Madawa ya kulevya; Serikali kama ina nia ya dhati kutokomeza ianzie hapa kwa sasa!!

Ray C alisaidiwa na awamu ya NNE wamuulize ni wapi aliyapata
 
Kwa jinsi nilivyomuelewa mtoa mada hajamaanisha hela ya serikali itumike kwa wala Unga, bali hao vijana walioathirika watumike kuwabaini wauzaji vivyovivyo back wise hadi kuwapata importers. Na kwa kuongezea wakishabainika na kuthibitishwa wafanyiwe kile anachofanya Rais wa Philippines ndugu Rodrigo Dutetre. Kusema serikali isihangaike nao kuwa ni maisha waliojichagulia sio sahihi, leo ni kwa Chidi Benz kesho akinasa ndugu yako wakaribu utaona umuhimu wa serikali kulivalia njuga suala la drugs.
100% nashukuru sana kwa kuelewa hili vyema na kilichomaanishwa ni kipi!!
Naamini ulichoandika watakielewa vyema zaidi hao wanaoonekana kutokuelewa hii mada!!
 
sio kweli mtu akiwa ameathirika na madawa ya kulevya,then kuacha ni maamuzi yake mwenyewe,ukiingia huko huelewi kinachoendelea unless watu wako wa karibu wahangaike na wewe mpaka upone.
Hujui unachoongea,mabadiliko ya kweli ya MTU huanza na yeye mwenyewe na si kutumia nguvu ktk kumbadilisha ktk social life.

Na hiyo ndiyo ilivyo kwa watuamiaji wa madawa ya kulevya.

Kama hajaamua kubadilika toka moyoni mtatumia mbinu zote lakini akipata nafasi anarudi kulekule.

Na akiamua kubadilika kwa dhati then issue zingine za kumweka zinakuwa rahisi sana na supportive kwa mtaka mabadiliko.
 
Tunahitaji viongozi aina ya rais wa philippine hii. Kitu INA madhara makubwa kwa jamii tukitaka kuishugulikia tufumbe masikio wala tusisikilize makelele ya hao wanaojiita watetezi wa haki za binadamu
 
Anaetakiwa kumkamata muuzaji ndio muuzaji mwenyewe..kwa hy unashauri ajikamate?Haitatokea
 
Hujui unachoongea,mabadiliko ya kweli ya MTU huanza na yeye mwenyewe na si kutumia nguvu ktk kumbadilisha ktk social life.

Na hiyo ndiyo ilivyo kwa watuamiaji wa madawa ya kulevya.

Kama hajaamua kubadilika toka moyoni mtatumia mbinu zote lakini akipata nafasi anarudi kulekule.

Na akiamua kubadilika kwa dhati then issue zingine za kumweka zinakuwa rahisi sana na supportive kwa mtaka mabadiliko.

easier said than done,,unadhania ukiwa tayari addict,ni rahisi kuacha kama kuvaa nguo Fulani na kuvua???,

Eti hajaamua kubadilika moyoni,unavyoona kuna mtu anapenda kwa utashi wake kudhoofu,mpaka kila mtu anamshangaa....,kuwa gumzo kwenye media?

Nakusihi angalia picha za chid,afu ujiulize mtu wa hivi anapenda kweli kufikia alipofikia?

Happy new year.
 
kama hujui vzr, mvuta unga hata umsaidie vp , hawez akaacha kuvuta ndugu yangu, na kama unakumbuka vzr rais wa awamu iliyopita alifanya juhud za makusud kumsaidia yule dada mwanamuziz ray . lakin umeona kilichotokea?
 
Kwa ujumla wapo wengi walioathirika ila huyu jamaa anatolewa mfano kwa umuhimu wake katika tasnia.
 
..... Mwigulu Nchemba inaonekana wizara hii imemshinda. Mimi ni miongoni mwa watu niliosifia uteuzi wake wizazra husika. Ila kwa sasa naona Tz tatizo siyo madawa tu, bali wizi, ujambazi, hasa Dar, na kibaya hakuna dalili za kuisha wala kutafutiwa ufumbuzi. Natamani wizara ile angepatikana kama Mrema. Mfano, kwanini wizi wa vifaa vya magari dar umeshamiri sana na wezi wanajulikana walipo na waziri yupo tu??? Kwa nini uvamizi umeshamiri na waziri yupo tu na hakuna mkakati?? Kwa nini watumia madawa wapo wanazagaa mitaani na waziri yupo tu??? I hate politics kwenye mambo ya msingi. Nchi haiwezi kuendelea in terms of viwanda kama hakuna usalama wa raia na mali zao.
 
Police hawajui madawa yalipo bt chid benz na hali yake anajua yalipo na anaomba na chenchi
 
easier said than done,,unadhania ukiwa tayari addict,ni rahisi kuacha kama kuvaa nguo Fulani na kuvua???,

Eti hajaamua kubadilika moyoni,unavyoona kuna mtu anapenda kwa utashi wake kudhoofu,mpaka kila mtu anamshangaa....,kuwa gumzo kwenye media?

Nakusihi angalia picha za chid,afu ujiulize mtu wa hivi anapenda kweli kufikia alipofikia?

Happy new year.
Hata akiwa addicted kiasi gani still bado mabadiliko yanaanza na yeye mwenyewe wewe utalazima kumbadilisha kama hajaamua hatabadilika.

