Madeni yanavunja urafiki

Isack Elia

JF-Expert Member
Jul 9, 2016
331
474
Kama heading inavyojieleza,

Nimekuwa na tatizo kila nikikopesha marafiki zangu pesa wananidhulumu hawanilipi. Wakati wananiomba wanaomba kwa huruma kuwanyima nashindwa lakini mwisho wa siku wananikimbia na kuvunja urafiki kabisa kiasi kwamba hata nikipiga simu wanauliza mimi ni nani.

Nikipiga mahesabu pesa ya madeni kwa marafiki ni mtaji tosha kabisa.

Je nifanye nini nisiendelee kudhulumiwa?
 
Pindi ukiwa na pesa hata unaemdai akikwambia vyuma vimekaza utamuelewa ila ikatokea unamdai mtu then anakuzunguusha alafu vyuma vimekaza upande wako hapo ndipo utapojijua kama umejaaliwa hekima au laa
 
Nina rafiki yangu nampenda ila akianza kunikopa siwezi kumkopesha sababu najua hatarudisha na ndo utakua mwanzo wa kuwa maadui. Namwambiaga tu sina au nataka ninunue kitu flan cha nyumbani.
 
Ni bora utoe msaada kuliko kukopesha hizi pesa ndogo ndogo. Kama mtu anaomba umkope laki tano, mwambie nakupa laki moja isiyo ya mkopo umalizane naye.
 
Nina rafiki yangu nampenda ila akianza kunikopa siwezi kumkopesha sababu najua hatarudisha na ndo utakua mwanzo wa kuwa maadui. Namwambiaga tu sina au nataka ninunue kitu flan cha nyumbani.
Una kosea sana inakupaswa umsaidie ikiwa unacho chakumsaidia.
 
kuna mmoja nilimkopesha laki na nusu kunilipa ikawa kasheshe nkamwambia anilipe hata nusu afu hyo nyingne niisamehe napo akanipga chenga ikapita miezi kadhaa nkamwambia bas nilipe hata elfu 10 tu hyo nyingne nitasame nijue sikukupa hela bure...kilichofuata sasa hadi machozi yananitoka nilichezea block kote yan daaah ubinadamu kazi japokua hatulipwi
 
Mkuu maisha ni kusaidiana kama unao uwezo usife moyo pengine kipato kinaongezeka kwa sababu hiyo, kuna siri sana katika kutoa, na wanayo ijua siri hiyo maisha yao yanakuwaga na amani na furaha tele.
 
Mkuu kutoa ni Jambo jingine na kukopesha ni jingine kabisa
 
Usikopeshe, nakama ikilazimika basi muandikishiane kwenye serekali za mtaa na mashahidi wawepo kama kumi hivi,
 
Mkuu kutoa ni Jambo jingine na kukopesha ni jingine kabisa
Yote nisawa tu kutokana na msukumo wako wandani juu ya tatizo linalo mkabili huyu unae msaidia, akikurushia nisawa na asipo kurudishia nisawa vilevile huna cha kupoteza.
 
Hapana ,ninaamin kutokana na imani yangu kuwa unaposaida wapata kheri nyingi sana ,ila kwa kukopesha unaweza kuingia na kwenye dhambi
 
Kwasababu umesema kwaimani yako ni sawa, lakini ipo hivi ukimsaidia mtu pia hilo ni deni kwake siyo kwako pengine wewe huwezi kuona lakin yeye anahesabu kama deni na atakulipa anaweza asikulipe kwa njia ile ambayo wewe uliitumia. Pia ukimkopesha hilo ni deni utalipwa tu.
 
Back
Top Bottom