Madereva, dawa nzuri ya anayekuja nyuma yako kawasha full nyakati za usiku

Mdakuzi mkuu

JF-Expert Member
Dec 27, 2016
212
719
Habarini hapa ndani.

Kumekuwa na kitabia fulani, mtu anatembelea taa zenye mwanga mkali yaani 'full light' barabara nzima,hasa usiku. Hasa watu wenye ma-vx, fuso, semi trailer.Kiasi kwamba, kama upo na starlet au passo yako, unashangaa pamegeuka mchana, unamulikwa kagari kako kote.

Utaratibu upo hivi:

Usiku ukiona mtu anatoka nyuma anakuja na taa zake full,wala usigope, tulia!

Geuza geuza (set) site mirror yako uliyo karibu nayo elenge vzr huo mwanga mkali unaotoka nyuma.

Huo mwanga mkali unamrudia dereva wa hiyo gari ya mwanga mkali,hapo hapo atapotea njia au labda asimame au atoe full light. Ni dawa tosha sana na haina gharama kwako
 
Hiyo haina shida kwa aliyeko nyuma mbaya ni mnayepishana tena ukifanya kama unavyojiaminisha ndio umekikaribisha kifo mazima
 
You can't be seriously...,sasa huo muda wa kuset site mirror utaupata wapi na wakati huo huo na yeye sio kwamba atakuwa anakuja nyuma kanyoosha gari kama ipo kwenye rula.,mwisho wewe mrekebisha site mirror ndiyo utaingia mtaroni.
 
Umefikria kama ni bus liwe ba abiria ufanye hvyo then aingie mtaroni?
 
Kuna watu wana Maudhi sana Barabarani!
Kwanza unakuta anadrive gari speed 30 saa 11 asubuhi, hivi kwa nini usilale???
Kuna Mtu Mwingine anaendesha gari kwa speed 30, unataka kumpita anakaza! Unampisha, anafika mbele anakaa na speed yake 30, kwa mtu kama huyu me huwa napata hasira namuwasha fulu, tena bahati mbaya gari yake ndogo atapisha tuu!
Ukiwa Barabarani endesha kistaarabu, tupishane, wenye haraka waende, wewe wa polepole kaa pembeni!!!
Lingine akina dada sisi wanaume tunawapisha sana Barabarani, Lakini Nyie kutupa nafasi ya kuingia Barabarani hakuna, Hivi Aliewafundisha driving ni Mwalimu Mmoja???
 
Ila nashindwa kuelewa watu wanajisahau au kutokuelewa au nini? Kwa nn utembee barabarani full light?

Unaweza sababisha kugongwa na kujipotezea uhai hiv hv kwa sababu ya uzembe
 
Habarini hapa ndani.

Kumekuwa na kitabia fulani, mtu anatembelea taa zenye mwanga mkali yaani 'full light' barabara nzima,hasa usiku. Hasa watu wenye ma-vx, fuso, semi trailer.Kiasi kwamba, kama upo na starlet au passo yako, unashangaa pamegeuka mchana, unamulikwa kagari kako kote.

Utaratibu upo hivi:

Usiku ukiona mtu anatoka nyuma anakuja na taa zake full,wala usigope, tulia!

Geuza geuza (set) site mirror yako uliyo karibu nayo elenge vzr huo mwanga mkali unaotoka nyuma.

Huo mwanga mkali unamrudia dereva wa hiyo gari ya mwanga mkali,hapo hapo atapotea njia au labda asimame au atoe full light. Ni dawa tosha sana na haina gharama kwako
Mkuu, dawa nzuri zaidi ni kupunguza mwendo, wacha akupite.
Akiwa mbele, give him a piece of his own medicine~full light!
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom