ndugu zanguni kama kuna kampuni inaendeshwa kihuni basi kampuni ya mafuta ya lake oil haina mfano.kampuni hii licha ya kukosa utaratibu maalum wa kazi hali inayoonyesha haina uongozi wenye akili timamu,madereva wanaosafirisha mafuta ktk nchi za kongo,zambia,Rwanda,Burundi nk wamekuwa wakiwekwa ndani ktk nchi hizo za ugenini kwa kisingizio cha kukutwa na hasara ya mafuta,hasara ambayo aidha husababishwa kwa makusudi na vipimo vya sehemu ambayo mafuta yanashushwa na kupelekea baadhi ya madereva kulazimika kuyakimbia magari kukwepa unyanyasaji huo.mbaya zaidi dereva ambae wamemwajiri tanzania wanakwenda kumweka ndani ktk nchi ya kigeni ambako hana mdhamini,na anawekwa ndani bila maelezo wala maandishi yoyote.madereva ktk kampuni hii ya mafuta wanaishi kwa mashaka kama watumwa.nimeliweka hili hapa jamvini ili kama kuna wadau wa haki za wafanyakazi waitupie jicho LAKE OIL kwa vitendo vya unyanyasaji wafanyakazi hasa madereva na kwa wataalam wa sheria pia watusaidie juu ya kumfunga mtu ughaibuni tena bila maelezo yoyote.
Meneja wa hii kampuni anaitwa ndugu ahmed na mkurugenzi wake ni ndugu alliy.
Karibuni wadau.
Meneja wa hii kampuni anaitwa ndugu ahmed na mkurugenzi wake ni ndugu alliy.
Karibuni wadau.