Madarasa kujengwa ndani ya mwezi mmoja inawezekana au ndo siasa?

Sanyambila

JF-Expert Member
Jan 24, 2018
339
457
Wadau habari za majukumu
Napenda nianze kwa kumpongeza Rais wetu Samia kwa kuona changamoto ya upungufu wa madarasa nchini

Na ndiyo maana alipo pata pesa za IMF Kupambana na COVID-19 akazipeleka mashuleni kila wilaya kujenga madarasa mapya sasa maagizo ndo tatizo.

Madarasa hayo yameamuriwa kujengwa ndani ya mwezi mmoja yawe yameisha je! Wamezingatia ubora au yapo kisiasa ili baada ya miaka mitano yawe yamechakaa ? Kwanini wasingetoa muda mzuri walau miezi sita ili yawe imara?
Kwa sasa sehemu nyingi walimu hawafundishi wapo bize na mradi huku viongozi wa kisiasa na wataalamu wakitoa maagizo yanayokinzana .

Huyu nunua Batu gauge 28 huyu akija nunua msauzzi, huyu wekeni marumaru huyu weka sakafu ya cement, huyu vile huyu hivi

Wadau nini kifanyike ili miradi iwe madhubuti?

FB_IMG_1639065010500.jpg
 
Inategemea na aina ya jengo. Kwa jengo la chini tena kwa aina ya madarasa yetu inawezekana. Chamsingi kanuni za ujenzi zifuatwe.
 
Madarasa yajemgwe miezi sita, ni madarasa ya ghorofa au?

Kwenye swala la ujenzi mchawi pesa, maana kila kitu kipo kwa wakati.
 
Back
Top Bottom