Madereva wa mabasi ya Khandahar yanayofanya safari mikoa ya Singinda, Manyara na Arusha wako very rough

Architect E.M

JF-Expert Member
Nov 15, 2010
1,211
1,360
Za jioni wakuu,

Madereva wa hii kampuni wako very rough. Kuna siku mmoja aliwahi kuikwaruza gari yangu halafu akakimbia..

Leo nimeshuhudia overtake mbaya sana kwenye corner.Basi no. T 575 BVD ikitokea Babati kuelekea Arusha inaovertake lorry lenye kontena 40 ft kwenye kona kali na alama za barabara zinaonesha kabisa hairuhusiwi kuovertake eneo hilo. Oneni picha niliyoattach.

Madereva wa kampuni hii kuweni makini na mjirekebishe. Mmebeba roho za watanzania.

Askari polisi pia fuatilieni hili jambo. Dereva muhusika achukuliwe hatua za kisheria.
 

Attachments

  • 20190706_200558.jpg
    20190706_200558.jpg
    98.1 KB · Views: 56
Mabasi muda wote yanaharaka,,,mm binafsi nikisafiri napenda basi lenye kwenda speed Akina mghamba,isamilo,sasebosa,kisbo,sabena,Arusha express
 
kwamba police hawashughuliki na taarifa za mitandaoni mkuu...
 
Hili ni kosa kubwa na la kizembe kabisa! Polisi wameliona hili na watalifanyia kazi. Ahsante kwa uzalendo wako
 
Mkuu usafiri huu wa mabasi ni hatari sana mimi nilisafiri na new force hivi karibuni ni hatari sana
 
Niliapa kutopanda hizo bus labda niwe mgonjwa na kupandishwa pasipo kujijua.

Ilikuwa natokea Mwanza kuja Dar, sijui mmiliki wake ndiye alikuwa dereva majibu na karaha zilizokuwepo kwa abilia nikajua huyu kavamia biashara.
 
Hizi mambo hupaswi kuleta hapa. Peleka kwa RTO wako wa karibu
Barabara inaonesha hapo kuna njia 3 ingawa wa kushoto haruhusiwi kuovertake ila kuna nafasi kubwa mno ya kuovertake.. Tupunguze ujuaji. Chuki yako ni kukichuna ki vitz chako.
 
Hiyo barabara ya njia 3.

Labda mleta malalamiko aseme tuu generally madereva wa hiyo kampuni wako rafu lkn hiyo picha sio ushahidi.
Nadhani mleta habari ana mambo yake na kandahari.
Halafu mleta mada alikuwa anatembelea Slow climbing Lane ambayo imemuweka nyuma lori kama unagari ndogo au nyepesi ungetumia middle lane
 
Za jioni wakuu... madereva wa hii kampuni wako very rough. Kuna siku mmoja aliwahi kuikwaruza gari yangu alafu akakimbia..

Leo nimeshuhudia overtake mbaya sana kwenye corner.
basi no. T 575 BVD ikitokea babati kuelekea arusha inaovertake lorry lenye kontena 40 ft kwenye kona kali na alama za barabara zinaonesha kabisa hairuhusiwi kuovertake eneo hilo. Oneni picha niliyoattach..

Madereva wa kampuni hii kuweni makini na mjirekebishe. Mmebeba roho za watanzania.

Askari polisi pia fuatilieni hili jambo. Dereva muhusika achukuliwe hatua za kisheria.
Pia naona miundombinu ya hii barabara inamruhusu dereva kupita alipopipita tazama mistari inayoigawa barabara ni kama njia tatu hapo anapopita dereva huyo yupo sawa kabisa
 
Pia naona miundombinu ya hii barabara inamruhusu dereva kupita alipopipita tazama mistari inayoigawa barabara ni kama njia tatu hapo anapopita dereva huyo yupo sawa kabisa
Hakuna haja ya kumpigia simu RTO ni kumpotezea muda tu waache Wanyampaa wawahi
 
Hivi nyie mnaotetea mnajua hata kuendesha mkokoteni kweli? Mnaona ni kwenye kona na pia hairuhusiwi kuovertake hapo mistari chini inaonyesha halafu mnaanza kutetea.
 
Mimi hiyo barabara nimeanza kupita na gari mwaka 80 mpaka inawekewa lami nilikuwa napita sijawahi kugonga hata nzi na tokea iwekewe lami ni magugu tu ndio huwa natembea mdogo kwa sababu ya trafiki njaa

Ila sehemu nyingine huwa namwagika
 
Njia tatu maana yake, gari inayoenda taratibu inapita kushoto kabisa, kama ilivyoonyeshwa kwenye picha, na basi linaenda kasi limepita njia ya kati, na kimsingi hapo haovertake kama mtoa mada anavyojaribu kueleza. gari inayoshuka ina njia yake kama picha inavyoonyesha
 
Hizi mambo hupaswi kuleta hapa. Peleka kwa RTO wako wa karibu pumbavu wewe
Barabara inaonesha hapo kuna njia 3 ingawa wa kushoto haruhusiwi kuovertake ila kuna nafasi kubwa mno ya kuovertake.. Tupunguze ujuaji. Chuki yako ni kukichuna ki vitz chako.
Wewe unaweza kuwa mpumbavu mara milioni moja. Unajua shera za barabarani? Hao waliochora hiyo mistari ya katikati waliweka urembo? Idiot!
 
Back
Top Bottom