Herbalist Dr MziziMkavu
JF-Expert Member
- Feb 3, 2009
- 42,266
- 33,039
Madhara 14 ya dawa za kupanga uzazi ambayo madaktari huwaficha wanawake.
Madhara 14 ya dawa za kupanga uzazi ambayo madaktari huwaficha wanawake
Wasichana na wanawake hutumia tembe za kupanga uzazi nyakati ambapo wameshiriki ngono bila kinga na wanahofia kuwa wanaweza kupata uja uzito ambao hawakupanga. Wengi hutumia tembe za Postinor-2 wanazozinunua kutoka kwenye maduka ya madawa huku baadhi yao wakitumia tembe za mwezi mzima za kupanga uzazi.
Kuna wale ambao hujikuta wameshiriki ngono na watu wasiowajua baada ya kunywa pombe usiku kucha na kurusha roho,
hivyo hulazimika angalau kuzuia kupata uja uzito. Hata hivyo, kuna madhara ambayo hutokana na matumizi ya dawa hizo ambazo wengi hawazijui
1. Kisunzi.
2. Alama za hedhi zinazotoka katikati ya mzunguko wa mwanamke.
3. Uchungu kwenye matiti.
4. Maumivu ya kichwa na kipandauso.
5. Kuongeza uzani.
6. Mabadiliko ya hisia
7. Kukosa kuwa na hedhi.
8. Kupungua kwa uthabiti wakati wa ngono.
9. Majimaji yanayotokea kwenye sehemu ya uzazi.
10. Kubadilika kwa jinsi mtu anavyoona kwa wanaotumia miwani.
11. Kuwa na vilia au vidonge vya damu.
12. Maumivu ya tumbo na kiuno.
13. Maumivu ya kifua, muda mfupi wa kuvuta pumzi au zote.
14. Kufura kwa miguu na mapaja na uchungu katika sehemu hizo.
ZAIDI SOMA:
Madhara ya kutumia vidonge vya uzazi wa mpango huku wanawake wakisahau njia bora ya kupanga uzazi ni kutumia kondom na kalenda tu
MADHARA YA KUTUMIA VIDONGE VYA UZAZI WA MPANGO
Serikali huwa haiwaambii ukweli wanawake hasa pale matangazo kuhusu uzazi wa mpango yanaposhika kasi kwenye Tv na Radio
Ili kuepuka kupata ujauzito, wanawake hutumia njia mbalimbali za kupanga uzazi wao ikiwa ni pamoja na utumiaji wa vidonge, vitanzi, vijiti na wengine wachache hutumia mipira wakati wa tendo la ndoa.
Njia hizi kila moja ina athari chanya na hasi na mara nyingi hutegemea na hali ya mtu anayezitumia kwani akitumia mmoja anaweza kuona madhara kadhaa lakini mwingine asione.
Katika kuchambua madharaya ya njia hizi za kupanga uzazi, tutaelezea madhara ya matumizi ya vidonge vya kupanga uzazi kwa wanawake.
Kupata kichefuchefu.
Mtumiaji anayetumia dawa hizi kwa mara ya kwanza ana uwezekano mkubwa wa kupatwa na kichefu chefu ambacho hudumu kwa muda mfupi hadi mwili utakapozoea dawa hizo. Ukitumia dawa hizi wakati wa chakula, au muda mfupi kabla ya kulala huenda ikakusaidia kupunguza hali hiyo.
Aidha, unashauriwa kuwa, endapo utaona hali hiyo imeendelea kwa muda mrefu, muone mtaalamu wa afya kwa ushauri zaidi.
Kuongeza hamu ya kula
Wakati mfumo wa homoni za oestrogen na progesterone unapobadilishwa kwa kutumia vidonge humfanya mtumiaji kuwa na njaa sana na hivyo kukufanya ule sana hali inayoweza kupelekea kuongezeka uzito. Lakini hakuna ushahidi madhubuti unaoonyesha uhusiano wa moja kwa moja kuwa dawa hizo zenyewe huongeza uzito.
Kubadilika kwa hisia (mood)
Wanawake ambao hukumbwa na matatizo ya kubalika kwa hali/hisia zao kama kuwa na hasira, kutotaka kusemeshwa, hali hiyo huongezeka pale anapotumia vidonge vya kupanga uzazi. Wanawake wa aina hii wanashauriwa kujadiliana na wenza wao kabla ya kuanza kutumia dawa hizi.
Maumivu ya kichwa
Mabadiliko ya homoni katika mwili wa mwanamke anayetumia vidonge hivi, hupelekea maumivu ya kichwa na kipandauso. Mabadiliko tofauti ya homoni hupelekea dalili tofauti tofauti za maumivu ya kichwa. Lakini maumivu na dalili hizo zitaendelea kupungua kadiri ya muda.
Kuganda wa damu
Mtumizi ya vidonge hivi wakati mwingine huwaweka wanawake katika hatari kubwa kutokana na kupelekea damu zao kuwa mabonge mabonge. Wanawake wenye matatizo haya ya damu kuwa mabonge wanashauriwa kutotumia dawa hizi kwani zitawasababishia madhara zaidi. Lakini pia kabla hujaanza kutumia dawa, unashauriwa kumuona mtaalamu wa afya.
Maziwa kuongezeka ukubwa
Vidonge hivi vinaweza kukusababishia maziwa yako kuongezeka ukubwa au kupata maumivu ya maziwa madhara ambayo yataanza kutoonekana baada ya kutumia dawa hizi kwa wiki kadhaa. Hata hivyo, kama utaona maziwa yako hayapo sawa, au maumivu yamedumu kwa muda mrefu, utahitaji kumuona mtaalamu wa afya haraka.
Kutokwa na uchafu ukeni
Baadhi ya wanawake hukumbwa na tatizo la mabadiliko ya utoaji uchafu ukeni hali ambayo huathiri kujamiiana kwao kutokana na kupungua au kuongezeka kwa muda na kiasi cha utoaji uchafu. Utoaji wa uchafu kwa njia ya uke si tatizo kwa wanawake, lakini kama utahisi kuna hali ambayo si ya kawaida, unashauriwa kwenda hospitali.
Athari hizo za vidonge tulizozitaja hap juu sio zote ni mbaya. Madhara mengine kubwa za kutumia vidonge hivyo ni pamoja na kuumwa sana na kichwa, Maumivu ya nyonga, maumivu ya kifua, uono hafifu pamoja na maumivu ya miguu au mapaja.
Endapo moja ya haya madhara makubwa tuliyoyataja hapo yatatokea, unatakiwa kumuona daktari haraka ikiambatana na kusitisha matumizi ya videonge hivyo.
Maumivu hayo yanaweza kuashiria matatizo katika kibofu, ini, damu kuwa mabonge, shinikizo la damu au hata ugonjwa wa moyo.
Vijiti, vidonge, sindano kwa ajili ya uzazi wa mpango ni hatari kwa afya ya mwanamke
Mbaya zaidi hata wanaume wanaitwa huku wakiaaminisha watu njia ya hizo si kwa ajili ya wanawake tu . Madhara ya kutumia vidonge vya uzazi wa mpango huku wanawake wakisahau njia bora ya kupanga uzazi ni kutumia kondom na kalenda tu
Pia unashauriwa kusoma
- Madhara ya kutumia vidonge vya uzazi wa mpango huku wanawake wakisahau njia bora ya kupanga uzazi ni kutumia kondom na kalenda tu