madhala ya dawa ya ukimwi iliyogunduliwa | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

madhala ya dawa ya ukimwi iliyogunduliwa

Discussion in 'JF Doctor' started by Mpangamji, Jul 16, 2010.

 1. Mpangamji

  Mpangamji JF-Expert Member

  #1
  Jul 16, 2010
  Joined: May 12, 2010
  Messages: 536
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 35
  hii dawa ya ukimwi iliyogunduliwa Marekani na kupata support ya Prof. waziri wa Afya Tanzania, kwangu mimi naiona ni hatari sana. dawa hii haitibu yaani haiondoi virus wa ukimwi badala yake inazuia virus hao wasilete madhara mwilini hivyo kila mtu atatakiwa awe na hiyo dawa kwa kuwa tutaendelea kuambukizana, baada ya hapo watasema hiyo dawa haifanyi tena kazi, hapo ndipo patakapochimbika
   
 2. Gamaha

  Gamaha JF-Expert Member

  #2
  Jul 16, 2010
  Joined: Jul 17, 2008
  Messages: 2,694
  Likes Received: 752
  Trophy Points: 280
  Tuombe Mungu tu atusaidie wajameni manake hata ukisema wasinywe wanakufa haraka, nani anapenda apoteze ndugu yake au uhai wake mwenyewe mapema. hamna
   
 3. minda

  minda JF-Expert Member

  #3
  Jul 16, 2010
  Joined: Oct 2, 2009
  Messages: 1,070
  Likes Received: 13
  Trophy Points: 135

  nijuavyo mimi serikali bado haijatoa tamko kuhusu dawa hiyo na na waziri huyo hajatamka lolote, na kama kuna thread yoyote tupatie.
   
 4. M

  Mike 1234 JF-Expert Member

  #4
  Jul 16, 2010
  Joined: Feb 23, 2009
  Messages: 1,634
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  ulichosema ni kweli kabisa ije ata kesho maana nina ndugu yangu hapa anateseka sana nawaonea huruma watoto wake wadogo we acha ni huruma tu,mmoja mzima mwingine ndo hivyo tena lkn ikija hiyo itamsaidia sana ukizingatia mtoto mwenyewe ni mkali ile mbaya darasani,mi nashuri serikali ifanye haraka kufatilia hiyo dawa,
   
 5. B

  Babuyao JF-Expert Member

  #5
  Jul 16, 2010
  Joined: Jun 6, 2009
  Messages: 1,734
  Likes Received: 29
  Trophy Points: 145
  Nadhani ndiyo maana ya dawa kuitwa chanjo. Inakujengea immunity ili isku ukijaambukizwa wale virus wasiweze kuishinda kinga ya mwili wako na kukudhuru. Kumbe hata ukiupata ukimwi kinga uliyo nayo itawafanya wale virus washindwe kuleta madhara mwilini mwako hata kama watabaki mwilini.
   
 6. roselyne1

  roselyne1 JF-Expert Member

  #6
  Jul 16, 2010
  Joined: Feb 18, 2010
  Messages: 1,369
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 0
  Mie sijaelewa hio dawa inafanyaje kazi,aliyeelewa naomba anieleweshe tafadhali.....
   
 7. M

  Mutu JF-Expert Member

  #7
  Jul 16, 2010
  Joined: Mar 30, 2008
  Messages: 1,333
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 0
  Huoni ni hatua kama unataka ya kufanya unavyotaka kungua wewe
   
 8. Abdulhalim

  Abdulhalim JF-Expert Member

  #8
  Jul 16, 2010
  Joined: Jul 20, 2007
  Messages: 16,472
  Likes Received: 125
  Trophy Points: 160
  Tamko la nini?Kwa faida ya nani na ili iweje?? Kwani ilichangia kwene utafiti??
   
