MaDC na maRC wanatolea wapi kiburi!

Luqman mohamedy

JF-Expert Member
Jul 24, 2016
892
1,226
Kilichonisukuma kuandika uzi huu ni kuhusu strory inayotrend ya DC kumchapa viboko mzaz wa mtot aliyepasua kioo cha gari lake na kuchoshwa na kukua kwa viburi vya baadhi ya maDC na MaRC na kujikuta Miungu watu na kuwatreat watu jinsi wapendavyo wao kwakua wakidhani hawana mandate ya kuwang'oa katika nafasi yao.
Tabia hii pia imeonekana na baadhi ya maRC
Imeonekana kazi kubwa ya maDC na maRC ni kuziimpress media pamoja na aliowateua na si wanaowatumikia.
Wakiondolewa wao tunao wawakilishi wetu na watumishi wengine kibaooo so hata kama wako kikatiba hatuwataki unless wabadilike.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Tathimini hizi zitajitokeza baada ya utawala huu kumaliza muda wake!!
 
wanapata viburi kutoka kwa bos kubwa, wao wameteuliwa tu, sio viongozi wa kuchaguliwa ni jambo la ajabu sana katika nchi yenye democracy kuwa na viongozi wenye nguvu kiasi hiki kisha wasiwe wamechaguliwa na wananchi

rc ni mkuu wa mkoa wote na raisi ni mkuu wa nchi nzima,kiuhalisia madc/rc walikuwa wapigiwe kura ili kuwahudumia wananchi wa mikoa yao,wananchi wa mikoa husika wachague wakuu wao wa mikoa na sio kupelekewa mtu asiekuwa na mahusiano nao na asiejua wala kujali shida zao
 
Kavunja mtoto mzazi anachapwaje? Huyu mzazi apatiwe msaada wa kisheria amshitaki DC kumsababishia maumivu na kumdhalilisha. Wanasheria jitokezeni mmsaidie huyu mzazi alichofanyiwa ni unyanyasaji mkubwa

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Siku wanaapishwa waliambiwa na mkuu waendee wakaimplement ile sheria ya kumweka mtu ndani masaa 48. Nadhani wengi wanajua kwamba wao ni maRAIS na Wafalme ndani ya Mikoa/Wilaya zao na wanaweza kufanya lolote, sasa yoyote bila ruhusa ya yeyote. Wanaakisi mienendo ya boss wao.
 
Mfumo ndio unaowapa kiburi. Tumewapa nguvu nyingi mfano eti wao ndio wenyeviti wa kamati ya ulinzi na kwamba wanaweza mweka mtu ndani masaa 48 na polisi wanatii. Hivyo siku tukiwa na DC kichaa ujue ni noma noma maana atawafanya watu ambendavyo.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hawa ma DC uchwara wamkumbuke Dr. Kleruu aliekuwa mkuu wa mkoa wa iringa alifumuliwa kifua kwa risasi na mkulima Saidi Mwamwindi kwa mambo ya kipumbav yanayofanana na ya huyo DC ingekuwa mimi tungegawana taasisi yeye angeishia uzazi na vifo nami ningeishia wizara ya mambo ya ndani ujumbe ungefika kwa waliobaki duniani
 
Hawa vijana wenzetu baada ya kupewa madaraka na elimu zao za KKK yamewalevya kukandamiza kuwadhalilisha watumish na wananch waliochin yao...
Tofaut na madc/rc watu wazima wanakuwaga na hekima hata kwny maamuz yao huwa na weled sana...
Hata wale wanajeshi waliopewa ofis hawana ubabe wakipuuz...
.
.
KKK ndio tatzo lao kubwa
 

Similar Discussions

2 Reactions
Reply
Back
Top Bottom