ni dalili ya insecure and incompetence!!
Wanataka tuone sample Kwanza kupitia CDM.

Otherwise, huwezi kuonja sumu ili ujue kama itakuua au la.
 
Usituletee uchuro hayo mambo hatujazoea sisi...Nchi yetu tutaibadili kwa amani na bila vurugu yeyote. Jeshi letu limekuwa na nidhamu ya hali ya juu kwa Jamuhuri ya Muungano usiliingize kwenye mambo maovu kama haya...Haijalishi kama unapenda au unauvhukia kila uongozi watoka kwa Mungu na anakuwa na sababu zake kwanini uwe huo...Mungu ameumba wema na ubaya kwa matumizi yake binafsi

Narudia tena, machafuko pekee ndio njia ya kuleta mabadiliko ya kweli kwenye nchi hIi. Subiri uone kitakachoendelea.
 
Narudia tena, machafuko pekee ndio njia ya kuleta mabadiliko ya kweli kwenye nchi hIi. Subiri uone kitakachoendelea.
Kama una miguvu si uende kubomoa ukuta wa chumba chako? 😂😂😂

Wewe ndiyo wale wanaposhindwa jambo wanaona kama dunia imefika mwisho...Sahau haitakaa itokee...Tupo walinzi imara wa nchi yetu bila malipo wala tamaa zisizo na mpangilio, tuna nguvu mno japo ukituangalia tu dhaifu kiasi cha kudharaulika...Get it!
 
Back
Top Bottom