Madereva wa daladala, Manispaa ya Bukoba mkoani Kagera wagoma baada ya kupandishiwa tozo za maegesho

Papaa Mobimba

JF-Expert Member
Jan 27, 2018
747
3,059
Madereva wa daladala, Manispaa ya Bukoba mkoani Kagera wamegoma kusafirisha abiria baada ya kupandishiwa gharama za maegesho.

Wasafiri kwenda maeneo mbalimbali mkoani humo wameshindwa kusafiri kutoka stendi ya mabasi Bukoba baada ya kutokea kwa mgomo leo asubuhi

Wanapinga ongezeko la ushuru kotoka Tsh. 1,000 hadi Tsh. 2,000 kwa magari madogo(Hiace) na Tsh. 2,000 hadi Tsh. 4,000 kwa Coster huku kukiwa hakuna maboresho yaliyofanyika kituoni

Mwenyekiti Chama cha Kutetea Abiria Kagera(CHAKUA), Samidu Bashiru amepinga ongezeko hilo na kuongeza stendi hiyo haina choo wala jengo la kupumzikia abiria

Aidha, kufuatia mgomo huo, abiria waliokuwa wasafiri kutoka wilaya mbalimbali kwenda mjini Bukoba wanadaiwa kushindwa baada ya kukosekana kwa usafiri

Kamanda wa Polisi Bukoba, Revocatus Malimi amesema jeshi hilo linafuatilia mgomo wa madereva uliotokea kwenye manispaa hiyo kwa kile kilichodaiwa ni kupinga baadhi ya tozo zilizowekwa na manispaa hiyo.

Kwa mujibu wa Kamanda Malimi, Jeshi la Polisi linafuatilia kwa ukaribu ili kufahamu kuwa waliogoma ni madereva au ni wamiliki wa magari, na hivi karibuni jeshi hilo litatoa taarifa juu ya mgomo huo.

Akizungumza na www.eatv.tv Kamanda Revocatus Malimi amesema “taarifa ni za kweli ila jeshi letu linafuatilia lijue madai yao ni nini, pia tunahitaji kujua waliogoma ni wasafirishaji au ni abiria, na tumeambiwa ni mgomo baridi wa kutokutoa huduma.”

Mapema leo majira ya saa 3 asubuhi zilianza kusambaa taarifa juu ya kutokea kwa mgomo wa madereva wa daladala kutokutoa huduma za usafiri wakielekeza malalamiko yao kwa manispaa ya Bukoba.

Mbali na madai hayo pia inaelezwa kuwa madereva hao pia wanagomea juu ya ubovu wa miundombinu kwenye eneo ambalo wamekuwa wakiegesha magari yao.

Ds_eacWXcAA9wZd.jpg large.jpeg
 
Kuna mpuuzi tu mmoja... Kakaa zake ofisini halafu anasema kuanzia leo wale wa 1000 watalipa 2000 na wale wa 2000 watalipa 4000.

Just mpuuzi mmoja tu anayepepewa na kiyoyozi ofisini kwake.
 
kuliko kugoma wangeongeza bei tu
Hizi sio Zama za mikwara ya kugoma ukigoma baki Na mgomo wako wengine wanaendelea
 
Kwa hali ya hcho kituo ni bora wagome kabsa... kituo hakna choo mvua ikinyesha ndo tabu tupu!!!! hafu mtu unaongezewa ushuru wa maegesho? shame on them
 
Back
Top Bottom