Madhaifu na maradhi ya Ujinga, Umasikini, Unyonge, na Utegemezi wetu!

Rev. Kishoka

JF-Expert Member
Joined
Mar 7, 2006
Messages
4,536
Points
2,000

Rev. Kishoka

JF-Expert Member
Joined Mar 7, 2006
4,536 2,000
Najiuliza.. Leo mwanasiasa anakuja jimboni na kusema nitawaletea pikipiki, nitanunua lori, na wananchi tunashangilia na kumpa kura zetu kwa kuwa kaahidi kutuletea pikipiki na lori.
Leo chama kinasema tutamenunua ndege na kujenga daraja, nasi twashangilia kwa nguvu na kutoa dhamana ya kura zetu kuwa sasa tumepata uongozi!

Lakini tunapouliza kwa undani sera na mipango imara ya kutusaidia kuchangia uzalishaji na pato la taifa kama Wakulima, wavuvi, wafugaji, wahunzi, wafanyabiashara, wafanyakazi, wanamichezo wasanii, na fani nyingine.... hatusikii msisimko wa namna gani mipango inafanywa kuhakikisha tunashiriki kwa dhati kwa juhudi na maarifa kuzalisha mali na kuchangia pato la Taifa!

Leo kuulizia maslahi na vitendea kazi vya waalimu ili Taifa liwe na uzao na vizazi endelevu vyenye weledi na ufahamu wa mambo na kuwa washiriki wakuu wa ujenzi wa Taifa ni kosa na ni rahisi kuitwa kuwadi wa mabeberu na kunyang'anywa uzalendo wako unaoangalia hatima ya vizazi vijavyo.

Lini tutaachana na kukoshwa na ahadi ya vitu ambavyo kiuhalisia havitusaidii moja kwa moja? kama mpaka leo hii pato langu kama mkulima ni lilelile la tangu 2013 na nabahatisha kesho itakuwaje, iweje nishangilie kununuliwa ndege, kujenga vitu huku mahitaji yangu ya muhimu na lazima hayapewi kipaumbele?
 
Mwalimu

JF-Expert Member
Joined
Aug 21, 2008
Messages
1,533
Points
1,500

Mwalimu

JF-Expert Member
Joined Aug 21, 2008
1,533 1,500
Mkuu @Rev. Kishoka

Hapo ndipo utakapoona madhara ya ukosefu wa elimu ya uraia kwa wananchi. Wengi wetu hatuna ufahamu na uelewa kuhusu wajibu wetu kwa nchi na zaidi haki zetu tunazopaswa kuzipata na kuzidai pale zinapokosekana kutoka kwa wale tunaowaopa dhamana kutuongoza. Tunaumia na kupigika lakini hatuna uthubutu wa kuwawajibisha wale ambao wamesababisha tufikie hapo tulipo sana sana tunaishia kusema ni kudra za mwenyezi mungu. Matokeo yake watawala hawaheshimu wala kuwaogopa wapiga kura wanajua wanaweza kuvuruga mambo kadiri wapendavyo lakini ikifika wakati wa uchaguzi wakitoa ahadi chache hata za uongo ukijumlisha na tshirt na khanga inatosha kuwapa kura za kubaki madarakani.
 
TUJITEGEMEE

JF-Expert Member
Joined
Nov 6, 2010
Messages
14,996
Points
2,000

TUJITEGEMEE

JF-Expert Member
Joined Nov 6, 2010
14,996 2,000
Shida kubwa ipo hapo kwenye madhaifu na maradhi ya Utegemezi. Yaani Utegemezi ndiyo hasa unaupa viburi Ujinga, Umaskini na Unyonge. Utegemezi ndiyo kamada wa maadui ujinga, umaskini, na unyonge. Tukiweza kumshughulikia kamanda huyu Utegemezi kikosi hiki cha maadui kitasambaratika.

Njia ya kwanza ya kushughulikia na kumdhibiti na kumuondoa kabisa huyu kamanda Utegemezi ni kuhakikisha sisi sote tunakuwa na imani kuwa tunaweza kupanga, kuamua na kutekeleza mambo yetu ya msingi sisi wenyewe. Hii imani iingie vichwani mwetu kabisa kabisa...na yeyote anayekaidi imani hii tutumie diplomasia kumuaminisha mara mbili ikishindikana mara ya tatu tutumie nguvu kumuaminisha!!!

Ngoja niishie hapa kwanza.
 
