Madawati ya Bil 78.7 Chenji ya Rada?

tatizo tunachagua watu kuingia bungeni kudai posho zao badala ya kujadili mambo ya msingi si ccm wala ukawa hilo jambo nilitegemea lingeulizwa kwenye maswali ya papo kwa papo badala yake wamekaa kupigana vijembe
 
CHADEMA siku zote mnapinga maendeleo ya Tanzania. Hakuna anayewasikiliza sasa. Madawati yamepatikana na yanaendelea kupatikana. Alioguswa wamechangia. Ninyi ambao hamjaguswa endeleeni kukaa kimya
Jamaa anaulizia chenji ya Rada povu zanini? Siumjibu tu?
 
Hili limejibu vipi hoja ya Rada? Hoja iliyopo ni Rada!
Wewe ndiye unatakiwa ufuate mtiririko wa hoja bila kudandia treni kwa mbele.

Unachofanya hapa ni kudandia hoja kwa mbele na matokeo yake hufahamu hata vigezo vilivyotumika kufika kwenye comment uliyo quote.
 
Kuipa ridhaa CCM muda mrefu kwa sasa siyo hoja, hoja ni nani atakayechukua nafasi ya CCM? Rais wa Tanzania atakuwa ni nani?

kwa hio wewe kwa mtazamo wako finyu unadhani watanzania milioni 45 hakuna mtu anayefaa isipokuwa atoke CCM? Hata hivyo of the recent tumepata chaguo bovu kabisa ambalo vizazi vyetu vijavyo hadi kizazi cha sita vitauja kujuta...Point is CCM kwa sasa haina uwezo wa kuiponya nchi hii...Inapaswa ife aje hata Rungwe Hashim kwa sababu anaweza kuwa bora mara milioni kuliko Wezi wazoefu CCM.

Mwl. Nyerere aliposema ili nchi iendelee inahitaji watu hakuna na maana ya watu wengi wasiojitambua, bali alikuwa na maana ya watu wanaojitambua. Huwezi kuwa na taifa la watu vigeugeu halafu ukategemea kusimamia falsafa na itikadi za kimaisha achilia mbali siasa.

Lakini endapo Taifa hili la Tanzania haliendelei kwa sababu ya watu wasiojitambua......hiyo bado inarudi kwenye utawala mbovu wa CCM ....CCM imetengeneza na kulea ujinga kwa muda mrefu....Hivyo basi..ninavyokwambia Root Cause ya matatizo ya nchi hii ni Utawala Mbovu wa CCM uliofeli hata kutengeneza Skilled and knowledgeable Human Reources namaanisha

Hii ni mpya, kwamba unatoa hukumu halafu baadaye unatafakari na kutafuta ushahidi. Hii ni sawa ni kusema, unaua halafu baadaye ndiyo unaanza kutafakari na kutafuta ushahidi. Hii ni dhana ya kutojitambua!

Nadhani hii sio hoja ya msingi sana...Be Objective

Kumekuwapo kuchangishana fedha nyingi tuu kwa hiari na lazima kwa ajili ya ununuzi wa Madawati.
Pila lipo tishio pale ambapo RC, DC, REO,DEO hata mtendaji wa kata kutumbuliwa ikiwa zoezi LA madawati halita kamilika.
Lakini mbona serikali haijatueleza zile pesa tulizokuwa tumeibiwa na kampuni ya BAE System ya UK kwa msaada wa wenzetu wachache kina Change na zikarudishwa Bil 78.7 (figure inaweza rekebishwa) na kupelekwa kwenye madawati mbona kimya?
Hizo ni fedha nyingi sana, na kama zingenunua kweli hayo madawati pengine tatizo lingeisha au kuwa dogo la kawaida lisilohitaji kampeni kiasi hiki.
Au na Chenji ya Rada nayo ilipigwa? Na kama ilipigwa mtumbuaji mbona yuko kimya na wengine sasa hivi ndio wanakosa amani kuchangisha wasio na fedha?
 
Wewe ndiye unatakiwa ufuate mtiririko wa hoja bila kudandia treni kwa mbele.

Unachofanya hapa ni kudandia hoja kwa mbele na matokeo yake hufahamu hata vigezo vilivyotumika kufika kwenye comment uliyo quote.
Nimefuatilia kika bandiko, ninachokiona ni wewe kubadili hoja ya rada kwa kuleta mada nyingine.

Hili si jambo geni ndio utaratibu wako wa kuharibu mada ambao wenye macho na fikra wanaujua

Umeulizwa simple tu,pesa za rada vipi? Hayo mengine hayahusiana na mada wala hayana tija kuyasoma.
 
Ahsante kwa taarifa hii.

