Madawa ya Kulevya: Mtanzania aishie Marekani ashtakiwa kwa kuingiza heroin nchi humo

EMT

Platinum Member
Jan 13, 2010
14,483
15,308
Mtanzania aishie Marekani ameshtakiwa kwa kuhusika katika njama ya kimataifa ya kuingiza heroin nchni humo kutoka Tanzania. Mamlaka husika huko Marekani wamemtaja Mtanzania huyo kuwa ni Allen Jordan Baisi (34) na anahusika kwenye mtandao wa kimataifa wa kuingiza madawa ya kulevya Marekani kwa kutumia vifurishi vinavyotumwa kutoka Tanzania kwenda kwa "wateja" mbalimbali Marekani.

Hata hivyo, "wateja" hao walikutwa kuwa ni wasaidizi wake wakuu katika biashara yake haramu ya heroin. Kwa mujibu wa nyaraka za kimahakama, mtandao wake unajumuisha kusafirisha heroin iliyofichwa ndani ya soli za makubadhi (sandals) kwenye vifurushi vilivyokuwa vinatumwa kutoka Tanzania kwenda kwenye anwani za nyumbani zilizoko katika kaunti ya Muskegon.

Kwa mujibu ya wa tovuti ya mlive.com, Allen Jordan Baisi, ambaye anaishi Mount Prospect, Ill, alikamtwa huko Illinois na kushshtakiwa mwezi Octoba mwaka huu kwa kosa la kujihusisha kusambasa karibu gramu 100 za heroin na kosa la money laundering. Kwa mujibu wa nyaraka za kimahakama, Allen Jordan Baisi, ni Mtanzania na alikamatwa kwenye trafiki September 22 mwaka akiwa njia kuelekea uwanja wa ndege kuja Tanzania. Kesi yake itaanza kusikilizwa Januari 6, 2015.

Bw. Baisi anashtakiwa pamoja na watuhumiwa wengine ambao wanajulikana kwa majina na wengine hawajulikani. Waendesha mashtaka wanadai kuwa heroin ilikuwa inafichwa kwenye vifurishi vya nguo ambavyo vilikuwa zinatumwa kwenye anuani za nyumbani zilizopo katika kaunti ya Muskegon na kuwa mtu mwingine ambaye nyaraka za kimahakama zinamtambulisha kama "Individual A" alikuwa anapokea heroin hiyo na kuisambaza eneo hilo. Mtu huyo alikuwa anakusanya malipo kutoka kwa wateja na kuyawasilisha kwa Bw. Baisi huko Illinois ambaye alikuwa anazituma Tanzania na kubakia na nyingine.

Mwaka 2013 na 2014, Bw. Baisi alipokea fedha kama malipo halafu akazituma jiji Dar Es Salaam kama malipo ya alikonunua heroin hiyo. Kwa mujibu wa uchunguzi uliofanywa na Homeland Security ya Marekani kwenye simu mbili za Bw. Baisi Ocktoba 7 mwaka huu baada ya kukamatwa, mtuhumiwa aligundulika kuwa kwenye sehemu ya mtandao wa kimataifa wa biashara ya heroin na money laundering kati ya Tanzania na Marekani.

Kwa mujibu wa ripoti ya Homeland Security, wanachama wa mtandao huo wanaishi sehemu mbalimbali duniani zikiwemo Tanzania, India, kaskazini mwa Illinois and magharibi mwa Michigan. Bw. Baisi anadaiwa kusimamia na kufuatilia kwa njia ya kieletroniki jinsi vifurishi hivyo vilivyokuwa vinasafirishwa kutoke Tanzania hadi Muskegon.

Mamlaka husika zilishtukia biashara hiyo ovu Disemba 2013 baada ya kukamata vifurishi viwili (Express Mail parcels) vilivyokuwa vimetumwa kwa wakazi wawili katika eneo la Muskegon. Kila kifurishi kilikuwa na karibu gramu 150 za heroin iliyokuwa imefichwa ndani ya soli za sandals. Uchunguzi ulidumu kwa miezi kadhaa kabla ya kukamata kifurishi cha tatu chenye heroin July 2014 katika uwanja wa John F. Kennedy Airport jijini New York kilichokuwa kinaenda katika anwani iliyopo magharibi mwa Illinois iliyokuwa na uhusiano na Bw, Baisi.