 9. macho_mdiliko

  macho_mdiliko JF-Expert Member

  #9
  Jul 16, 2010
  Joined: Mar 10, 2008
  Messages: 6,434
  Likes Received: 2,303
  Trophy Points: 280
  Roselyne1
  Usibabaishwe! Hakuna dawa ya ukimwi iliyogunduliwa!!!!! Ni just a 'break through' ya reseach ya dawa ya ukimwi! Ona hizi comments za watu walivyo-respond kuhusu hii habari uchwara ya gazeti la mwananchi..

  Commentt 1:
  Comment 2:
  Comment 3:
  Kwa maoni yangu haya ndiyo mambo yanayotakiwa kuangaliwa ili gazeti lifungiwe.... na mwananchi lilistahili. MBONA DAILY NATION AMBALO LINAMILIKIWA NA HAO HAO HALIPIGII HII STORI UPATU? WAMEONA WA TZ NDIO BONGOLALA WA KUDANGANYWA?????
   
 10. Ramthods

  Ramthods JF-Expert Member

  #10
  Jul 16, 2010
  Joined: Jun 2, 2009
  Messages: 494
  Likes Received: 33
  Trophy Points: 45
  Kwanini uogope kuambukizana? Kinga ya ukimwi ipo mbona miaka nenda rudi, ni rahisi. ACHA NGONO ZEMBE.

  Ukipenda boga, penda na ua lake. Kama hutaki kuacha totoz, basi lazima ukae mkao wa kula!
   
 11. Anyisile Obheli

  Anyisile Obheli JF-Expert Member

  #11
  Jul 16, 2010
  Joined: Dec 13, 2009
  Messages: 3,304
  Likes Received: 19
  Trophy Points: 135
  hakuna dawa ya ukimwi, dawa ya ugonjwa huo ni kila mtu mme/mke, binti/kijana wa kiume, kuishi kwa kufuata maagizo ya Mungu tu hiyo ndiyo itakayo kuwa dawa ya ukimwi,

  vinginevyo hapo ni biashara tu ya Y2K
   
 12. n

  nndondo JF-Expert Member

  #12
  Jul 17, 2010
  Joined: Feb 1, 2010
  Messages: 1,250
  Likes Received: 534
  Trophy Points: 280
  Na wala hata hao watafiti hawajasema kwamba wamepata dawa hiyo sijui hao mwananchi wameelewaje kwamba hiyo ni dawa, specific wording of the press release says 'researchers have finally found a potential basis for an HIV vaccine'. mimi naamini kama kwaida ya viongozi wetu hawa waziri atakua alirukia kujibu bila kusoma hiyo press release yenyewe na kushauriana na wataalamu wake badala yake analeta confusion nchini. Ila ukweli ni kwamba tunawaombea mungu watafiti wafikie huku tunakotaka tupate kupona na hili balaa kubwa kwetu na vizazi vyetu.
   
 13. m

  matambo JF-Expert Member

  #13
  Jul 17, 2010
  Joined: May 14, 2009
  Messages: 728
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 0
  Kwanini uogope kuambukizana? Kinga ya ukimwi ipo mbona miaka nenda rudi, ni rahisi. ACHA NGONO ZEMBE.

  Ukipenda boga, penda na ua lake. Kama hutaki kuacha totoz, basi lazima ukae mkao wa kula!

  hakuna dawa ya ukimwi, dawa ya ugonjwa huo ni kila mtu mme/mke, binti/kijana wa kiume, kuishi kwa kufuata maagizo ya Mungu tu hiyo ndiyo itakayo kuwa dawa ya ukimwi,

  vinginevyo hapo ni biashara tu ya Y2K

  enyi wajinga katika medical field nani aliyewaambia kuwa watu wote waliupata ukimwi kwa kuendekeza ngono zembe au kwa kuishi kinyume na maagizo ya Mungu? niwakumbushe mtawazungumziaje wale waliopata ukimwi kutokana na blood transfusion?wewe unamfahanu ryan white aliyekuwa akitengwa kule marekani kwa kuwa na virusi vya ukimwi mpaka michael jackson alimtungia wimbo wa gone too soon alipokufa?vipi kuhusu health personell waliojiprick viungo vyao with infected sharp utensils that have been contaminated with HIV?vipi kuhusu wale wazee waliopata virusi kutokana na kujitoa kwa roho moja kulea watoto wao na wajukuu wao wagonjwa wa ukimwi kwa kuwa nyie wajinga mliwakimbia na kuwanyanyapaaa?vipi kuhusu watu waliozaliwa na virusi hivi kutokana na
  uambukizi wa kutoka kwa mama kwenda kwa mtoto?