Turudi kwenye mada, pesa za rada vipi kama alivyouliza mchokoza mada?
Kujibu moja kwa moja kuwa zimeliwa na walio kula wawajibishwe hawataki.
Lakini kesho wakisikia John anatangaza kumwajibisha mtu kwa fedha za chenji ya Rada watakuja hapa kwa speed kupongeza na kusifu kwa mapambio.
Ndio unafiki ulipo ota mizizi, nafasi ya kusema hawasemi ila jamaa akitusikiliza akatenda wanatugeuzia kibao kuwa ni idea yao
 
kwa hio wewe kwa mtazamo wako finyu unadhani watanzania milioni 45 hakuna mtu anayefaa isipokuwa atoke CCM? Hata hivyo of the recent tumepata chaguo bovu kabisa ambalo vizazi vyetu vijavyo hadi kizazi cha sita vitauja kujuta...Point is CCM kwa sasa haina uwezo wa kuiponya nchi hii...Inapaswa ife aje hata Rungwe Hashim kwa sababu anaweza kuwa bora mara milioni kuliko Wezi wazoefu CCM.

Sijasema hakuna watanzania wa kuongoza Tanzania, ninachotaka kufahamu ni chama chenye uwezo ambacho kitatoa Rais wa Tanzania mwenye uwezo zaidi ya uliopo.

Kusema kwa kutumia hisia kuwa tumechagua chaguo bovu kabisa hakuwezi kuondoa msingi wa hoja yangu kwa sababu kuna wengine watakuambia tumechagua chaguo bora kabisa.

Ni nani anafaa kuwa Rais wa Tanzania zaidi ya hili unalodai ni chaguo bovu kabisa.
Lakini endapo Taifa hili la Tanzania haliendelei kwa sababu ya watu wasiojitambua......hiyo bado inarudi kwenye utawala mbovu wa CCM ....CCM imetengeneza na kulea ujinga kwa muda mrefu....Hivyo basi..ninavyokwambia Root Cause ya matatizo ya nchi hii ni Utawala Mbovu wa CCM uliofeli hata kutengeneza Skilled and knowledgeable Human Reources namaanisha
Lengo namba moja la chama chochote cha siasa ambacho kiko serious ni kushinda uchaguzi mkuu.

Kama CCM wanashinda uchaguzi wakati utawala wao ni mbovu, basi tatizo siyo la CCM bali ni tatizo la vyama vinavyopambana na CCM.

Badala ya kuilalamikia CCM inayochaguliwa, ingekuwa ni vizuri pia kuviangalia vyama vya upinzani ambavyo havichaguliwi pamoja na uwepo wa ubovu wa CCM.
Nadhani hii sio hoja ya msingi sana...Be Objective

Kumekuwapo kuchangishana fedha nyingi tuu kwa hiari na lazima kwa ajili ya ununuzi wa Madawati.
Pila lipo tishio pale ambapo RC, DC, REO,DEO hata mtendaji wa kata kutumbuliwa ikiwa zoezi LA madawati halita kamilika.
Lakini mbona serikali haijatueleza zile pesa tulizokuwa tumeibiwa na kampuni ya BAE System ya UK kwa msaada wa wenzetu wachache kina Change na zikarudishwa Bil 78.7 (figure inaweza rekebishwa) na kupelekwa kwenye madawati mbona kimya?
Hizo ni fedha nyingi sana, na kama zingenunua kweli hayo madawati pengine tatizo lingeisha au kuwa dogo la kawaida lisilohitaji kampeni kiasi hiki.
Au na Chenji ya Rada nayo ilipigwa? Na kama ilipigwa mtumbuaji mbona yuko kimya na wengine sasa hivi ndio wanakosa amani kuchangisha wasio na fedha?
Yes, kuna uwezekano chenji ya Rada ilipigwa.

Unachokifanya hapa ni sawa na kuuliza bunge la 11 kuhusu sheria zilizotungwa na bunge la 10 eti kwa sababu kuna baadhi ya wabunge walikuwa kwenye bunge la kumi ambao wamechaguliwa tena kwenye bunge la 11.

Hii ni serikali ya awamu ya tano wakati chenji ya Rada ilifanyika wakati wa awamu ya nne.
 
Ahsante kwa taarifa hii.

Turudi kwenye mada, pesa za rada vipi kama alivyouliza mchokoza mada?
Baadhi ya pesa za chenji ya Rada kuna uwezekano mkubwa zimeenda kwenye mifuko ya watu ''wajanja'' kwa sababu mpaka serikali ya awamu ya nne inamaliza muda wake, hatukuweza kupata majibu sahihi.
 
Nimefuatilia kika bandiko, ninachokiona ni wewe kubadili hoja ya rada kwa kuleta mada nyingine.

Hili si jambo geni ndio utaratibu wako wa kuharibu mada ambao wenye macho na fikra wanaujua

Umeulizwa simple tu,pesa za rada vipi? Hayo mengine hayahusiana na mada wala hayana tija kuyasoma.
Ungekuwa umefuatilia kila bandiko nadhani ungefahamu kuwa haya unayodai hayahusiani na mada yameanzishwa na yule niliyekuwa nime-quote comment yake.