Nguruvi3

Platinum Member
Joined
Jun 21, 2010
Messages
13,491
Points
2,000

Nguruvi3

Platinum Member
Joined Jun 21, 2010
13,491 2,000
"Rev. Kishoka, post: 30245048, member: 18"]Najiuliza.. Leo mwanasiasa anakuja jimboni na kusema nitawaletea pikipiki, nitanunua lori, na wananchi tunashangilia na kumpa kura zetu kwa kuwa kaahidi kutuletea pikipiki na lori.
Na wananchi wanaahidiwa gari la kubeba maiti wanashangilia badala ya kushangalia huduma za afya zitakazozuia vifo na kutohitajika gari la kubeba maiti
Siku hizi wanasiasa wanamsemo wao ''Niwaletee maendeleo'' . Kauli hii ni ya kuudhi na kudhalilisha sana
Lini maendeleo yamekuwa lumbesa la mihogo au kontena la mitumba kutoka bandarini!
Lakini tunapouliza kwa undani sera na mipango imara ya kutusaidia kuchangia uzalishaji na pato la taifa kama Wakulima, wavuvi, wafugaji, wahunzi, wafanyabiashara, wafanyakazi, wanamichezo wasanii, na fani nyingine.... hatusikii namna gani mipango inafanywa kuhakikisha tunashiriki kwa dhati kwa juhudi na maarifa kuzalisha mali na kuchangia pato la Taifa!
Ni kwasababu bajeti yetu inategemea kodi za sigara na bia
Tukiwa na bahari na maziwa mengi kwanini uvuvi usiwe zaidi ya utalii?
Ukiwasikiliza wale wa njengoni Dodoma na nguvu za kubishana na mgonjwa pengine unaweza kupata jibu kwanini Wachina wanakuja kuvua samaki kwetu na kwanini hatuwezi kuwa wasafirishaji wakubwa wa samaki
Leo kuulizia maslahi na vitendea kazi vya waalimu ili Taifa liwe na uzao na vizazi endelevu vyenye weledi na ufahamu wa mambo na kuwa washiriki wakuu wa ujenzi wa Taifa ni kosa na ni rahisi kuitwa kuwadi wa mabeberu na kunyang'anywa uzalendo wako unaoangalia hatima ya vizazi vijavyo.
Kuna hoja inayosemwa tena hata mabalozi wetu wanachangia kwa nguvu, kwamba, vijana wanasoma bure darsa la kwanza hadi Form four. Ni jambo jema, lakini je, kuna ubora wa elimu unaokidhi haja ya nyakati?
Hatukujifunza na uanzishwaji wa shule za kata bila vitendea kazi na Walimu, nadhani tunarudi kule kule
Lini tutaachana na kukoshwa na ahadi ya vitu ambavyo kiuhalisia havitusaidii moja kwa moja? kama mpaka leo hii pato langu kama mkulima ni lilelile la tangu 2013 na nabahatisha kesho itakuwaje, iweje nishangilie kununuliwa ndege, kujenga vitu huku mahitaji yangu ya muhimu na lazima hayapewi kipaumbele?
Ukitaka kumuuzi mwanadamu mnyime elimu. Elimu si kwa ajira, ni maarifa yanayompa mtu uwezo wa kujitambua
 
Rev. Kishoka

JF-Expert Member
Joined
Mar 7, 2006
Messages
4,536
Points
2,000

Rev. Kishoka

JF-Expert Member
Joined Mar 7, 2006
4,536 2,000
Na wananchi wanaahidiwa gari la kubeba maiti wanashangilia badala ya kushangalia huduma za afya zitakazozuia vifo na kutohitajika gari la kubeba maiti
Siku hizi wanasiasa wanamsemo wao ''Niwaletee maendeleo'' . Kauli hii ni ya kuudhi na kudhalilisha sana
Lini maendeleo yamekuwa lumbesa la mihogo au kontena la mitumba kutoka bandarini!
Ni kwasababu bajeti yetu inategemea kodi za sigara na bia
Tukiwa na bahari na maziwa mengi kwanini uvuvi usiwe zaidi ya utalii?
Ukiwasikiliza wale wa njengoni Dodoma na nguvu za kubishana na mgonjwa pengine unaweza kupata jibu kwanini Wachina wanakuja kuvua samaki kwetu na kwanini hatuwezi kuwa wasafirishaji wakubwa wa samaki
Kuna hoja inayosemwa tena hata mabalozi wetu wanachangia kwa nguvu, kwamba, vijana wanasoma bure darsa la kwanza hadi Form four. Ni jambo jema, lakini je, kuna ubora wa elimu unaokidhi haja ya nyakati?
Hatukujifunza na uanzishwaji wa shule za kata bila vitendea kazi na Walimu, nadhani tunarudi kule kule
Ukitaka kumuuzi mwanadamu mnyime elimu. Elimu si kwa ajira, ni maarifa yanayompa mtu uwezo wa kujitambua
Mkuu naomba nichomekee kitu...

