Madereva, vifuatavyo ni vipande hatari /vibovu mno vya barabara...

Mdakuzi mkuu

JF-Expert Member
Dec 27, 2016
212
719
Salam ndg zangu, waendesha vyombo vya moto hasa magari ya mizigo na ya abiria.

Nimeona ni vyema tuweka wazi "portions" za barabara zetu za mikoani ambazo ni mbovu, nyembamba, zina mawimbi mawimbi na utelezi mkubwa.

Soma hapa ili upate picha halisi hasa kwa wewe mgeni au msahaulifu wa kupita maeneo haya bila kuwa na tahadhari kubwa:-

1. Kipande cha barabara toka Ruvu Darajani mpk Mlandizi. Barabara nyembamba mno na ina mawimbi sana

2. Kipande cha barabara Mzumbe - Mikumbi. Barabara iko rough sana na nyembamba

3. Makambako - Mafinga. Haishagi kutengenezwa

4. Msata - Mizani ya Chalinze. Mawimbi mno

5. Msambiazi - Mbuyuni - Chekelei (Korogwe Tanga). Mawimbi

6. Same - Mgagao - Lembeni (Mwanga) na Mwanga - Kifaru. Hovyo mno

7. Mdaula - Mikese (Morogoro)


Naomba tuongeze hapa...
 
>Pia mteremko wa K9 inabidi tukumbushane
>Tamasenga barabara inalewalewa mawimbi
>Ndiuka bado kuna wizi sio sehemu nzuri ya kupaki kama unataka kupumzika.
>Namba 1.hiyo sehemu ni korofi kitambo.
>Msamvu machangudoa wamezidi usiku
 
1) Barabara ya Pugu/Kajiungeni - Chanika: Ni hatari kwa malori ya mchanga na ni nyembamba pia
2) Barabara ya Kilwa kipande cha Msikitini: Hatari pale mteremko pia kuna vibaka gari ikiharibika bora uisukume.
3) Singida Manyoni: Hatari hiyo barabara inaita tu unaweza kufika hata 200km/h bila kujua ukishtuka uso kwa uso na mwenzako.
4) Barabara ya Nyakanazi - Biharamuro, Nyakanazi - Ngara milima na miteremko hatari!!
5) Nzega - Tabora: Vumbi sijui wameshaweka lami siku hizi
6) Barabara ya Ngorongoro - Serengeti kwenda mugumu town kuna sehemu barabara inamchanga hatari, ni vizuri kwenda kwa tahadhali
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom