Madawa ya Kulevya Awamu ya III: RC Makonda amkabidhi majina 97 Kamishna Mkuu wa madawa ya kulevya

Ilikuwa lazima Madabida ahudhurie ile windup ya jana! Kwamba, alitengeneza ARV Fake hilo ni jambo moja lakini kuhudhulia shughuli ya kisiasa ni jambo lingine! Tangu mwanzoni watu tulikuwa tunasema kwamba zoezi limejaa viashiria vya siasa ndani yake! Jambo lolote linalohusisha siasa utalijua tu kwa sababu professionalism inakuwa sio hoja ya msingi kwenye suala husika bali publicity!

Jana Madabida amethibitisha kwamba lilikuwa ni suala la kisiasa! Kule background kulikuwa ama na vijana wadogo au audio iliyokuwa inatoa vibwagizo kwa mtindo wa Chipukizi wwa CCM!
Ajabu kuna watu hawakuliona hilo tokea mwanzo.
Hii sio vita ya madawa ya kulevya,ni muendelezo wa siasa chafu za kuchafuana.
Baada ya kumtaja Mbowe (KUB) wengine wamekabidhiwa kwa mkuu wa kitengo kimyakimya.
 
Mheshimiwa Makonda kwa ujasiri aliamua kutangaza vita dhidi ya madawa ya kulevya bila kuogopa wala kumuonea mtu haya.
Huu mjadala wa vita dhidi ya madawa ya kulevya ni mjadala ambao kwa siku nyingi ulikuwepo lakini hakuna mtu aliyejitokeza hadharini na kuanza kupambana nao kwa wazi zaidi kama alivyofanya Mheshimiwa Makonda. Kuna mapungufu RC Makonda aliyafanya katika kuanzisha vita hivi lakini Makonda kama mwanadamu hakosi mapungufu.
Nilisikitika sana kusikia idadi ya watanzania waliopo kwenye majela ya nje kama alivyotoa Rais Magufuli haiwezekani kwa vijana hao waendelee kusota kwenye majela ya huko wakati waliowatuma wapo hapa nchini wakitanua na mali na magari ya kifahali. Faida ya vita hivi ni kwasasa kwa hawa wafanyabiashara wa madawa ya kulevya wameshatumiwa message kwamba serikali iliyopo madarakani imeamua rasmi kupambana nao na vijana wakitanzania hawataongezeka katika majela ya nje.
Nawaomba wabunge wote bila kujali vyama vya siasa waunge mkono vita hivi wala wasiingize itikadi za kisiasa katika vita hivi.
Tanzania bila madawa ya kulevya inawezekana.
 
Ajabu kuna watu hawakuliona hilo tokea mwanzo.
Hii sio vita ya madawa ya kulevya,ni muendelezo wa siasa chafu za kuchafuana.
Baada ya kumtaja Mbowe (KUB) wengine wamekabidhiwa kwa mkuu wa kitengo kimyakimya.
Nashukuru since Day 01 nilipinga approach ya Makonda na drama zake!! Na sasa nafurahi kuona hata wenyewe kumbe wamempinga Makonda in other way round!! Jana nilikuwa namuona alivyokuwa anajichekeshachekesha kwa namna ya kumshawishi Kamishna afanye ujinga kama aliokuwa anafanya yeye...
 
Mapambano ya dawa za kulevya yapo kwenye ILANI ya uchaguzi ya CCM 2015, naye anahitajika kushiriki kutekeleza ilani.

Uwepo wake siku hiyo ni muhimu sana, maana yeye kwa DSM ndiye mwenye chama.
 
Leo siku ya Jumatatu kuanzia saa nne asubuhi Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Mhe Paul Makonda ataongea na waandishi wa habari kutangaza listi ya wauzaji na watumiaji wa madawa ya kulevya kwa mara ya tatu.

Nipo njiani kuelekea ukumbini ntawaletea updates yanayojiri kutoka ukumbini.

========

UPDATES;

========



Waandishi wa habari ambao watakuwa na vitambulisho maalumu ndo wataruhusiwi kuingia ukumbini. Nje ya ukumbi ulinzi umeimarishwa sana baadhi ya waandishi wa habari wameshaanza kuwasili.