  wanyanyapaaaji wakubwa nyie na wauaji wakubwa,wenye mawazo kama nyie
   
 14. roselyne1

  roselyne1 JF-Expert Member

  #14
  Jul 17, 2010
  Joined: Feb 18, 2010
  Messages: 1,369
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 0
  heee :A S confused:
   
 15. m

  matambo JF-Expert Member

  #15
  Jul 17, 2010
  Joined: May 14, 2009
  Messages: 728
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 0
  gazeti la mwananchi limeonyesha udhaifu mkubwa sana,ningependa serikali iwaeleweshe watanzania ukweli kuwa dawa ya kutibu UKIMWI bado haijagunduliwa ili watu wasipate false hopes
  laiti makala hiyo ingetoka kwenye gazetri halisi la kitanzania ungeona majirani namna ambavyo wangeshambulia udhaifu wa waandishi wetu ila kwa kuwa limetoka kwa gazeti la majirani wapo kimya
   
 16. Ramthods

  Ramthods JF-Expert Member

  #16
  Jul 17, 2010
  Joined: Jun 2, 2009
  Messages: 494
  Likes Received: 33
  Trophy Points: 45
  Hata hivyo, badili kichwa cha hii thread. Siyo madhala, ni madhara.
   
 17. Mpangamji

  Mpangamji JF-Expert Member

  #17
  Jul 17, 2010
  Joined: May 12, 2010
  Messages: 536
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 35
  Mwakyusa: Tumshukurmu Mungu kwa dawa ya ukimwi Send to a friend Wednesday, 14 July 2010 07:58 0diggsdigg

  [​IMG] Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii Tanzania, Profesa David Mwakyusa

  Leon Bahati
  WAKATI wanasayansi waliogundua dawa ya Ukimwi wakiweka bayana jinsi inavyofanya kazi mwili kupambana na ugonjwa huo, Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii, Profesa David Mwakyusa amemshukuru Mungu kwa taarifa za ugunduzi wa dawa hiyo.Taarifa ya kupatikana kwa dawa hiyo zilitangazwa mwishoni mwa wiki na wanasayansi wa Taasisi ya Magonjwa ya Kuambukiza na Mzio (Niaida) ya Marekani, akisema kuwa tiba hiyo inaweza kutibu ugonjwa huo hatari kwa asilimia 90, kiwango kinachoiweka dawa hiyo kwenye uwezekano mkubwa wa kupitishwa na Shirika la Afya Duniani (WHO) na hivyo kuanza kutumika rasmi.

  Dawa hiyo huchochea mwili na kuuongoza katika kujitengenezea aina ya chembechembe za kinga zenye uwezo wa kukabili virusi vya ukimwi. Chembechembe hizo zimepewa jina la kitaalamu la VRCO1 na VRCO2 ambazo utafiti wake umeonyesha kuwa zinaweza kuvikabili virusi vya Ukimwi kwa asilimia 90.

  Habari hizo, ambazo zimekuwa gumzo duniani kote, zilimfurahisha pia Waziri Mwakyusa, wakati wasomaji wa Mwananchi walikuwa wakituma maoni yao kuzungumzia matokeo ya utafiti wa dawa hiyo, wengi wakifurahia kuwa sasa "wamewekwa huru".

  Akizungumza na Mwananchi, Prof Mwakyusa alisema: "Serikali imekuwa ikifanya juhudi mbalimbali katika kuhakikisha kwamba wananchi wake wanapata huduma za tiba hata kama ni ghali kiasi gani.