How do we build a developing country and create a sustainable and strong middle class? Je kwenye template za ilani za vyama kuna blue print ya kufikia hapo kwenye developing country yenye strong middle class kutumia nguvu na rasilimali zetu wenyewe ? not misaada? au nguvu za wawekezaji?
 
Nguruvi3

Platinum Member
Joined
Jun 21, 2010
Messages
13,491
Points
2,000

Nguruvi3

Platinum Member
Joined Jun 21, 2010
13,491 2,000
Mkuu naomba nichomekee kitu...

How do we build a developing country and create a sustainable and strong middle class? Je kwenye template za ilani za vyama kuna blue print ya kufikia hapo kwenye developing country yenye strong middle class kutumia nguvu na rasilimali zetu wenyewe ? not misaada? au nguvu za wawekezaji?
Mkuu hakuna taifa linalofanikiwa bila kuwa na nyenzo muhimu ambayo ni Elimu. Kwa makosa au kutoelewa baadhi wanadhani elimu ni kwa kupata ajira
Tatizo lipo nchi zetu ambazo tunatoa elimu bila elimu ya maarifa

Kwa nchi za wenzetu mtoto anakwenda shule si kusoma namba za hesabu au vinginevyo bali kupata maarifa ya maisha. Utakuta mtoto hawezi hesabu rahisi sana lakini anajua kwanini anapaswa kunawa mikono, kwanini anaugua na anaweza kujikinga vipi na matatizo hayo

Tujiulize kwanini ukitaka kuona mgonjwa wa kipindu pindu unatakiwa kwenda Buguruni!
Kwanini siyo masaki au Oysterbay! kwanini siyo Sinza au Mbezi beach

Ukiwa na elimu ya kawaida huhitaji hospitali za kutibu kuhara , utapiamlo au malaria
Hoja hapa ni kuwa ukiwa na elimu utaondoa ujinga hutakuwa na maradhi au magonjwa, utalekea kufuta umasikini

Gharama za kutibu maradhi ya kuambukiza (communicable disease) ni kubwa na zisizo na ulazima ikiwa watu watapewa elimu ya maarifa kuanzia utotoni

Elimu inasaidia watu ujitambua na kwamba badala ya kushangilia gari la kubeba maiti watahoji kuhusu zahanati au kituo chao cha afya kisivyokidhi mahitaji yao.

Elimu inasaidia watu kutambua ukweli, kupanga mipango yao na kukataa mipango ya kupandikizwa. Elimu inawapa wahusika ''ownership' ya fate yao kwa mantiki na hata nguvu

Tumejadiliwa kuwa na arable land isiyo na mipaka kwa ukubwa, maziwa, bahari na madini
Kwasababu wengi wa wananchi wetu hawana elimu, uwezo wa kutumia rasilimali hizo haupo

Vyama vya siasa havina template ya kufikia middle class. Siyo CCM au upinzani
Laiti kungekuwa na template CCM miaka 50 isingehaki kama ilivyo sasa

Sasa tunafikia vipi middle class? Pakuanzia ni elimu ili watu wajitambue, waitumie kupambana na ujinga, maradhi na umasikini ili kutoa nafasi ya kuzitumia rasilimali zetu lukuki kikamilifu

Katika kujitambua kielimu, wananchi wangekuwa na uwezo wa kuwawajibisha waliowapa dhamana ya kupanga mipango yao iwe Dodoma au kwingineko
Kupitia hili kungekuwepo na ushindanishi wa sera kwa template na siyo kofia na khanga
 
Mwalimu

JF-Expert Member
Joined
Aug 21, 2008
Messages
1,533
Points
1,500

Mwalimu

JF-Expert Member
Joined Aug 21, 2008
1,533 1,500
Tunajinyima vyuma vinakaza, ili kutengeneza maisha ya baadae miladi anayoanzisha jiwe yote faida itaonekana kwa watoto wetu.
Miradi ya Ndege, SGR, Stieglers Gorge itanufaisha vipi watoto wetu? Itachangia vipi kuhakikisha wanapata elimu na afya bora? Fafanua tafadhali...
 
Thread starter Similar threads Forum Replies Date
Shayu Great Thinkers 0

Forum statistics

Threads 1,390,254
Members 528,131
Posts 34,047,390
Top