Rev. Kishoka
JF-Expert Member
- Mar 7, 2006
- 4,526
- 1,529
Najiuliza.. Leo mwanasiasa anakuja jimboni na kusema nitawaletea pikipiki, nitanunua lori, na wananchi tunashangilia na kumpa kura zetu kwa kuwa kaahidi kutuletea pikipiki na lori.
Leo chama kinasema tutamenunua ndege na kujenga daraja, nasi twashangilia kwa nguvu na kutoa dhamana ya kura zetu kuwa sasa tumepata uongozi!
Lakini tunapouliza kwa undani sera na mipango imara ya kutusaidia kuchangia uzalishaji na pato la taifa kama Wakulima, wavuvi, wafugaji, wahunzi, wafanyabiashara, wafanyakazi, wanamichezo wasanii, na fani nyingine.... hatusikii msisimko wa namna gani mipango inafanywa kuhakikisha tunashiriki kwa dhati kwa juhudi na maarifa kuzalisha mali na kuchangia pato la Taifa!
Leo kuulizia maslahi na vitendea kazi vya waalimu ili Taifa liwe na uzao na vizazi endelevu vyenye weledi na ufahamu wa mambo na kuwa washiriki wakuu wa ujenzi wa Taifa ni kosa na ni rahisi kuitwa kuwadi wa mabeberu na kunyang'anywa uzalendo wako unaoangalia hatima ya vizazi vijavyo.
Lini tutaachana na kukoshwa na ahadi ya vitu ambavyo kiuhalisia havitusaidii moja kwa moja? kama mpaka leo hii pato langu kama mkulima ni lilelile la tangu 2013 na nabahatisha kesho itakuwaje, iweje nishangilie kununuliwa ndege, kujenga vitu huku mahitaji yangu ya muhimu na lazima hayapewi kipaumbele?