Madereva tuache tabia hizi

Juakali jr

JF-Expert Member
Aug 8, 2019
685
1,671
madereva wa siku hizi wamekua wakuda sana yani hadi kero.

Ngoja kwanza tutambue ukuda ni upi.
1. Upo barabara kuu hamna matuta wala kizuizi chochote lakini wewe unaamua kuendesha 30 kmph (sio kosa), nyuma yako kuna gari linataka kuovertake lakini haliwezi sababu upande wa pili upo busy, pale wapili unapokua free wewe unaongeza maspeed kama yote mpaka itakapokua shida kuwa overtaken. Wewe ni mkuda.

2. Upo double ways wewe na wapembeni yako wote mnaamua kuendesha sambamba 30 kmph na kulazimisha magari ya nyuma yashindwe kuwavuka, angali mlikua mnauwezo wakupishana kidogo na kuendelea kuenjoy na slow motion zenu. Wewe ni mkuda.

3. Umbali wenyewe wa dakika 5 tu, barabara yenyewe ya vumbi lakini wewe mjamaa unaendesha 80 kmph. , Wewe ni mkuda na ndo maana tunawachimbia matuta makubwa kama makaburi.

4. Kuna madimbwi ya kutosha lakini wewe mjamaa unaendesha na maspedi kama yote mpaka unaturudisha nyumbani wapita njia. Wewe ni mkuda

Zingine tutaendelea taratibu.
 
Madereva wa daladala nao wakuda kinoma, hawaingii kushushia na kupakia abiria stand! Wanasimama barabarani na kusababisha foleni wakuda hawa! Hasa stand ya Mkwajuni kama unakwenda Magomeni kutokea Moroko na Buguruni chama kama unakwenda Ubungo tokea TAzara baada ya taa!! Wakuda sana, wanaboa kinoma halafu unakuta stand iko empty
 
Madereva wengi sana Tz hawajui kuwa kama kuna njia mbili za kwenda upande mmoja basi kama wewe uko slow kaa kushoto wenzio wapite kulia. Na ndio kitachotokea kwenye njia 8 za Ubungo-Kibaha. Utashangaa malori yanabana kulia then wote mnachelewa.
 
Ipo pia
1. Stand ya Kimara Mwisho. Wamejengewa kabisa njia ya kuchepuka wakapakie abiria ila wao wanapakilia main road na kufanya foleni

2. Stand ya daladala Mwenge wamejengewa pia sehemu ya kuingia ila wao wanaenda kule juu kabisa na kuleta usumbufu
 
Na kuna wale wanabadili lane kutoka kushoto kwenda kulia au kulia kwenda kushoto bila kuangalia gari ya nyuma inakuja na spidi gani jitu linahamia kwako afu lipo slow kuliko wewe tatizo sana ka una mawazo yako unaeza gonga...

Yan mtu badala yakuangalia kioo anawasha indicator anahama
 
Kwani stendi ya Mwenge imekamilika? Au una maanisha kituo?
 
Na kuna wale wanabadili lane kutoka kushoto kwenda kulia au kulia kwenda kushoto bila kuangalia gari ya nyuma inakuja na spidi gani jitu linahamia kwako afu lipo slow kuliko wewe tatizo sana ka una mawazo yako unaeza gonga...

Yan mtu badala yakuangalia kioo anawasha indicator anahama

Wewe siyo dereva makini. Dereva makini anaendesha gari 5 akiwa barabarani. Ya kwake, ya mbele, nyuma, na kulia na kushoto.

Ni jukumu lako kumlinda wa mbele yako, tena hili halina mjadala. Yaani hata kama wa mbele anacheza zigzag, ni sharti umlinde usimgonge, kama unabisha gonga halafu traffic aje. Tena utoe sababu eti jamaa alikuwa anayumba? Traffic atakuambia hukuweka umbali unaotakiwa wa mita 3. Yaani, unatakiwa uone matairi ya gari ya mbele yanazunguka. Ukisogelea sana na usipoyaona matairi ya mwenzako ujue muda wowote unamgonga. Sijui udereva mnasomea wapi?

Huwa ninasikitika sana, lakini hakuna namna.

Kingine, hapa mtoa mada analalamikia mwendo wa 30KM. Kimsingi, huu mwendo haukatazwi na sheria. Sanasana, kama speed limit inasoma 50km/hr, ukitembea 30km siyo kosa. Kosa, ambalo utapewa karipio iwapo ukibainika, ni kutembea speed 20 wakati limit ni 50. Ila Kama hamna limit ukiwa 50 hakuna kosa.

