Freed Freed
JF-Expert Member
- Jun 27, 2017
- 6,224
- 6,468
Habari zenu familia ya JF. Mada hapo juu yajifafanua. Kumekuwa na ajali nyingi za pikipiki humu nchini na hutokana na sababu mbalimbali ikiwa ni pamoja na matumizi ya sehemu mbalimbali za pikipiki. Je ni lini na wapi mwendesha pikipiki atatumia breki ya mkono wa kulia awapo barabarani? Ikumbukwe breki hii ni hatari sana na huogopwa na wengi. Jamani tushauriane maana breki hii ishaniangusha na kuniumiza sana. Tanbihi: Mods huu Uzi muiache muda mrefu kwenye safu za mbele kwani ni elimu mahususi ya USALAMA BARABARANI hivyo mchango wake utapunguza ajali za pikipiki na ulemavu ktk jamii.