Baisi alikuwa bado anatumikia kifungo cha nje tokea mwaka 2009 baada ya kufungwa kwa kosa la kujihusisha na biashara ya heroin. Agosti 5 mwaka huu, Polisi walimhoji Baisi nyumbani kwake Illinois. Inadaiwa kuwa katika mahojiano hayo, Bw. Baisi alikiri kujihusisha katika mtandao wa biashara ya madawa ya kulevya na money laundering kati ya Tanzania na Marekani.

Baada ya Bw. Baisi kushirikiana na polisi waliokuwa wanafanya uchunguzi, ikiwa ni pamoja na kuwakabidhi simu zake Augosti 25, polisi walipokea taarifa Septemba 19 kuwa angeweza kuondoka Marekani Septemba 22. Maafisa wa Customs waliidhibitishia polisi kuwa Baisi alikuwa amepanga kuondoka na ndege ya Emirates kutoka Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa O.Hare kwenda Dar Es Salaam, Tanzania, kinyume na makubaliano ya yeye kutumikia kifungi cha nje.

Baada ya kuambiwa hivyo, polisi walipata warrant na kumkamata Septembe 22 kwenye taa za trafiki maeneo ya Mount Prospect wakati akielekea uwanja wa ndege kurudi Tanzania. Oktoba 30, mahakama iliamua kumweka ndani bila bail kusubiri kesi yake. Jaji alisema Baisi ametenda kosa ambalo adhabu yake ni si chini ya miaka 10 jela na kwamba kuna uwezekano kuwa Baisi angeshindwa kutokea mahakamani au kuhatarisha maisha ya mtu mwingine au jamii kama akiachiliwa.

Chanzo: Government: International drug ring smuggled heroin to Muskegon from Tanzania; suspect charged | MLive.com
 
Iwapo viongozi wakuu wa nchi ni wezi wa kutupwa, wananchi wa kawaida watafanya nini?

attachment.php
 
Unajua kuna majitu mengine yanavyoona yanafanya michezo yao michafu kirahisi wakiwa Bongo, basi wanaona kwamba kokote wanaweza tu kufanya bila kudakwa.
Ni vile wanaona wanaenda Mombasa kupokea shehena zao za sembe kisha wanasafirisha kwa gari zao kupitia Tanga na kwenda nazo Magomeni kwenda kufunga mzigo kusafirisha nje huku polisi wote wakikusalimia kwa heshima, basi wanaona kote ni hivyo hivyo.
Yaani watu wengine naona kama wana ubongo wa Mbuni.
Ova
 
Sikio la kufa ndiyo Hili hapa
1. On bail at suspended sentence bado haiingii kichwani unaendeleza kamchezo
Halafu unabook ticket obviously ita-alarm
2. Kwa Us kupeleka vifurushi wakati kuna kila aina ya scanners on parcels
 
Subiri anti-wabeba maboksi brigade waamke.....

Hili siyo swala la Anti-wabeba box Presidaa sidhani kama hata wewe wewe unabariki raia wako kujihusisha na biashara ya dawa za kulevya na inapigwa vita kila mahala.

Mtu yeyote anayechafuwa taswira ya Tanzania si wakuchekewa hata kidogo na nitakupa mfano mdogo sana.

Mwaka 1996 nilikwenda Canada, London Eathrow to Gatwick kwa ajili ya kubadili ndege ilikuwa ni issue ya transint ya kawaida kabisa hata kama ingebidi kulala London na hata kuingia Uingereza Watanzania tulikuwa hatutumii Visa.

Wapemba na CUF yao wakatuharibia UK wote wakiingia wakimbizi wa kisiasa, Nilipokuwa Canada niliona watu wakiingia Marekani kwa urahisi kwa kutumia border ya Canada na US Osama na watu wake wakaharibu Marekani ikafuta viza za border kwa mataifa mengi sana, sasa huyu raia wako unajuwa huu ujinga aliofanya una impact gani kwa nchi yetu?