Waandishi wa habari kutoka vyombo mbalimbali wapo nje ya ukumbi.

Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda atawasili muda mfupi ujao.

Waandishi wa habari wamebakia nje ya ukumbi
Mkuu wa Mkoa Makonda hajafika ukumbini
Ikifika saa tano Mkuu wa Mkoa hajafika tutaondoka nje ya ukumbi wa Mwl Julius Nyerere kuendelea na majukumu mengine.

Waandishi wa habari tumeshaingia ndani ya ukumbi
Bado tunasubiri Mkuu wa Mkoa Paul Makonda....

Kutoka ukumbini: Waandishi wakimsubiri Mkuu wa Mkoa DSM, Paul Makonda kwa taarifa juu ya vita ya Madawa ya Kulevya.

Maofisa wa Jeshi la Polisi wakiwa ukumbini
Mkuu wa Mkoa Makonda Paulo akiwa ukumbini.
View attachment 470185

=====

Alhadi: Ukiwa kiongozi muadilifu, ukipendwa na mwenyezi Mungu na malaika wake inatosha, ukitaka kupendwa na watu wewe utakuwa zaidi ya Yesu.

Sheikh Alhadi: Mapambano ya dawa za kulevya yanahitaji kumtanguliza Mungu

Sheikh A. Mussa: Tunataka viongozi walio tayari kuchukua maamuzi magumu katika kusimamia haki bila kumwangalia mtu usoni


Alhadi: Tunataka viongozi ambao wako tayari kusimamia haki kama alivyosema mheshimiwa Rais na baraka itamiminika katika nchi yetu.

Askofu: Haki kutendeka si jambo jepesi. Haki ni kuleta amani na utulivu. Mungu ndiye msimamizi wa mambo yote ya haki

"Sisi Viongozi wa dini tunaunga mkono jitihada za Serikali dhidi ya dawa ya kulevya"-Mwakilishi madhehebu ya kikristo

Askofu: Tunawakia hekima viongozi wetu katika maamuzi ya haki, Tunaunga juhudi hizo zinazoendelea katika nchi yetu. KKKT tunaye mchungaji ambae ameanzisha juhudi hizi. Naomba mkuu wa mkoa umshirikishe sana mchungaji huyu.
KAMANDA SIRRO: "Nampongeza Mkuu wa Mkoa, Paul Makonda kwa jitihada juu ya vita hii ya dawa za kulevya..."
Kamanda Sirro: Taarifa ya operesheni tuliyoifanya wiki ya tatu iliyozinduliwa na mkuu wa mkoa Paul Makonda, lengo ni kuwakamata wote wanaojihusisha na biashara hii ya madawa ya kulevya. Mkuu wa mkoa aliunda kamati ya kufanya upelelezi. Watuhumiwa waliokamatwa ni watuhumiwa 311 na vielelezo. Kete 544 za heroin, Mirungi bunda 21.

Kamanda Sirro: Watuhumiwa 117 wamekutwa na vielelezo, 194 hawajakutwa na vielelezo. Watuhumiwa 77 walitakiwa kuja baada ya kutajwa na mkuu wa mkoa. Hadi jana watuhumiwa 32 wameripoti na kuhojiwa, watuhumiwa 45 hawajaripoti na juhudi zinafanyika kuwapata.

Kamanda Sirro: Amabao hawajaripoti watasakwa popote walipo na kupelekwa mahakamani.

Kamanda Sirro: Watuhumiwa wengine upelelezi unaendelea. Pongezi za dhati kwa mkuu wa mkoa kwa ushiriki wake binafsi ya kuongoza mapambano haya. Ukishakuwa mwenyekiti wa kamati ya ulinzi na usalama ni vizuri kwenda kwenye ground uone kazi zinazofanyika.

Kamanda Sirro: Mkuu wa mkoa anaambatana na Askari kwenye operesheni ili kujua ugumu wa kazi inayofanywa.

Kamanda Sirro: Kuna mwanamke amejisalimisha mwenyewe na magunia 5 ya bangi, hivyo tunajua wananchi wamejitolea kutusaidia.

Khalid Salum Mohamed(TID): Nilipotea njia na kuingia katika Janga la Kutumia Dawa za Kulevya. Nakiri niliikosea jamii kwa ujumla.

