Madereva wa daladala jijini Dar es Salaam wanastahili pongezi

it's Zanzibar taratibu, Mkuu Zanzibar ni kama Tanga, hupaswi kuwa na haraka.
ata mimi nimeona maereva wa daladala hapo Dar wapo vizuri. Sio wao tu hata madereva wa kawaida japokuwa accident barabarani kitu cha kawaida tu. Njooni Zanzibar muone madereva wanavyoendesha magari. Kama huna Subira unaweza kutukana mwanzo wa safari hadi mwisho. Daladala inaweza ikasimama katikati ya njia na kupakia abiria, daladala anaweza akakuovertake halafu akasimama mbele yako bila ishara yoyote ilimradi apakie abiria, madereva wa kawaida kwenye barabara yenye 2 lanes anakaa katikati, ukimpigia honi akupishe hakupishi na mwendo wake utakuta mdogo. Tafrani tu madereva wa uku
 
Naonaga pale makumbusho daladala za ubungo-makumbusho via chuo kikuu road wanayapaki utafikiri wewe unavyoweka mche wa sabuni kwenye box lenye miche mingine.
Yaani anaipeleka mbele then anairudisha riverse kwenye nafasi ya kutosha gari moja tu, upana rula, hapo kwa kuangalia side mirror tu.
 
dereva akilala muda wote anatupatupa mikono anahisi yupo kazini.
Ila wapo vizuri sana suala la Manual Transimission mana wao simama tembea simama tembea tofauti na private ikichichea imechochea unakua ka automatic gear tu ila daladala gia inacheza hswa
 
SIo tatizo kuwa taratibu mkuu. Ila mtu unakaa katikati ya lanes unazuia hata wenzak kupita? Zanzibar ukiendesha gari kwa ustaarabu, una chance kubwa ya kupata ajali kuliko ukiendesha kama mwendawazimu. Mimi mtu akikaa mbele yangu kizembe huwa namfanyia fujo mpaka anakaa pembeni mwenyewe
 
Muda wanaolala na wanaoamka mimi hoi.

Saa 6usiku-10 alfajiri macho.

Nadhani huwa wakilala wanasikia milio ya engene tu

Kondakta mmoja alipolala akawa anaota. We denti shuka! (akamshusha mwanafunzi) halafu akapiga bodi ya gari, Endesha suka!

Kumbe kwa kuweweseka ndotoni, alimshusha kitandani mtoto wake mchanga, na kumpiga mkewe kofi mgongoni.

H/T: Kibonzo cha "Bi-Mkora"
 
Mkuu nadhani wewe dar utakuwa unakuja na kuondoka....usichokijua ni kwamba hao jamaa wana butuana sana ila kesi zao azimalizi dakika 5 barabarani washazimaliza kwani wengi wao wanafahamiana.
 
Kila siku ninapita NIT bila shaka nimeshakuwa dereva mzuri
Unapita ila hujapata cheti.. Bado hujakamilisha sifa ya kuwa dereva mzuri pasipo kuthibitishwa na NIT.. Kalipe ada ujiunge na mafunzo.. Itakusaidia kuiendesha kwa usalama familia yako iwapo hutofanya kazi ya udereva kama ajira!
 
nimekaa sana Zanzibar naifamu vizuri. Tabia yakufanya mambo kwa mazoea ndio chanzo cha yote hayo.
SIo tatizo kuwa taratibu mkuu. Ila mtu unakaa katikati ya lanes unazuia hata wenzak kupita? Zanzibar ukiendesha gari kwa ustaarabu, una chance kubwa ya kupata ajali kuliko ukiendesha kama mwendawazimu. Mimi mtu akikaa mbele yangu kizembe huwa namfanyia fujo mpaka anakaa pembeni mwenyewe
 
kesi wanamaliza fasta ila tukio halifichiki MKUU.
Mkuu nadhani wewe dar utakuwa unakuja na kuondoka....usichokijua ni kwamba hao jamaa wana butuana sana ila kesi zao azimalizi dakika 5 barabarani washazimaliza kwani wengi wao wanafahamiana.
 
Hivi mnaijua ligi ya gari za gongo la mboto- Masaki!!!! Ama mbagala kawe""

Uwiii hizi icha!!!!!Na Tata""" utazan zinaenda mkoa""""
Nimekuwa abiria wa Mbagala miaka 10,
Sijawahi pata ajali kwenye gari yeyote ya ruti ya mbgla.
Ukiacha tu uabiria wa Mbgl,Nimepanda daladala Dar, miaka yote sijawahi kupatwa na ajali ktk daladala nililopanda.
Wasifiwe tu hawa jamaa wanastahili.
Japo ajali zipo ila ni chaaaache sana.
 
Wapo vizuri kwa kwakweli, hasa ukizingatia muda wote wawapo barabarani wanaharaka.
Nimekuwa abiria wa Mbagala miaka 10,
Sijawahi pata ajali kwenye gari yeyote ya ruti ya mbgla.
Ukiacha tu uabiria wa Mbgl,Nimepanda daladala Dar, miaka yote sijawahi kupatwa na ajali ktk daladala nililopanda.
Wasifiwe tu hawa jamaa wanastahili.
Japo ajali zipo ila ni chaaaache sana.
 
Huwezi amini ila ndio ukweli wenyewe, licha ya kuongoza kwa uvunjaji wa sheria za barabarani ni nadra sana kusikia au kuona daladala za Bongo zimegongana zenyewe au na magari mengine.

Wanaziendesha kwa spidi ya juu kabisa muda wote tena katikati ya jiji kwenye msonganano mkubwa wa magari ya kila aina na vyombo vingine vya usafiri huku wakipitana ama kutanua njia mara kwa mara na hata kuzipitisha kwenye barabara za mitaani inapolazimu lakini bado uhakika wa kufika SALAMA waendako ni mkubwa.

Ni rahisi kuona gari ya mtu binafsi imeingia mtaroni, kugongana na nyingine au kugonga mahala kutokana na dereva kushindwa kuhimili mikikimikiki ya barabarani lakini si kwa daladala, chakushangaza zaidi ni kwamba udereva wao unategemea akili zao zaidi kuliko sheria.

Kuna madereva wa daladala ukimuangalia unaweza kuhisi ni chizi lakini analiendesha kutwa nzima pasi kupata hata mchubuko! Naamini kama wangekua wanajali sheria za barabarani basi wangeweza kuwa ndio madereva hodari zaidi dunia nzima.
Ni kweli Madereva wa Daladala Dar es salaam Wanàstahili Pongezi. Nikiwakumbuka waendeshao Eicher wanavyopita Kariakoo penye msongamano wa watu, Magari na bidhaa huwa nasema Heko Sana kwao.
Above All thanks to Almighty God atulindae daily tukiwa ndani ya Daladala.
 
30 Reactions
Reply
Back
Top Bottom