Madhara ya CCM Kuunga Mkono kila Hoja Yaanza Kujitokeza! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Madhara ya CCM Kuunga Mkono kila Hoja Yaanza Kujitokeza!

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Rich Dad, Aug 9, 2011.

 1. Rich Dad

  Rich Dad JF-Expert Member

  #1
  Aug 9, 2011
  Joined: Dec 15, 2010
  Messages: 741
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 0
  Kambi rasmi ya upinzani ilitoa mapendekezo ya kushushwa kwa bei ya mafuta kwa 50% kupitia bajeti kivuli iliyosomwa wakati wa kuanza mjadala wa bajeti ya serikali 2011/2012.<br />
  Lakini wabunge wa CCM kwa kutumia uwingi wao na attitude waliyojijengea waliibeza bajeti kivuli ya upinzani bila kufanya critical analysis kwa baadhi ya mambo.
  Sasa mambo yamegeuka, hadi imepelekea Januari Makamba kuomba kuitisha kikao cha dharura ili wabunge waweze kujadili adha ya kutopatikana kwa mafuta.
   
 2. P

  Penguine JF-Expert Member

  #2
  Aug 9, 2011
  Joined: Nov 29, 2009
  Messages: 1,226
  Likes Received: 390
  Trophy Points: 180
  mara nyingine kuunga hoja mkono by 100% siyo tu kwamba ni kutii falsafa za chama chao bali pia ni kukosa upeo wa kutambua madhara ya wanachokiunga mkono kwa 100%.

   
 3. Kamakabuzi

  Kamakabuzi JF-Expert Member

  #3
  Aug 9, 2011
  Joined: Dec 3, 2007
  Messages: 1,497
  Likes Received: 81
  Trophy Points: 145
  Nilisikia eti kamati kuu nayo imeiagiza serikali ipunguze bei ya mafuta ya taa! Hii ni ajabu na undumilakuwili. Baraza la mawaziri ambalo ndilo hupitia bajeti za wizara zote mstai kwa mstari kabla ya kuja bungeni mwenyekiti wake ni Rais JK. Huko wakakubaliana kuondoa ruzuku ili bei yake ilingane na ya diesel. Kwenye kamati kuu mwenyekiti ni huyo huyo - kulikoni?
   
 4. Inanambo

  Inanambo JF-Expert Member

  #4
  Aug 9, 2011
  Joined: Jun 26, 2011
  Messages: 2,864
  Likes Received: 1,147
  Trophy Points: 280
  nawashukuru sana wapinzani waliomo bungeni ambao hawana ndoa na CCM. Kusema ukweli hoja zao zimeleta tija na mageuzi makubwa nchi hii. BIG UP sana na msijali kuzomewa mimi niko nyuma yenu. Hayo ya mafuta hata sielewi kwa vile mimi ni mtumiaji nzuri sana wa KEROSENE kwenye vibatari na Jiko. bei yake bado iko juu sana. Mkaa nao bei mbaya kipimo cha kuchemsha maharage ROBO ni Shs 700. habari ya Nishati Bongo ni ISHU. Wabunge wa CCM hawajali kwamba vijijin KEROSENE ni ndio Source ya Mwanga. Bado kipimo kidogo 1000. Jamani maisha ni magumu tumekuwa sugu.
   
Loading...