Utegemezi au addiction huwezi kutumia nguvu kuiondoa kwa mtu kama haitoki ndani.pata concept sio issue ya Huruma hapo kwasababu kuna MTU anadhalilika ktk media.

Pata kwanza kujua heroin ni nini elewa cocaine ni nini inafanyaje kazi mwilini mtumiaji kwanini anatumia na anafurahia nini mpaka anafikia kuwa addicted ndiyo utafahau.

Kama hataamua kuacha kutumia yeye mwenyewe wewe nafasi yako ya kusaidia ni kidogo sana kufika mafanikio.
 
..... Mwigulu Nchemba inaonekana wizara hii imemshinda. Mimi ni miongoni mwa watu niliosifia uteuzi wake wizazra husika. Ila kwa sasa naona Tz tatizo siyo madawa tu, bali wizi, ujambazi, hasa Dar, na kibaya hakuna dalili za kuisha wala kutafutiwa ufumbuzi. Natamani wizara ile angepatikana kama Mrema. Mfano, kwanini wizi wa vifaa vya magari dar umeshamiri sana na wezi wanajulikana walipo na waziri yupo tu anakenue meno??? Kwa nini uvamizi umeshamiri na waziri yupo tu na hakuna mkakati?? Kwa nini watumia madawa wapo wanazagaa mitaani na waziri yupo tu??? I hate politics kwenye mambo ya msingi. Nchi haiwezi kuendelea in terms of viwanda kuwa na utulivu.
Umenena vyema...
 
Kwa kuwa serikali imekuwa ikitangazia umma kuwa inapambana na madawa ya kulevya kwa juhudi zote, sasa ionyeshe umma kuwa haijashindwa chochote kwenye hili suala!

Kwanza kuna huyu anayeitwa Chid Benz sijui ni kwanini hadi hivi sasa serikali imekaa kimya kuhusu hili suala lake, imeshathibitika kwamba huyu mtu ni drug abuser, ameshaathirika sana na madawa ya kulevya, hivi ni kwanini serikali haitaki kumsaidia kama ina nia ya dhati kabisa ya kupambana na madawa ya kulevya..
Anaachwa tu aendelee kutumia aangamie..?

Ni vijana wangapi kama huyu Chid wapo katika hali aliyonayo huyu Chid benz..?

Binafsi huwa nakutana na vijana wengi mno ambao wapo kwenye hali mbaya sana ambao wameshakuwa addicted!

Sasa kama haijulikani hao wauzaji wanapatikana wapi mbona njia ya kuwapata ni rahisi sana.

Hawa vijana ambao ni addicted wakamatwe au wapelekewe wapelelezi wanaweza kujifanya wao ni watumiaji wakadeal na hawa addicted mwisho wa siku ikajulikana wanakoyapata na hatimaye huo mtandao kunaswa!

Au ni kwamba wapo vigogo wa serikali waliopo kwenye huu mtandao wa kuuza madawa ya kulevya?

Huyu chid ataangamia tukiwa tunamuona na wala haitasaidia chochote kama hatu stahiki zisipochukuliwa mapema, achukuliwe asaidie huko anakoyapata ili tuokoe vijana wengine!

Wakichukuliwa vijana kadhaa ambao ni addicted wakataja huo mtandandao itasaidia sana kuokoa kizazi hiki, kuwapeleka sorber haitasaidia sana, kikubwa tudeal na ile source wapi wanayapata!

Nawasilisha
So kuna watu walisema serikali hii imewamaliza wauza unga?May be Child anatumia akiba aliyokuwa nayo
 
Kwani sikuna mwaka huyu mtoto wa mstaafu JJjjJjjjjjjj alikamatwa huko China kesi ilikuwa ni mahfjsjcjsjcjs na akaachiwa huru hivyo muhusika wa madawa anajudjdjshcjsjfjsf ila tunafjsjfjsjf tu
 
Hili suala kwa kweli inabidi litazamwe kwa jicho la tatu..
Na siyo kupiga tu kelele vijana wanaaangamia pasipo kuchukua hatua stahili, hatuwezi kusema tumwache mwizi aendelee tu kuiba eti atajirekebisha mwenyewe!!
Mtoa mada naungana na wewe tunahitaji nia ya dhati kutokemeza hili janga lakini tumekuwa na mikakati mibovu, wauzaji wanajulikana lakini bila shaka kuna viongozi wenye maslahi kwenye hili suala na ndio wanaotuangusha kwa kweli!!
 
madhara ya madawa sio watumiaji pekee.pia kama taifa.we need to do something
 
Hili suala kwa kweli inabidi litazamwe kwa jicho la tatu..
Na siyo kupiga tu kelele vijana wanaaangamia pasipo kuchukua hatua stahili, hatuwezi kusema tumwache mwizi aendelee tu kuiba eti atajirekebisha mwenyewe!!
Mtoa mada naungana na wewe tunahitaji nia ya dhati kutokemeza hili janga lakini tumekuwa na mikakati mibovu, wauzaji wanajulikana lakini bila shaka kuna viongozi wenye maslahi kwenye hili suala na ndio wanaotuangusha kwa kweli!!
Well said...
 
9 Reactions
Reply
Back
Top Bottom