  "Kama ni kweli dawa hiyo imepatikana, ni jambo la kumshukuru Mungu kwa kuwa Ukimwi ni ugonjwa ambao umeiathiri sana dunia."

  Alisema serikali imekuwa ikitumia mamilioni ya fedha kupambana na ugonjwa huo na hivyo kuwezesha dawa nyingi ghali duniani zinazopunguza makali ya ugonjwa huo na kutibu magonjwa sugu kutolewa bure kwa wananchi.

  Alitoa mfano wa dawa hizo kuwa ni zile za kutibu malaria maarufu kwa jina la Alu, dawa za kutibu kifua kikuu na zile za kupunguza makali ya ukimwi.

  "Na hata kama hizo za kutibu ukimwi zitakuwa zimepatikana, bado mataifa makubwa yana wajibu wa kuhakikisha zinaweza kuwafikia kirahisi watu katika nchi masikini," alisema Profesa Mwakyusa.

  Kwenye chumba cha habari cha Mwananchi, wasomaji walikuwa wakipiga simu kuelezea kufurahishwa na taarifa hiyo huku wengine wakitoa maoni yao kwenye mtandao, wengi wakisifu matokeo ya utafiti huo na wengine wakisema kuwa bado kuna safari ndefu.

  Nchini Marekani, wanasayansi wa Niaida waliweka bayana namna dawa hiyo inavyoweza kufanya kazi katika mwili wa binadamu wakati wa kupambana na ugonjwa huo hatari.

  Niaida imetoa taarifa hiyo kufuatia taarifa iliyotangazwa wiki iliyopita kwamba wamegundua chembechembe za kinga ambazo zinaweza kutumika kutibu ugonjwa wa ukimwi kwa asilimia 90.

  Mkurugenzi wa Niaida, Dk Anthony Fauci alisema katika taarifa kwenye mtandao wa taasisi hiyo kwamba dawa waliyoigundua siyo ya kwenda kuua moja kwa moja virusi vya Ukimwi kwenye mwili wa binadamu, bali ni kuchochea mwili na kuuongoza katika kujitengenezea aina ya chembechembe za kinga zenye uwezo wa kukabili virusi vya ukimwi.

  Dk Fauci alisema kuwa chembechembe hizo, VRCO1 na VRCO2, zinapambana tu na virusi vya Ukimwi jambo ambalo linawapa faraja kuwa chembechembe hizo haziwezi kusababisha madhara kwa mwili wa binadamu.

  Mtaalamu huyo alieleza kwamba kinachofanywa na chembechembe za kinga za VRCO1 na VRCO2 kwenye mwilini binadamu, ni kuvibana virusi vya Ukimwi na kuvifanya vishindwe kuendelea kushambulia seli nyeupe za damu.

  Kwa kawaida virusi vya Ukimwi hushambulia seli nyeupe za damu ambazo ni muhimu katika kusaidia mwili kujikinga na maradhi ama kwa jina jingine la kitaalamu CD4, ambako virusi vya Ukimwi hugeuza kuwa makazi yake.

  Kila seli nyeupe inayoshambuliwa, wataalamu wanasema, hufa baada ya kutumika kuzalisha virusi wengine na mzunguko huo huendelea hadi mwili unapojikuta umepungukiwa na kinga kiasi cha kushindwa kuhimili vishindo vya maradhi ya kawaida.

  Wataalamu wanasema hali hiyo ndiyo inayomfanya mwathirika wa Ukimwi kufa.

  Dk Fauci alisema Chembechembe za VRCO1 na VRCO2 hubana mashambulizi ya virusi vya Ukimwi kiasi cha kushindwa kuendelea na uharibifu wa CD4.

  Kwa sababu hiyo, alisema dawa watakayoitoa katika hatua ya kwanza kupitia chanjo ni kwa ajili ya kuufundisha mwili namna ya kutengeneza chembechembe za VRCO1 na VRCO2 ambazo zitakabiliana na virusi wa ukimwi.

