JanguKamaJangu
JF-Expert Member
- Feb 7, 2022
- 2,308
- 5,460
Madereva wa taxi za mitandao (Uber na Bolt) wameamua kuandamana mpaka makao makuu ya Mamlaka ya Udhibiti Usafiri Ardhnj(LATRA), kudai kupandishwa kwa bei elekezi ambazo licha ya kupandishwa wahusika bado hawazifanyii kazi hali hiyo inatokana na kuendelea kupanda kwa bei ya mafuta
Source: Dar Mpya
==========================================
Madereva wa taksi za mitandao wameandamana mpaka makao makuu ya Mamlaka ya Udhibiti Usafiri Ardhini (LATRA) Jijini Dar es Salaam kudai kupandishwa kwa bei elekezi ambazo licha ya kupandishwa bado kuna wahusika awazifanyii kazi hali hiyo inatokana na kuendelea kupanda kwa bei ya mafuta.
Madereva hao ambao ni wanachama wa Chama cha Madereva wa Mtandaoni (Tanzania Online Drivers Association - TODA) wamedai kuwa wamiliki wa huduma ya Uber na Bolt ndiyo ambao hawataki kupandisha bei ya nauli kitu ambacho kinawaumiza wao.
"Tumekuja LATRA kwa kuwa wao ndiyo waliowapa leseni Uber na Bolt, kuna App nyingine zimeshaongeza bei ya nauli, lakini wao hawataki, hivyo wateja hawawezi kwenda kwenye App yenye bei kubwa.
"Tunataka LATRA wafanye maamuzi, tulikuwa nao leo asubuhi (Aprili 12, 2022) pale Leaders Club, tukashindwana kwa kuwa wao wanaishia kusema wamewaandikia Uber na Bolt barua, kila siku hivyohivyo, ndiyo maana tumewafuata ofisini kwao watuleleze vizuri.
"Muda huu kuna wenzetu wachache tumewachagua wameingia ndani wanazungumza na viongozi, tunasubiri majiu yao," alisema dereva mmoja wa walioandamana.