TID: Nipo mbele yenu kama kijana shupavu, jasiri na mnyama! Inabidi uwe mnyama kama kaka yangu Makonda kufanikisha mapambano haya.

Ramadhani Madabida(CCM Dar): Chama hiki ndo kinatawala na kuongoza nchi hii. Tumeomba ridhaa yenu kuwaongoza kupitia ilani.

Madabida(CCM): Ktk Ilani yetu ya Uchaguzi mwaka 2015, ukurasa wa 197 tuliahidi kupambana na matumizi ya Dawa za Kulevya.

Madabida(CCM): Niko hapa kushuhudia kama tuliyoahidi ktk Ilani yanatekelezwa! Tunatakiwa kuiunga mkono Serikali katika mapambano haya.

RC Makonda: Vita hii inakupunguzia idadi ya marafiki, inatia hofu kwako na waliokuzunguka. Si vita ndogo! Rais ana dhamira ya dhati.

RC Makonda: Kuna wanaopiga kelele... Wengine ni wanufaika, kuna waliopata kura na fedha za kampeni kupitia Wauzaji wa Dawa za Kulevya.

RC Makonda: Wapo pia wanaopiga makelele mitandaoni na mitaani kwakuwa hawajui maana ya vita hii au wanafikiria kisiasa.

RC Makonda: Leo ninayo majina mengine 97. Wapo wanaotaka kuhakikisha tunapotea njia; shida yetu ni kuondoa Dawa za Kulevya Dar, basi.

Makonda: Sheria iko wazi. Mtumiaji wa Dawa za Kulevya ni JELA miaka 3. Tatizo watu hawajaisoma sheria hiyo.

RC Makonda: Wengine wanaotumia Dawa za Kulevya wamejikuta wakishiriki mapenzi ya jinsia moja. Kinyume kabisa na misingi ya utu.

RC Makonda: Watanzania takribani 296 wameshakamatea South Africa wakihusishwa na Madawa ya Kulevya.

RC Makonda: Kwa sasa wauzaji wa Dawa za Kulevya wanatumia Mitungi ya Gesi. Hapa Dar zipo takribani bandari bubu 50.

RC Makonda: Leo usiku mtausikia moto utakaowaka ktk viunga vya jiji la Dar. Zipo nyumba takribani 200, nyingine za wanasiasa.

RC Makonda: Kuna Club takribani 20 ambazo zinatumiwa kuuza #MadawayaKulevya jijini Dar. Vipo vijiwe 107 vinavyofanya hivyo.

RC Makonda: Jijini Dar wapo kina mama wanauza vitumbua na ni wauzaji wakubwa wa #MadawayaKulevya.

RC Makonda: Kuna "Bureau de Change" zinazotakatisha fedha za Wauzaji wa Dawa za Kulevya. Wanafanya hivyo kwa kutumia USD.

RC Makonda: Jijini Dar zipo "Bureau de Change" nyingi sana na nyingine zinafanya miamala ya hadi $3,000,000 kwa siku!

RC Makonda: Umri wangu unaniruhusu kujaribu kila kitu! Usilete mbwembwe kwenye utawala huu. Ukiitwa Polisi nenda, acha mbwembwe.

RC Makonda: Kuna wanaofanya biashara hizi si rahisi kuwakamata! Wanaficha sana njia wanazotumia ila wote tumeshawabaini.

RC Makonda: Mtikisiko utakaotokana na Daraja la 3 litapandisha joto. Linahusisha uongozi wa Awamu ya Tatu! Linahusisha makundi mengi.

RC Makonda: Tunapomwita mtu ktk kadhia hii ya #DawaZaKulevya basi ujue tunakufahamu kwa takribani miaka 10 iliyopita! Ujumbe umefika.

Traffic hajawahi hata siku moja kunisamehe. Hamna taasisi yeyote ya serikali ambayo imenipa msamaha kwa kuvurunda. Huu ni utawala wa sherii na kama amevunja sheria basi aadhibiwe. Rais alisema hamna mtu juu ya sheria.

Naomba tuachie sheria ifuate mkondo wake kwa wanaojishughulisha na madawa ya kulevya na rc pia. Mama Ana Kilango hakusamehewa kwa kosa ambalo ukilinganisha na hili ni cha mtoto. Naomba pia shutuma dhidi yake zifanyiwe kazi.
 
Mapambano ya dawa za kulevya yapo kwenye ILANI ya uchaguzi ya CCM 2015, naye anahitajika kushiriki kutekeleza ilani.

Uwepo wake siku hiyo ni muhimu sana, maana yeye kwa DSM ndiye mwenye chama.

Ilani inasema hivyo lakini dhamira ya viongozi wa ccm ni tofauti kwani ndio sababu kuu biashara hiyo imeshamiri
 
Mapambano ya dawa za kulevya yapo kwenye ILANI ya uchaguzi ya CCM 2015, naye anahitajika kushiriki kutekeleza ilani.

Uwepo wake siku hiyo ni muhimu sana, maana yeye kwa DSM ndiye mwenye chama.
Wachapisha tisheti zile korigo kutoka china zile zinazogawiwa bure kwa maskini wa akili wale wengi ndio wafadhili wa ccm na ndio wauza madawa ya kulevya,ccm bila rushwa,polisi na Nec,ccm haipo
 
Jana nilimuona mzee madabida aakiongea wakati mkuu wa mkoa alipoita waandishi wa habari kuongea kuhusu madawa ya kulevya,huyu mzee aliongea meeeengi na jinsi CCM inavyopambana ili kutokomeza madawa haya yanayoangamiza nguvu kazi ya taifa.
Swali likanijia hivi huyu si ndo mtu alokuwa anatengeneza ARV feki na watu wengi walikufa kwa sababu ya kuzitumia?hivi CCM hawaoni kuwa ARV Feki ni bomu lingine lililoangamiza watanzania.?hivi madabida alipata wapi moral authority ya kukemea uovu huu wa madawa wakati yeye aliweka ma rehani ya watu wetu wengi kwa ARV zile feki?
Mmmmh hapa napita tu sichangii kitu maana pesa ya kujidhamini katika uchochezi sina
 
Iiwa Mheshimiwa kakabidi orodha ya Majina 97 ya awamu ya tatu.. je ndio mwisho wake wa kupambana na madawa ya kulevya....

Tazama Neno OMEGA Kisha tutafakari kwa pamoja
c0d0bf6d4698f44168ff982c729f69da.jpg
 
Umeambiwa yeye na kamanda Sirro wanaawamu saba, na jana ni awamu ya tatu tu, bado anaendelea ila akipata majina akakabidhi kwa kamishna
 
Umeambiwa yeye na kamanda Sirro wanaawamu saba, na jana ni awamu ya tatu tu, bado anaendelea ila akipata majina akakabidhi kwa kamishna

Hayo maneno ya kwenye kanga tu. Magufuli keshaonyesha kwamba hiyo ni kazi ya tume. Huyu bwana misifa aliingilia kazi isiyo yake.
Dar imefanya vibaya mitihani ya fom foo. Ajibu kwanza hilo.
 
Iiwa Mheshimiwa kakabidi orodha ya Majina 97 ya awamu ya tatu.. je ndio mwisho wake wa kupambana na madawa ya kulevya....

Tazama Neno OMEGA Kisha tutafakari kwa pamoja
c0d0bf6d4698f44168ff982c729f69da.jpg
OMEGA ni jina la kampuni ya kutengeneza mafile
 
Ili vita hii ya kupigana na madawa ya kulevya ifanikiwe haipaswi kuligea taifa hofu watu wakashindwa kufanya kazi zao nyingine. Vita hii ilenge kuzitokomeza dawa zote za kulevya ndani ya mipaka ya nchi yetu leo sio jana. Nadhani sio sawa kutafuta miaka 5 au 30 iliyopita hali ilikuwaje, kufanya hivyo ni sawa na kufukua makaburi hasa katika kipindi hicho pia kulikuwa na uongozi halali ambao ulipaswa kuyafanya hayo. Nadhani nguvu kubwa tuielekeze kwenye kupambana na wauza na waleta madawa hayo sio watumiaji. Kwani baadhi ya watumiaji ni ama walikuwa watoto walioshawishiwa amma walikuwa watoto wakati wanaanza kuyatumia..
 
Back
Top Bottom