Kuna viju vinakera sana miaka kama 10 na kitu iliyopita nilikuwa naelekea South Africa kufika border ya Zimbabwe na South Africa upande wa South Beitbrigde border kwenye bus abiria Mtanzania nilikuwa peke yangu wale Polisi waliniweka pembeni nilipigwa sachi mpaka bus likaniacha mpaka msamalia mwema mmoja akanishauri next time kama unakuja South Africa kwa bus ukifika Lusaka panda mabasi yanayomilikiwa na mkaburu wenyewe Greyhound au Translux mkifika border driver anakusanya passport zenu wote na zinagongwa entry mnapita na kama kuna issue ya customs wanakuclear faster nilipatwa na unyanyasaji wote huu kwakuwa jina la Tanzania tayari lilishakuwa chafu kwa biashara ya dawa za kulevya kwa hasira siku ya kurudi nikakata one way ya ndege kutuwa Bongo yaleyale nikawekwa pembeni masaa ndege 3 zinashusha abiria mimi sijatoka arrival kisa kumbe bakari Malima ndio kipindi alikamatwa na Mandrax kutoka Souka South Africa ambako ndiko sokoni.
 
Huyu Baisi si mhaya huyu? Hivi nyie wahaya nini kimewapata siku hizi, mmeingilia deal za wachaga?

Huu ni ushamba kuattack makabila ya watu, first nadeclare mimi siyo muhaya kama Maxence Melo wala siyo mchaga kama Mike Mushi ila ukitaka kulihusisha kabila na michezo ya nyunga basi kama wewe bado mshamba na umekuja mjini juzi hi ni michezo ya watoto wa ukanda wa pwani hasa Dar na Tanga, kama hizo sehemu wenyeji wake ni wahaya na wachaga haya.
 
Nadhani hukunielewa tu.

Ni kwamba, kwa vile jamaa aliyekamatwa ni Mbongo aishiye Marekani basi wale anti-wabeba maboksi brigade wanaweza kuitumia hii habari kama fursa ya kurusha madongo.

Ushakuwepo hapa jamvini kwa muda na nina imani unaelewa jinsi baadhi ya mambo yalivyo kwa baadhi ya watu.

Binafsi sibariki kabisa ushiriki wa yeyote yule katika mambo haramu. Lakini ikija kwenye hawa anti-wabeba maboksi tabia zao zinatabirika kama kucha na kuchwea kwa jua!!
 
Umeguswa nini, mbona povu jingi. Tulia, escrow nyinyi, unga nyinyi pia mna laana?
 
Nimekuelewa vyema ila hao watu hapaswi kuitwa Anti wabeba mabox bali jina lao sahihi ni Viza refusal victim.

Nakuhakikishia 90% ya vijana wa Kitanzania wanaomba usiku na mchana wapate fursa ya kuwa raia wako wapya kwa jinsi huku mavumbini hali ilivyokuwa ngumu.

Asikudanganye mtu mimi kipindi nafunga mkanda kwa mara ya kwanza nafasi za Canada zilitoka 30 lakini tuliostahili tulikuwa 10 tu nafasi zingine zingine viongozi wa wizara waliziuza na nyingine wakubwa wakapachika watoto wao na wengine tulivyofika kule hawakurudi wala hawakuendelea na kazi iliyotupeleka.
 
Umeguswa nini, mbona povu jingi. Tulia, escrow nyinyi, unga nyinyi pia mna laana?

BTW wewe siyo size yangu ninakuignore tu, kama una bifu na wahaya JF Founder Maxcence Melo ni Muhaya hebu elekeza bifu lako kwake.
Cia.
 
Hili siyo swala la Anti-wabeba box Presidaa sidhani kama hata wewe wewe unabariki raia wako kujihusisha na biashara ya dawa za kulevya na inapigwa vita kila mahala.

Mtu yeyote anayechafuwa taswira ya Tanzania si wakuchekewa hata kidogo na nitakupa mfano mdogo sana.

Mwaka 1996 nilikwenda Canada, London Eathrow to Gatwick kwa ajili ya kubadili ndege ilikuwa ni issue ya transint ya kawaida kabisa hata kama ingebidi kulala London na hata kuingia Uingereza Watanzania tulikuwa hatutumii Visa.

Wapemba na CUF yao wakatuharibia UK wote wakiingia wakimbizi wa kisiasa, Nilipokuwa Canada niliona watu wakiingia Marekani kwa urahisi kwa kutumia border ya Canada na US Osama na watu wake wakaharibu Marekani ikafuta viza za border kwa mataifa mengi sana, sasa huyu raia wako unajuwa huu ujinga aliofanya una impact gani kwa nchi yetu?

