Madereva wahuni wanatumaliza, wanaongeza idadi ya walemavu na umaskini Tanzania! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Madereva wahuni wanatumaliza, wanaongeza idadi ya walemavu na umaskini Tanzania!

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Magobe T, Mar 23, 2011.

 1. M

  Magobe T JF-Expert Member

  #1
  Mar 23, 2011
  Joined: Mar 19, 2008
  Messages: 2,663
  Likes Received: 200
  Trophy Points: 160
  Ingawa mara nyingi watu wanasema ajali haina kinga, mimi nasema ajali nyingi zinazotokea hapa nchini zina kinga, ambayo ni kuendesha gari kwa kuheshimu sheria za barabarani na kwa uangalifu. Kama idadi kubwa ya madereva watazingatia haya, wataweza kupunguza ajali nyingi sana! Kungekuwa na mfumo mzuri wa kuwathibiti madereva wahuni (wanaoendesha magari kihuni) tungeweza kuzuia ajali nyingi sina.

  Lakini kuendelea kuhuzunika na kutoa ubani kwa wafiwa hakusaidii kitu kama taifa linaendelea kupoteza raslimali watu kila siku kutokana na ajali za barabarani na majini na kufanya wanaosalimika katika ajali hizo kuwa na ulemavu wa kudumu na wao wenyewe kuwa tegemezi. Ajali iliyotokea huko Morogoro juzi na ajali zingine zinazotokea hapa nchini zinatutia huzuni sana. Inasikitisha!

  Ombi langu kwa wabunge wetu ni kuwasilisha mswada bungeni ili Sheria ya Usalama Barabarani ifanyiwe marekebisho na kumfanya dereva anayesababisha ajali kwa uzembe wake awajibike zaidi - ikiwa ni pamoja na kulipa fidia (na kama hana hela afanye kazi za kijamii ili hela hiyo ipelekwe kwenye familia za walioachwa na wapendwa wao au majeruhi) na kuwa na kesi ya kusababisha kifo/vifo au ulemavu wa muda au wa kudumu kwa majeruhi.

  Ili kuwathibiti wenye magari wasiwaajiri madereva wahuni kwa kukwepa kuwalipa madereva wazuri mshahara mzuri, hawa nao wawajibike 'vicariously'. Inawezekana sheria ya zamani inasema hivi lakini ingepewa meno zaidi. Kitu kingine ni kubeba abiria kulingana na uwezo wa gari na siyo tamaa ya mwenye gari, dereva au kondakta. Lakini kwa hali ilivyo sasa hivi, abiria na mizigo wana thamani sawa. Hebu angalia magari ya abiria yanavyojazwa watu utafikiri ni kokoto! Hii ni hatari sana!

  Vilevile speed ya magari ithibitiwe! Mbona Ulaya magari mengi yanaenda mwendo unaokubalika kisheria lakini hapa kwetu sivyo? Jamani, inasikitisha sana na hasa haya magari ya daladala kuona yanaendeshwa na madereva na makondakta wahuni (baadhi yao wakiwa wala unga, wapiga debe)! Hivi kwa nini serikali haliweki mfumo mzuri wa kuwathibiti hawa wahuni wanaotuangamiza au kutufanya tuwe na vilema vya kudumu kila siku?
   
 2. saragossa

  saragossa JF-Expert Member

  #2
  Mar 23, 2011
  Joined: Jan 3, 2011
  Messages: 2,107
  Likes Received: 104
  Trophy Points: 160
  Mkuu tatizo serikali na wahusika wake wako bize kubadili sheria ambazo zitawanufaisha, kama sheria za manunuzi ya uma, hii itakuwa ngumu sana kudhibiti mambo mengine ambayo yanawagusa watanzania moja kwa moja.

  Vile vile udhibiti wa viwango bora vya magari ya kusafirisha abiria nalo ni jambo muhimu sana, kitu ambacho serikali imekuwa ikicheza makida makida kwa muda mrefu sana!

  Embu angalia hizo picha kwenye attachment utaelewa naongelea nini.

  Kingine ni kuwa na utaratibu wa kutosha kwa kutoa leseni za kuendeshea....hapa kila mmoja atakubaliana na mimi kwamba Tanzania, watu wengi wanaanza kujifunza kuendesha magari baada ya kupata leseni. Yaani leseni wanaletewa nyumbani, hata ukiwa kipofu au mlemavu au kiziwi, leseni unapata kwa kiulaini mno, coz presence yako pale mayfair kwenye leseni mpya haina uzito

  Nawaachia wana JF waendelee kuchangia!

  Alamsiki
   

  Attached Files:

 3. N

  Ntandalilo Member

  #3
  Mar 23, 2011
  Joined: Mar 15, 2011
  Messages: 96
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Its so scary mkuu.............. We real need to act haya mambo yabadilike
   
 4. h

  housta Senior Member

  #4
  Mar 23, 2011
  Joined: May 25, 2009
  Messages: 160
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 33
  Asilimia zaidi ya 50 ya magari yaliyopo barabarani hayafai kutembea.Kwa nini tusianzishe mfumo wa kupima magari kila mwaka na kuyapa leseni ya kutembea?leseni hii iwe centralised nchi nzima na Ministry of Transport ndiyo iwe wakala wa hizi leseni.Kwani road license ina kazi gani?Magari yanatakiwa kupita kwenye system maalum kuyapima kuanzia mikanda mpaka bolt and nut zote zilizo kwenye gari.Kuwe na official centres za kufanyi haya yote.Tuanzishe point system as well.Ukikutwa unaendesha umelewa,utolewe points kwenye license yako pamoja na faini na kufikishwa mahakamani.TRA should collect all the moneys collected from all these.Kwa nini tunaogopana?Sheria za uwajibikaji zinabidi zianziswe kuokoa maisha ya yetu sote na siyo kuuana kiuzembe.
   
 5. saragossa

  saragossa JF-Expert Member

  #5
  Mar 23, 2011
  Joined: Jan 3, 2011
  Messages: 2,107
  Likes Received: 104
  Trophy Points: 160
  wakati tunaendelea na huu mjadala, watu watatu wamekufa hapo hapo, baada ya canter kugongana na basi la lucky star uso kwa uso, wakati basi hilo lilkikwepa mwendesha baiskeli, huko mikumi leo SOURCE: RADIO ONE
   
Loading...