Madereva tisa wa magari ya abiria wafungiwa leseni kwa kusababisha ajali na vifo mkoa wa Ruvuma


Donatila

Donatila

JF-Expert Member
Joined
Oct 23, 2014
Messages
3,091
Likes
4,085
Points
280
Age
28
Donatila

Donatila

JF-Expert Member
Joined Oct 23, 2014
3,091 4,085 280
Kikosi cha Usalama Barabarani mkoa wa Ruvuma kimewafungia leseni madereva tisa wa magari ya abiria waliosababisha ajali na kusababisha vifo vya watu na majeruhi ikiwa ni mikakati ya kikosi hicho mkoani Ruvuma kupunguza ajali.

Akizungumza kwenye uzinduzi wa Wiki ya Nenda kwa Usalama Barabarani mkoa Ruvuma uliofanyika katika kituo cha mabasi ya Mbinga, Kaimu Mkuu wa kikosi hicho mkoa wa Ruvuma ADAM KIMBESI amesema polisi wanalazimika kufanya hivyo ili kupunguza ajali.

Mwenyekiti wa Kamati ya Usalama Bara barani mkoa wa Ruvuma Bwana PHILIP SHANTEMBO ametaka uwepo ushirikiano kati ya polisi ,abiria na madereva ili kupunguza ajali na kwamba kila mmoja atimize wajibu wake.

Mkuu wa wilaya ya Mbinga Bwana COSMAS NSHENYE amewataka polisi kuendelea kusimamia sheria na wao pia kuwa wa kwanza kufuata sheria.


ITV
 

Forum statistics

Threads 1,251,853
Members 481,915
Posts 29,787,757