Madee: Muziki wa hip hop bongo unapendwa na wahuni ambao hawawezi nunua kazi za wasanii

brave one

JF-Expert Member
Feb 5, 2013
4,879
7,382
Msanii wa muziki kutoka Tip Top Connection Madee amefunguka na kueleza ni kwanini wasanii wengi wa muziki wa Hip Hop nchini wanashindwa kufanya vizuri licha ya nyimbo zao kupendwa mitaani.

Muimbaji huyo ambaye anafanya vizuri na video yake ya wimbo, Migulu Pande, ameiambia Times Fm kuwa Hip Hop inapendwa na kundi la ‘wahuni’ wachache na machizi mtaani ambao ni ngumu kwenda dukani kununua kazi anayoipenda.

Katika hatua nyingine, Mdee amesema kama yeye angeendelea kudumu na staili yake ya kurap kama zamani mpaka sasa, angekuwa amekwisha potea kwenye ‘Game’ na ulimwengu wa muziki.

“Watu wanataka changes, kama biashara haikulipi kwanini uendelee kufanya inakuingizia hasara kila kukicha, ningekuwa narap mpaka leo nisingekuwepo kwenye game ningepotea, dunia yenyewe inabadilika sasa kwa nini wewe usibadilike” alisema Madee.

1463502054387.jpg
 
Hakuna ukweli wowote huyo jamaa ajitambui...wenzie kina sugu umaarufu wao umeanzia kwenye mziki huo huo ananaosema ni wa kihuni na Leo hii wanawakilisha watu zaid ya million moja bungeni...wache yeye na mwenzie ney waendelee kujiita marais wa manzese.
I'm sorry, hajaongelea umaarufu. Kaongelea mziki kulipa.
Soma vizuri, tafakari uelewe kabla hujani quote tena
 
Hakuna ukweli wowote huyo jamaa ajitambui...wenzie kina sugu umaarufu wao umeanzia kwenye mziki huo huo ananaosema ni wa kihuni na Leo hii wanawakilisha watu zaid ya million moja bungeni...wache yeye na mwenzie ney waendelee kujiita marais wa manzese.
Lakini umewatoa muziki hao kina Sugu? Umaarufu sio pesa. Madee kachana ukweli usiopendeza lakini ni ukweli. Hip hop ina washabiki wengi lakini ni tabaka la wasio na pesa. Kimapato huwezi kuifananisha hata na taarab, kina Joh makini, bonta, fid nk wana nini?
 
Basi kama HiP Hop haipo kibiashara inabidi msanii wa hip hop awe anafanya shughuli ingine ya kumuingizia kipato na kulea familia kama anayo na kufanya itikadi za hip hop kinyume na hapo ni maisha magumu kwenda mbele kitu ambacho wasanii wengi hawakitambui
 
HIP HOP means Higher Infinity Power Healing Our People.... Kama kuuza hata wangese wanauza tiGO na wanapiga pesa
Mkuu mbona mbona unyamwezini wakina jay z, kanye, dr dre na drake wanapiga pesa ndefu sana
 
Mimi namkubali maalim Nash MC kwanza anatumia Kiswahili fasaha na anafata misingi ya hip hop Na ni mwanaharakati kweli
 
Back
Top Bottom