Kuna viju vinakera sana miaka kama 10 na kitu iliyopita nilikuwa naelekea South Africa kufika border ya Zimbabwe na South Africa upande wa South Beitbrigde border kwenye bus abiria Mtanzania nilikuwa peke yangu wale Polisi waliniweka pembeni nilipigwa sachi mpaka bus likaniacha mpaka msamalia mwema mmoja akanishauri next time kama unakuja South Africa kwa bus ukifika Lusaka panda mabasi yanayomilikiwa na mkaburu wenyewe Greyhound au Translux mkifika border driver anakusanya passport zenu wote na zinagongwa entry mnapita na kama kuna issue ya customs wanakuclear faster nilipatwa na unyanyasaji wote huu kwakuwa jina la Tanzania tayari lilishakuwa chafu kwa biashara ya dawa za kulevya kwa hasira siku ya kurudi nikakata one way ya ndege kutuwa Bongo yaleyale nikawekwa pembeni masaa ndege 3 zinashusha abiria mimi sijatoka arrival kisa kumbe bakari Malima ndio kipindi alikamatwa na Mandrax kutoka Souka South Africa ambako ndiko sokoni.

Mkuu Matola:

Ni umasikini wa nchi na raia ndio unaofanya watanzania watakiwe kuwa na viza za kusafiria. Hata watanzania wakihamua kuwa watii na wasiojishughulisha na biashara ya madawa bado watatakiwa kuwa na viza.

Wataliano wanauza madawa kuliko watanzania na wanadunda bila viza.
 
Mkuu wangu nakushauri unapochangia jambo hakikisha uko well informed au una ufahamu mpana juu ya unachokisema.

Italy iko barani ulaya na pia Italy ni mwanachama wa EU na pia Italy ipo kwenye itifaki ya Sheghen contries/ Sheghen viza.

Hivi unataka kuniambia Malawi ni tajili kuliko Tanzania ambapo mpaka juzi tu walikuwa wanaingia kwa entry Uingereza?

Ok mimi mara ya kwanza nimeingia South Africa kwa Viza na leo hata wewe ukitaka kusafiri leo leo kwenda South Africa unakata ticket unapanda ndege unaondoka je Tanzania imegeuka kuwa nchi tajili?
 
Hili siyo swala la Anti-wabeba box Presidaa sidhani kama hata wewe wewe unabariki raia wako kujihusisha na biashara ya dawa za kulevya na inapigwa vita kila mahala.

Mtu yeyote anayechafuwa taswira ya Tanzania si wakuchekewa hata kidogo na nitakupa mfano mdogo sana.

Mwaka 1996 nilikwenda Canada, London Eathrow to Gatwick kwa ajili ya kubadili ndege ilikuwa ni issue ya transint ya kawaida kabisa hata kama ingebidi kulala London na hata kuingia Uingereza Watanzania tulikuwa hatutumii Visa.

Wapemba na CUF yao wakatuharibia UK wote wakiingia wakimbizi wa kisiasa, Nilipokuwa Canada niliona watu wakiingia Marekani kwa urahisi kwa kutumia border ya Canada na US Osama na watu wake wakaharibu Marekani ikafuta viza za border kwa mataifa mengi sana, sasa huyu raia wako unajuwa huu ujinga aliofanya una impact gani kwa nchi yetu?

Kuna viju vinakera sana miaka kama 10 na kitu iliyopita nilikuwa naelekea South Africa kufika border ya Zimbabwe na South Africa upande wa South Beitbrigde border kwenye bus abiria Mtanzania nilikuwa peke yangu wale Polisi waliniweka pembeni nilipigwa sachi mpaka bus likaniacha mpaka msamalia mwema mmoja akanishauri next time kama unakuja South Africa kwa bus ukifika Lusaka panda mabasi yanayomilikiwa na mkaburu wenyewe Greyhound au Translux mkifika border driver anakusanya passport zenu wote na zinagongwa entry mnapita na kama kuna issue ya customs wanakuclear faster nilipatwa na unyanyasaji wote huu kwakuwa jina la Tanzania tayari lilishakuwa chafu kwa biashara ya dawa za kulevya kwa hasira siku ya kurudi nikakata one way ya ndege kutuwa Bongo yaleyale nikawekwa pembeni masaa ndege 3 zinashusha abiria mimi sijatoka arrival kisa kumbe bakari Malima ndio kipindi alikamatwa na Mandrax kutoka Souka South Africa ambako ndiko sokoni.
Toka hapa na uongo wako kauzu wewe.

Cc: FaizaFoxy Bill Cosby faby Mipangomingi THE BIG SHOW Mshume Kiyate
 
Last edited by a moderator:
Back
Top Bottom