Ghazwat
JF-Expert Member
- Oct 4, 2015
- 23,718
- 66,266
Wakizungumza wakati wa mafunzo ya kuwajengea uwezo yaliyoandaliwa na mabalozi wa usalama barabarani (RSA) madereva hao wameitupia lawama TBS wakidai ndiyo chanzo cha magari kupata ajali
Dereva, Athuman Abdalah amesema wanashangaa wao kulalamikiwa kuwa ndio chanzo cha ajali wakati adui wao ni TBS ambayo inafanya ukaguzi wa ubora wa matairi
Amesema idadi kubwa ya ajali za barabarani husababishwa na matairi kupasuka hivyo gari kupoteza mwelekeo
Mkurugenzi wa RSA, Mallin Komba amesema madereva wanatakiwa kufahamu wajibu wao na kuzingatia sheria za usalama barabarani ili kupunguza ajali nchini
"Kazi yetu ni kutoa elimu kwenye vituo vya mabasi ya mikoani kila siku asubuhi kabla ya safari kuanza," alisema Komba
Hata hivyo Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa TBS, Profesa Egid Mubofu amesema shirika hilo haliwezi kupitia matairi yaliyo chini ya kiwango kwa sababu linavisimamia vilivyowekwa kitaifa
"Hizi tuhuma si za kweli hakuna uchochoro wowote unaotumika, kama wana ushahidi watuleteee. Sisi tunafanya kazi kwa kufuata viwango vilivyokuwa,"alisema Profesa Mubofu
Kamanda wa kikosi cha usalama barabarani, Mohamed Mpinga akitoa takwimu za ajali za barabarani mwaka 2016 amesema vifo vya madereva vilikuwa 242, watembea kwa miguu 992, na abiria 1,009.
Mpinga amesema kwa upande wa majeruhi madereva walikuwa 607, watembea kwa miguu 1,640 na abiria 4,650.
Chanzo : Mwananchi