Lakini pia Kuna speed limit za 20 na 30. Mfano, barabara ya kutoka Marangu Mtoni kwenda Rombo ina kona nyingi na miteremko. Speed limit sehemu kubwa ni 20 na 30. Sasa kuna madereva wengine wanataka ukiwa njia hii basi ukanyage 50 na 60 Jambo ambalo ni hatari. Nimeshuhudia huu usumbufu na mwingine anaovertake sehemu hatari.

Udereva siyo kujua kuendesha chombo Bali ni nidhamu, kujua na kutii sheria. Na hapa ndipo kuna wasumbua wengi. Hata Jana Singida ile ni ajali inatokana na wrong over taking.

Tujifunze utii
 
Madereva wa daladala nao wakuda kinoma, hawaingii kushushia na kupakia abiria stand! Wanasimama barabarani na kusababisha foleni wakuda hawa! Hasa stand ya Mkwajuni kama unakwenda Magomeni kutokea Moroko na Buguruni chama kama unakwenda Ubungo tokea TAzara baada ya taa!! Wakuda sana, wanaboa kinoma halafu unakuta stand iko empty
River side ndio kimeo zaidi ukiwa unaelekea Ubungo
 
Kuna hawa wa bodaboda,

Huwa hawajui kusubiri.

Wanapenda kujichomeka katikati na kupita na side mirror zetu.

Hawa wako radhi chombo chake kitembee bila breki lakini honi iwepo.

Gari nyingi hasa Dar zina mikwaruzo ya kuchubuka rangi kisa ni hawa vijana.
saivi wanaweka horn za HARRIER
 
Madereva wa daladala nao wakuda kinoma, hawaingii kushushia na kupakia abiria stand! Wanasimama barabarani na kusababisha foleni wakuda hawa! Hasa stand ya Mkwajuni kama unakwenda Magomeni kutokea Moroko na Buguruni chama kama unakwenda Ubungo tokea TAzara baada ya taa!! Wakuda sana, wanaboa kinoma halafu unakuta stand iko empty
Hawa mimi nilishawagroup ni vichaa, nahisi huo mtindo wakutoingia stendi walizojengewa wamefundishwa vyuoni kwao. Maana ni kama wote vile, unakuta kuna mafoleni yasio na kichwa wala mguu
Madereva wengi sana Tz hawajui kuwa kama kuna njia mbili za kwenda upande mmoja basi kama wewe uko slow kaa kushoto wenzio wapite kulia. Na ndio kitachotokea kwenye njia 8 za Ubungo-Kibaha. Utashangaa malori yanabana kulia then wote mnachelewa.
Haya malori huwa yanaogopa kukaa kushoto sababu ya mabasi, yakikaa kushoto ikifika sehemu ya mabasi itawalazimu kuhamia kulia, ndo maana yanaona bora yakae kulia tu. Changamoto inakuja pale yanaamua kukaa moja kulia lingine kushoto alafu yote yakaamua kwenda mwendo sawa.
Na kuna wale wanabadili lane kutoka kushoto kwenda kulia au kulia kwenda kushoto bila kuangalia gari ya nyuma inakuja na spidi gani jitu linahamia kwako afu lipo slow kuliko wewe tatizo sana ka una mawazo yako unaeza gonga...

Yan mtu badala yakuangalia kioo anawasha indicator anahama
Huu sasa ni uchizi, kuna raia zinaendesha magari kama vile bodaboda
 
Kuna hawa wa bodaboda,

Huwa hawajui kusubiri.

Wanapenda kujichomeka katikati na kupita na side mirror zetu.

Hawa wako radhi chombo chake kitembee bila breki lakini honi iwepo.

Gari nyingi hasa Dar zina mikwaruzo ya kuchubuka rangi kisa ni hawa vijana.
Hawa wajamaa huwa spendi urafiki nao barabarani, hata kwenye foleni saa nyingine naacha uwazi mkubwa ili waweze kupita. Maana kuna muda unaona kabisa mtu awezipita lakini jamaa anakomaa tu.
Navyoona bora uwaachie nafasi tu, vinginevyo ni kuingia gharama tu.
Dreva ana overtake kwenye kona au mwisho wa kilima na haoni mita 100 mbele, hajui upande wa pili kunaweza kuwa na mtu anakuja yupo 160kph. Huu nao ni ukuda
Daaah hawa pia Mungu awalinde
 
Similar Discussions

5 Reactions
Reply
Back
Top Bottom