  "Kwa kutumia teknolojia tuliyogundua tutatengeneza aina ya chanjo ambayo kazi yake itakuwa ni kuufundisha mwili namna ya kutengeneza chembechembe za kinga aina ya VRCO1 ambazo zitakuwa na uwezo wa kupambana na virusi vya ukimwi," alisema Dk Fauci.

  Wanasayansi wa Niaida walioshiriki kwenye utafiti huo ni Dk Peter Kwong, Dk John Mascola na Dk Gary Nabel.

  Wataalamu hao wanaelezewa kuwa waliongoza timu mbili ambazo ziliendesha utafiti huo ambao ulihusisha damu za waathirika kutoka karibu kona zote za dunia.

  "Tulitumia utaalamu wetu kujenga mazingira yote ya virusi wa Ukimwi na ndio tukaweza kufahamu namna ya kujenga mazingira ya kudhibiti virusi hivyo," alisema mmoja wa wajumbe wa jopo la madaktari hao waandamizi, Dk Nabel.

  Aliongeza: "Haikuwa kazi rahisi kwa sababu virusi vya Ukimwi vina tabia ya kujibadilishabadilisha. Na hii ndiyo imekuwa ikiwapa taabu wataalamu wengi katika kupata tiba.

  "Kujibadilishabadilisha huko kumefanya dunia kuwa na aina mbalimbali za virusi. Utafiti wetu umewezesha kutengeneza mazingira ya kukabiliana na namna zote za virusi kuweza kujigeuzageuza."

  Isitoshe Dk Nabel alisema chembechembe za kinga za VRC01 na VCR02 zina uwezo wa kupenya mazingira yote ambayo CD4 za mwili zinaweza kupatikana.

  Dr Mascola yeye alielezea ufanyakazi wa VCR01 na VCR02 kuwa ni wa ajabu kwa sababu zinapambana na aina zote za utendaji wa virusi vya Ukimwi.

  Wataalamu hao walisema VRC01 na VRC02 haviingilii itendaji kazi wa seli kwa namna yoyote ile bali kukabiliana na harakati za virusi vya ukimwi.
  Dk Faci alisema haya ni maendeleo mazuri katika kipindi hiki ambacho waathirika wa Ukimwi wamekuwa wakitumia tu dawa za kutuliza makali ya virusi.

  Maelezo ya wataalamu ni kwamba anayetumia dawa za kupunguza makali ya virusi vya Ukimwi atatumia maisha yake yote na huwa hazitibu.
  Lakini katika ugunduzi wa dawa yao, Dk Fauci alisema binadamu atapatiwa chanjo hiyo kwa mara moja na itatosha kabisa kuuweka mwili wake katika kuandaa majeshi ambayo yatakabiliana na virusi.

  Tayari baadhi ya wataalamu wamekiri kuwa ugunduzi huo wa Niaida umeleta mapambazuko ya tiba ya ugonjwa huo na mojawapo ni Mamlaka ya Chakula na Dawa Marekani ambayo imesema kuwa dawa hiyo haitakuwa na madhara yoyote kwa binadamu.

  Dk fauci amewahi kuongoza Taasisi ya Taifa ya Afya (NIH) ya Marekani kuanzia mwaka 1968 na kuaniza 1974 aliteuliwa kuongoza vitengo mbalimbali maalumu vya tiba nchini humo.

  Aliteuliwa kuwa mkuu wa kitengo cha utafiti wa tiba cha Niaida mwaka 1980 na mwaka 1984 akateuliwa kuwa mkurugenzi wa taasisi hiyo, nafasi ambayo anaishikilia hadi sasa.

  Add this page to your favorite Social Bookmarking websites
  [​IMG] [​IMG] [​IMG] [​IMG] [​IMG] [​IMG] [​IMG] [​IMG] [​IMG] [​IMG]
  Last Updated on Thursday, 15 July 2010 08:17
   
 18. Mpangamji

  Mpangamji JF-Expert Member

  #18

  “Tulitumia utaalamu wetu kujenga mazingira yote ya virusi wa Ukimwi na ndio tukaweza kufahamu namna ya kujenga mazingira ya kudhibiti virusi hivyo," alisema mmoja wa wajumbe wa jopo la madaktari hao waandamizi, Dk Nabel.

  Aliongeza: "Haikuwa kazi rahisi kwa sababu virusi vya Ukimwi vina tabia ya kujibadilishabadilisha. Na hii ndiyo imekuwa ikiwapa taabu wataalamu wengi katika kupata tiba.

  "Kujibadilishabadilisha huko kumefanya dunia kuwa na aina mbalimbali za virusi. Utafiti wetu umewezesha kutengeneza mazingira ya kukabiliana na namna zote za virusi kuweza kujigeuzageuza."

  Isitoshe Dk Nabel alisema chembechembe za kinga za VRC01 na VCR02 zina uwezo wa kupenya mazingira yote ambayo CD4 za mwili zinaweza kupatikana.

  Dr Mascola yeye alielezea ufanyakazi wa VCR01 na VCR02 kuwa ni wa ajabu kwa sababu zinapambana na aina zote za utendaji wa virusi vya Ukimwi.

  Wataalamu hao walisema VRC01 na VRC02 haviingilii itendaji kazi wa seli kwa namna yoyote ile bali kukabiliana na harakati za virusi vya ukimwi.
  Dk Faci alisema haya ni maendeleo mazuri katika kipindi hiki ambacho waathirika wa Ukimwi wamekuwa wakitumia tu dawa za kutuliza makali ya virusi.

  Maelezo ya wataalamu ni kwamba anayetumia dawa za kupunguza makali ya virusi vya Ukimwi atatumia maisha yake yote na huwa hazitibu.
  Lakini katika ugunduzi wa dawa yao, Dk Fauci alisema binadamu atapatiwa chanjo hiyo kwa mara moja na itatosha kabisa kuuweka mwili wake katika kuandaa majeshi ambayo yatakabiliana na virusi.

  Tayari baadhi ya wataalamu wamekiri kuwa ugunduzi huo wa Niaida umeleta mapambazuko ya tiba ya ugonjwa huo na mojawapo ni Mamlaka ya Chakula na Dawa Marekani ambayo imesema kuwa dawa hiyo haitakuwa na madhara yoyote kwa binadamu.

  Dk fauci amewahi kuongoza Taasisi ya Taifa ya Afya (NIH) ya Marekani kuanzia mwaka 1968 na kuaniza 1974 aliteuliwa kuongoza vitengo mbalimbali maalumu vya tiba nchini humo.

  Aliteuliwa kuwa mkuu wa kitengo cha utafiti wa tiba cha Niaida mwaka 1980 na mwaka 1984 akateuliwa kuwa mkurugenzi wa taasisi hiyo, nafasi ambayo anaishikilia hadi sasa.

  Add this page to your favorite Social Bookmarking websites
  [​IMG] [​IMG] [​IMG] [​IMG] [​IMG] [​IMG] [​IMG] [​IMG] [​IMG] [​IMG]
  Last Updated on Thursday, 15 July 2010 08:17
   
 19. Raia Fulani

  Raia Fulani JF-Expert Member

  #19
  Jul 17, 2010
  Joined: Mar 12, 2009
  Messages: 10,220
  Likes Received: 83
  Trophy Points: 145
  Watu wengine hovyo sana. Wanaishi upande wa hasi maisha yao yote wakijifanya kukosoa kila hoja. Wengine mjifunze na kusifia pia kha!
   
 20. minda

  minda JF-Expert Member

  #20
  Jul 19, 2010
  Joined: Oct 2, 2009
  Messages: 1,070
  Likes Received: 13
  Trophy Points: 135

  kuhusu dawa husika; kwa faida ya watanzania;ili kujua kama inafaa au la; serikali bila shaka haikuchangia kwenye utafiti husika lakini ni kazi ya serikali kupitia wizara ya afya kwamba kila dawa iliyogunduliwa inafaa kweli kwa watzn.
   
Loading...