Madawa ya Kulevya Tanzania, Serikali Yetu Hamyaoni Yanatumaliza?

anney

Senior Member
Jul 9, 2010
155
45
Wana JF, Nimeangalia hivi sasa serikali yetu imesahau jukumu la kulinda maisha ya watanzania hasa tatizo la madawa ya kulevya. Tatizo limekuwa kubwa kiasi kwamba siku hizi huhitaji nguvu kuyapata. Vijana wanasema unaweza kupiga simu ukaletewa. Jamani tutafika? Raisi wetu Jamhuri kuna wakati ulituambia unayo majina ya wauza madaya ya kulevya, ingawa wakati wa kampeni sijakusikia ukiongelea madawa ya kulevya basi chonde chode baba taifa linaangamia chukua hatua. Kitengo cha kupambana na dawa za kulevya mmelala? Msaidieni raisi.
Kwa taarifa watu wanaokamatwa viwanja vya ndege ni vidagaa vya madawa ya kulevya, Nyangumi wametulia tu wanatuaharibia watoto wetu. Watoto wetu mjini madaya kulevya yanawamaliza, kijijini GONGO limeshatulemaza, taifa tunaelekea wapi.
WanaJF tufanyeji na hili tatizo? Mi naona tulioonezee kwenye agenda ya Ufisadi. Yaani maandamano ya wananchi wote yafanyika katika miji mikuu kwa ajenda zifuatazo.
1. Madawa ya kulevya
2. Ufisadi wa rasilimali za umma
3. matokeo mabaya ya kidato cha nne
4. Umeme.
Nashauri upinzani waungane, Pressure groups (mf. Tamwa,hakielimu, utu mwanamke,NGOs nk) kwa hili na watanzania wenye mapenzi mema.
 
Serikali ni kiziwi hawawezi sikia pole sana... kuanzia juma kilaza na mafisadi wenzake... hata kaimbiwa wimbo wa mjomba awe anasikia ushauri wa bure lakini wapi nimegundua jamaa ni kilaza mjomba hata tukipata nauri hatuji yaelekea hujasafisha masikio yako tokea darasa la tano mjomba j.k.(Juma Kilaza)
 
This is worse than Mwinyi's era. Wakati huo tuliambiwa kuwa serikali iko likizo. This time serikali iko AWOL. Ndio maana mafisadi wanatamba.
 
Serikali na watu wake wataishije? 'Bonus' zao zinatoka humo.

Haf ukionekana unaongelea sana haya mambo utaambiwa kuna taarifa za kiintelijensia unataka kuchafua amani nchini
 
Ukifuatia hasa wanaoleta madawa hayo ni watoto wa vigogo,,,,,,tena mitaani wanatembea kwa kutanua
 
Back
Top Bottom