Madenti wachangishana 2,000 kukodi walimu! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Madenti wachangishana 2,000 kukodi walimu!

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by binti ashura, Feb 27, 2011.

 1. b

  binti ashura Senior Member

  #1
  Feb 27, 2011
  Joined: Jan 14, 2011
  Messages: 120
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 0
  Madenti wachangishana 2,000 kukodi walimu!

  Wakati tukiwa tunaaambiwa serikali ya JK inafanya kila jitihada ilimradi kuongeza idadi ya walimu mashuleni, hali ni tete ktk shule ya sekondari ya King'ong'o ya jijini Dsm....ambapo baada ya kukosekana kwa walimu....madenti wa skonga hilo wamefikia hatua ya kupiga doneee (kujichangisha) kiasi cha shilingi 2,000 kwa kila denti kwa mwezi ili waweze kukodi walimu wa kuwapa nondo (kuwafundisha).

  Akizungumzia walimu hao wa kukodi,Diwani wa Kata ya Saranga, Ephraim Kinyafu,alisema wanawakodi walimu ambao wamemaliza kidato cha sita na wengine kutoka shule binafsi.

  Hata hivyo, amesema hadi sasa walimu hao waliomaliza kidato cha sita tayari wameshaenda vyuoni na hivyo kuiweka shule hiyo kuendelea kuwasaka wengine kujaribu kutatua tatizo hilo.

  “Nimelichukulia tatizo hili kama janga na ndiyo maana nimewaomba madenti kushiriki kutatua tatizo hili ambapo nimeona afadhali tuchangishane sh. 2,000 kwa kila denti kwa kila mwezi ili tuzitumie kuwakodi walimu kwa ajili ya kunusuru tatizo hili,” amesema Kinyafu.

  source: Madenti wachangishana 2,000 kukodi walimu!


  kwangu naona wanafunzi hao wamechukua uamuzi wa msingi ila najiuliza je kule kijijini itakuwaje?
   
 2. k

  kituro Senior Member

  #2
  Feb 28, 2011
  Joined: Dec 25, 2010
  Messages: 176
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35
  hongera sana kwa kuchukua hatua mapema! vinginevyo ingekula kweno!
   
 3. doup

  doup JF-Expert Member

  #3
  Feb 28, 2011
  Joined: Feb 26, 2009
  Messages: 1,172
  Likes Received: 335
  Trophy Points: 180
  Hivi kwa nini wanafunzi wa UDSM - education na wengineo wakali wa science, law & engineering wasichukue hizo part time kuokoa taifa na kujiongezea boom!

  Na hii ni kwa kwa shule zote zilizo karibu na vyuo
   
 4. Gagurito

  Gagurito JF-Expert Member

  #4
  Feb 28, 2011
  Joined: Feb 11, 2011
  Messages: 5,610
  Likes Received: 25
  Trophy Points: 135
  wamefanya vizuri!
   
 5. f

  fungamesa Senior Member

  #5
  Feb 28, 2011
  Joined: Feb 20, 2009
  Messages: 128
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35
  Usiseme UDSM tu vyuo vyote ambavyo viko karibu na shule za secondari
   
 6. Husninyo

  Husninyo JF-Expert Member

  #6
  Feb 28, 2011
  Joined: Oct 24, 2010
  Messages: 23,814
  Likes Received: 583
  Trophy Points: 280
  una mawazo mazuri mkuu.
  Tatizo Wanafunzi wengi mabishororo na wengine inawezekana hawazioni hizo fursa.
   
 7. AK-47

  AK-47 JF-Expert Member

  #7
  Feb 28, 2011
  Joined: Nov 12, 2009
  Messages: 1,381
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 135
  Wanastahiki Kupongezwa kwa jitihada zao za kukodi walimu...ni vyema wamebaini kuwa serikali yao haikerwi na ziro wanazopata.
   
 8. Ndibalema

  Ndibalema JF-Expert Member

  #8
  Feb 28, 2011
  Joined: Apr 26, 2008
  Messages: 10,916
  Likes Received: 131
  Trophy Points: 160
  Hofu yangu ni kuwa wanaweza wakaibuka walimu feki ambao sio wanachuo.
  Watu wana mbinu bana!
   
 9. kilimasera

  kilimasera JF-Expert Member

  #9
  Mar 1, 2011
  Joined: Dec 2, 2009
  Messages: 3,073
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 135
  tanzania yetu hiyo inajiishia yenyewe
   
 10. M

  MZAWATA JF-Expert Member

  #10
  Mar 1, 2011
  Joined: Feb 10, 2011
  Messages: 555
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 35
  bora wafanye hivyo maana kwa sasa hatuna serikal
   
 11. Henge

  Henge JF-Expert Member

  #11
  Mar 1, 2011
  Joined: May 14, 2009
  Messages: 6,765
  Likes Received: 78
  Trophy Points: 145
  Haya yoote jk anasema ni chadema daaa huuu ni upumbavu!
   
 12. MESTOD

  MESTOD JF-Expert Member

  #12
  Mar 1, 2011
  Joined: Nov 12, 2010
  Messages: 4,640
  Likes Received: 142
  Trophy Points: 160
  Huu ndo mtaji wa mabadiliko ya kweli 2015. Hata mtu akiwaletea usanii somo halitaeleweka. Cjui na hili watalalamikia CDM?
   
Loading...