Madawa feki madukani, NANI ATANISAIDIA MIMI MKULIMA?? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Madawa feki madukani, NANI ATANISAIDIA MIMI MKULIMA??

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by fikirikwanza, Jun 25, 2012.

 1. f

  fikirikwanza JF-Expert Member

  #1
  Jun 25, 2012
  Joined: Jan 25, 2012
  Messages: 5,935
  Likes Received: 13
  Trophy Points: 135
  Ninaumwa, naenda kupimwa kumbe darubini ni mbivu siku nyingi, aandikiwa dawa kimungumungu tu; naangalia fedha niliyonayo, naomba mjukuu wangu aniongezee japo kwa mpesa, ananitumia baada ya kulalamika kuwa mshahara huko town haumtoshi kuendesha maisha, naingia dukani nanunua dawa kumbe expired, anajikusanya tena nanunua dawa kumbe feki, kwenye paketi mpya inayoonekana halisi.

  Ugonjwa unazidi, naona kifo kinanikaribia, dawa za wazungu siponi kumbe feki+expired, naona heli kibinadamu nijaribu kwa sangoma, mambo yanakuwa makubwa zaidi, kupona siponi na uhasama mkubwa unaanzishwa, siongei na jirani kisa ameniloga, siongei na ndugu na jamaa kisa wanahusika na ugonjwa wangu; vitisho, kukatana mapanga, na mengineyo vinafuatia.

  Je nani atanisaidia na hali hii ngumu kuishi?? TFDA wanajua kuna madawa feki na expired yanauzwa mjini na vjjijini??/ je nalipwa mishahara kufanya nini??? nani alaumiwe kwa huu mgogoro wa maisha has vijijini juu ya matibabu feki , uchawi na mauaji ya wachawi waliothibitika???

  Je CCM hata hili la dawa feki limewashinda?? tumeweza nini kama CCM, udhaifu na upuuzi huu mpaka lini? Je CDM itatusaidia kuondoa dawa feki madukani?? nani atanisaidia???
   
 2. f

  fikirikwanza JF-Expert Member

  #2
  Apr 13, 2015
  Joined: Jan 25, 2012
  Messages: 5,935
  Likes Received: 13
  Trophy Points: 135
  Hii bado naikumbuka sana
   
Loading...