Hiyo hoja mwambie yeye na siyo mimi ambaye nimejibu kulingana na comment yake.
 
Sijasema hakuna watanzania wa kuongoza Tanzania, ninachotaka kufahamu ni chama chenye uwezo ambacho kitatoa Rais wa Tanzania mwenye uwezo zaidi ya uliopo.

Kusema kwa kutumia hisia kuwa tumechagua chaguo bovu kabisa hakuwezi kuondoa msingi wa hoja yangu kwa sababu kuna wengine watakuambia tumechagua chaguo bora kabisa.

Ni nani anafaa kuwa Rais wa Tanzania zaidi ya hili unalodai ni chaguo bovu kabisa.

Lengo namba moja la chama chochote cha siasa ambacho kiko serious ni kushinda uchaguzi mkuu.

Kama CCM wanashinda uchaguzi wakati utawala wao ni mbovu, basi tatizo siyo la CCM bali ni tatizo la vyama vinavyopambana na CCM.

Badala ya kuilalamikia CCM inayochaguliwa, ingekuwa ni vizuri pia kuviangalia vyama vya upinzani ambavyo havichaguliwi pamoja na uwepo wa ubovu wa CCM.

Yes, kuna uwezekano chenji ya Rada ilipigwa.

Unachokifanya hapa ni sawa na kuuliza bunge la 11 kuhusu sheria zilizotungwa na bunge la 10 eti kwa sababu kuna baadhi ya wabunge walikuwa kwenye bunge la kumi ambao wamechaguliwa tena kwenye bunge la 11.

Hii ni serikali ya awamu ya tano wakati chenji ya Rada ilifanyika wakati wa awamu ya nne.
Unao uhakika wanachaguliwa? Mbona kuna kasoro nyingi zinatajwa na sio wapinzani wa ccm tuu bali hata observers wa nje?
Ndio maana unahitajika uwanja huru wa mchezo huo
 
Asante sana kwa kuweka hizi links.
Sasa tujiulize kama hela iliyokuwa imekusudiwa madawati imeliwa kwa njia haramu na serikali, Viongozi wanapata wapi moral authority ya kuwabana na kutishia kuwafukuza kazi wakishindwa kuwachangisha (kuwakamua) wananchi michango ya madawati?
Madawati ni muhimu, lakini kweli ni sahihi kunyang'anya masikini mbuzi au kuku kwa vile hana cash wakati waliolamba mabilioni ya hayo madawati wanatanua na ma V8?
 
Acha kupotosha katika hili. Unataka kutuambia haya yote anayotumbua Magufuli ni wizi na ubadhilifu uliofanyika awamu ya tano?
Wizi (kama upo) wa hela ya Rada hauna tofauti na NIDA, Makontena, DART nk nk ambayo yalifanyika huko nyuma na rais anachukua hatua
 
Hii taarifa ilitumika kuwahadaa kondoo na kuwapiga changa la macho wadanganyika.
Link Matumizi ya Chenji ya Rada - Bilioni 77.8 | Pmoralg - Tanzania
 
Unao uhakika wanachaguliwa? Mbona kuna kasoro nyingi zinatajwa na sio wapinzani wa ccm tuu bali hata observers wa nje?
Ndio maana unahitajika uwanja huru wa mchezo huo
Kusema wanachaguliwa au hawachuliwi ni kuingia kwenye mjadala mwingine ambao ni mpana zaidi kwa sababu hakuna mchakato hapa duniani ambao hauna mapungufu.

Kama wewe ni timu na ukaamua kuingia kwenye uwanja kucheza mpira, hiyo itahesabika umekubaliana na taratibu na pia sheria za mchezo.

Hii dhana ya kushindwa mchezo halafu wanaanza kulalamika tu kuhusu taratibu na sheria ambazo walikubali kuzitumia katika mchezo inaleta taswira ya kuukimbia ukweli.

Kama wanafahamu taratibu na sheria ni mbovu, kwa nini wasisusie kuingia uwanjani?
 
Acha kupotosha katika hili. Unataka kutuambia haya yote anayotumbua Magufuli ni wizi na ubadhilifu uliofanyika awamu ya tano?
Wizi (kama upo) wa hela ya Rada hauna tofauti na NIDA, Makontena, DART nk nk ambayo yalifanyika huko nyuma na rais anachukua hatua
Hakuna ninachopotosha.

Kwani ni kina nani walioiba pesa ya chenji ya Rada ambayo ilitakiwa kutengenezea madawati?
 
Mbona kujiwekea taadhari mapema swala chenji ya lada wapi
 
Similar Discussions

8 Reactions
Reply
Back
Top Bottom