100% nashukuru sana kwa kuelewa hili vyema na kilichomaanishwa ni kipi!!Kwa jinsi nilivyomuelewa mtoa mada hajamaanisha hela ya serikali itumike kwa wala Unga, bali hao vijana walioathirika watumike kuwabaini wauzaji vivyovivyo back wise hadi kuwapata importers. Na kwa kuongezea wakishabainika na kuthibitishwa wafanyiwe kile anachofanya Rais wa Philippines ndugu Rodrigo Dutetre. Kusema serikali isihangaike nao kuwa ni maisha waliojichagulia sio sahihi, leo ni kwa Chidi Benz kesho akinasa ndugu yako wakaribu utaona umuhimu wa serikali kulivalia njuga suala la drugs.
Hujui unachoongea,mabadiliko ya kweli ya MTU huanza na yeye mwenyewe na si kutumia nguvu ktk kumbadilisha ktk social life.sio kweli mtu akiwa ameathirika na madawa ya kulevya,then kuacha ni maamuzi yake mwenyewe,ukiingia huko huelewi kinachoendelea unless watu wako wa karibu wahangaike na wewe mpaka upone.
Hujui unachoongea,mabadiliko ya kweli ya MTU huanza na yeye mwenyewe na si kutumia nguvu ktk kumbadilisha ktk social life.
Na hiyo ndiyo ilivyo kwa watuamiaji wa madawa ya kulevya.
Kama hajaamua kubadilika toka moyoni mtatumia mbinu zote lakini akipata nafasi anarudi kulekule.
Na akiamua kubadilika kwa dhati then issue zingine za kumweka zinakuwa rahisi sana na supportive kwa mtaka mabadiliko.
kama hujui vzr, mvuta unga hata umsaidie vp , hawez akaacha kuvuta ndugu yangu, na kama unakumbuka vzr rais wa awamu iliyopita alifanya juhud za makusud kumsaidia yule dada mwanamuziz ray . lakin umeona kilichotokea?
Hata akiwa addicted kiasi gani still bado mabadiliko yanaanza na yeye mwenyewe wewe utalazima kumbadilisha kama hajaamua hatabadilika.easier said than done,,unadhania ukiwa tayari addict,ni rahisi kuacha kama kuvaa nguo Fulani na kuvua???,
Eti hajaamua kubadilika moyoni,unavyoona kuna mtu anapenda kwa utashi wake kudhoofu,mpaka kila mtu anamshangaa....,kuwa gumzo kwenye media?
Nakusihi angalia picha za chid,afu ujiulize mtu wa hivi anapenda kweli kufikia alipofikia?
Happy new year.
Umenena vyema........ Mwigulu Nchemba inaonekana wizara hii imemshinda. Mimi ni miongoni mwa watu niliosifia uteuzi wake wizazra husika. Ila kwa sasa naona Tz tatizo siyo madawa tu, bali wizi, ujambazi, hasa Dar, na kibaya hakuna dalili za kuisha wala kutafutiwa ufumbuzi. Natamani wizara ile angepatikana kama Mrema. Mfano, kwanini wizi wa vifaa vya magari dar umeshamiri sana na wezi wanajulikana walipo na waziri yupo tu anakenue meno??? Kwa nini uvamizi umeshamiri na waziri yupo tu na hakuna mkakati?? Kwa nini watumia madawa wapo wanazagaa mitaani na waziri yupo tu??? I hate politics kwenye mambo ya msingi. Nchi haiwezi kuendelea in terms of viwanda kuwa na utulivu.
So kuna watu walisema serikali hii imewamaliza wauza unga?May be Child anatumia akiba aliyokuwa nayoKwa kuwa serikali imekuwa ikitangazia umma kuwa inapambana na madawa ya kulevya kwa juhudi zote, sasa ionyeshe umma kuwa haijashindwa chochote kwenye hili suala!
Kwanza kuna huyu anayeitwa Chid Benz sijui ni kwanini hadi hivi sasa serikali imekaa kimya kuhusu hili suala lake, imeshathibitika kwamba huyu mtu ni drug abuser, ameshaathirika sana na madawa ya kulevya, hivi ni kwanini serikali haitaki kumsaidia kama ina nia ya dhati kabisa ya kupambana na madawa ya kulevya..
Anaachwa tu aendelee kutumia aangamie..?
Ni vijana wangapi kama huyu Chid wapo katika hali aliyonayo huyu Chid benz..?
Binafsi huwa nakutana na vijana wengi mno ambao wapo kwenye hali mbaya sana ambao wameshakuwa addicted!
Sasa kama haijulikani hao wauzaji wanapatikana wapi mbona njia ya kuwapata ni rahisi sana.
Hawa vijana ambao ni addicted wakamatwe au wapelekewe wapelelezi wanaweza kujifanya wao ni watumiaji wakadeal na hawa addicted mwisho wa siku ikajulikana wanakoyapata na hatimaye huo mtandao kunaswa!
Au ni kwamba wapo vigogo wa serikali waliopo kwenye huu mtandao wa kuuza madawa ya kulevya?
Huyu chid ataangamia tukiwa tunamuona na wala haitasaidia chochote kama hatu stahiki zisipochukuliwa mapema, achukuliwe asaidie huko anakoyapata ili tuokoe vijana wengine!
Wakichukuliwa vijana kadhaa ambao ni addicted wakataja huo mtandandao itasaidia sana kuokoa kizazi hiki, kuwapeleka sorber haitasaidia sana, kikubwa tudeal na ile source wapi wanayapata!
Nawasilisha
Well said...Hili suala kwa kweli inabidi litazamwe kwa jicho la tatu..
Na siyo kupiga tu kelele vijana wanaaangamia pasipo kuchukua hatua stahili, hatuwezi kusema tumwache mwizi aendelee tu kuiba eti atajirekebisha mwenyewe!!
Mtoa mada naungana na wewe tunahitaji nia ya dhati kutokemeza hili janga lakini tumekuwa na mikakati mibovu, wauzaji wanajulikana lakini bila shaka kuna viongozi wenye maslahi kwenye hili suala na ndio wanaotuangusha kwa kweli!!