Madaraka ya rais ndani ya rasimu ya katiba mpya yameporwa bila sababu za msingi


K

Kitorondo

Member
Joined
Oct 21, 2011
Messages
59
Likes
10
Points
15
K

Kitorondo

Member
Joined Oct 21, 2011
59 10 15
Mihimili mitatu ya dola inaingiliana katika rasimu ya katiba mpya.mfano Rais kuondolewa uwezo wa kufanya uteuzi wa watu anaoona wanafaa na badala yake yeye kupokea mapendekezo ni kumnyang'anya mamlaka yake.watu anaowateua kuthibitishwa na muhimili mwingine wa dola -Bunge ni kuvuruga dhana ya separation of power.Rais amewekwa na watanzania kwa niaba yao hivyo hatuna budi kumwamini kwa kile anahotenda kwa niaba ya ananchi
 
Z

zamlock

JF-Expert Member
Joined
Dec 25, 2010
Messages
3,846
Likes
57
Points
145
Z

zamlock

JF-Expert Member
Joined Dec 25, 2010
3,846 57 145
mbona kenya wanafanya hivyo hivyo na sehemu nyingi duniani ni hivyo
 
Kamakabuzi

Kamakabuzi

JF-Expert Member
Joined
Dec 3, 2007
Messages
1,534
Likes
98
Points
145
Kamakabuzi

Kamakabuzi

JF-Expert Member
Joined Dec 3, 2007
1,534 98 145
Ndugu Kitorondo bado Rais amepewa madaraka mengi ambayo si vizuri kuwa nayo. Kwanza nianze na hoja yako ya kuwa rais amechaguliwa na watanzania, je hao wabunge wamechaguliwa na nani. Mihimili him iwili inachaguliwa na watanzania moja kwa moja kwa kura; sualani namna ya kuupata muhimili wa tatu (mahakama) na tuupate katika namna ambayo haitaathiri uhuru wake.Hapa nido linakuja suala la muhimili mmoja kufanya uteuzi na mwingine kuthibitisha uteuzi; hii inasaidia kuufanya huo muhimili wa tatu ujione kuwa hauegemei upande wowote wa mihimili mingine miwili.Hoja yangu kuwa bado rais ameachwa na madaraka makubwa yapo kwenye namna ya kuupata huo muhimili wa tatu - makahama Angalia nani anamyeua mkuu wa mahakama (ni rais), nani anampemdekeza (ni tume ya utumishi ya makahama ambayo kwa asilimia zaidi ya 70 inateuliwa na rais) Angalia madaraka aliyopewa ya kutengua vifungu vya katiba, kama kifungu cha uzoefu katika kuwateua majaji - wakati katiba imeweka muda wa miaka kumi, bado rais amepewa madaraka ya kuweza kukikiuka kifungu hicho kwa kushauriana na tume ya utumishi awa mahakama ambayo anaiteua mwenyewe.Mchanganuo wa vifungu husika ni ufuatao:Kuna mahakama 2, mahakama ya juu na mahakama ya rufani:146.-(1) Bila ya kuathiri masharti yoyote yaliyotangulia katikaSehemu hii, kutakuwa na Muundo wa Mahakama katika Jamhuri yaMuungano utakaokuwa kama ifuatavyo:(a) Mahakama ya Juu; na(b) Mahakama ya Rufani.147.-(1)Kutakuwa na Mahakama ya Juu ya Jamhuri yaMuungano au kwa kifupi itaitwa “Mahakama ya Juu” ambayo itakuwana:(a) Jaji Mkuu ambaye atakuwa Rais wa Mahakama ya Juu;(b) Naibu Jaji Mkuu ambaye atakuwa Makamu wa Rais waMahakama ya Juu; na(c) Majaji wengine wa Mahakama ya Juu wasiopungua saba.Uteuzi wa jaji mkuu uko hivi:151.-(1) Jaji Mkuu atateuliwa na Rais kutoka miongoni mwamajina ya watu watatu yaliyopendekezwa na Tume ya Utumishi waMahakama na kabla ya kuapishwa jina lake litawasilishwa Bungeni kwaajili ya kuthibitishwa na Bunge.(2) Jaji Mkuu ndiye atakuwa Mkuu wa Mhimili wa Mahakamakatika Jamhuri ya Muungano.Uteuzi wa naibu Jaji mkuu uko hivi:152.-(1) Naibu Jaji Mkuu atateuliwa na Rais kutoka miongonimwa majina ya watu watatu yatakayopendekezwa na Tume ya Utumishiwa Mahakama na kabla ya kuapishwa jina lake litawasilishwa Bungenikwa ajili ya kuthibitishwa na Bunge.Uteuzi wa majaji wengine saba wa kuunda Mahakama ya juu uko hivi:153.-(1) Majaji wa Mahakama ya Juu watateuliwa na Rais kutokamiongoni mwa majina yatakayopendekezwa na Tume ya Utumishi waMahakama na wataapishwa na Rais.Uteuzi wa mwenyekiti wa mahakama ya rufani, na majaji wa mahakama hiyo unafuata mlolongo huohuo rejea vifungu vya 162 na 163Hiyo Tume ya utumishi wa mahakama inaundwa ifuatavyo:172.-(1) Kutakuwa na Tume ya Utumishi wa Mahakama ambayoitaundwa na wajumbe tisa watakaoteuliwa na Rais kama ifutavyo:(a) Jaji Mkuu ambaye atakuwa ni Mwenyekiti;(b) Mwanasheria Mkuu wa Serikali ya Jamhuri ya Muungano;(c) Jaji mmoja wa Mahakama ya Juu;(d) Jaji mmoja wa Mahakama ya Rufani;(e) Mwakilishi wa Chama cha Wanasheria wa Tanzania Bara;(f) Mwakilishi wa Chama cha Wanasheria wa Zanzibar;(g) Wakuu Wawili wa vitivo vya sheria kutoka vyuo vikuu, mmojakutoka Tanzania Bara na moja kutoka Zanzibarwatakaopendekezwa na Jaji Mkuu; na(h) Mtendaji Mkuu wa Mahakama ambaye atakuwa Katibu waTume ya Utumishi wa Mahakama.Wajumbe a,b.c.d, na h ni wateule wa Rais; yaani watano kati ya tisa, bado hata hao wa namba g watapendekezwa na jaji mkuu ambaye ni mteule wa Rais!Na kitu kingine ni kuwa Rais anaweza kutengua masharti ya katiba yanayohusu uteuzi wa watu wa muhimili huu, hasa sharti la muda (uzoefu), Kifingu cha 153 “……na amekuwa na sifa hizo mfululizo kwa muda usiopungua miaka kumi.basi Rais anaweza kutengua sharti la kuwa na sifa kwa muda usiopunguamiaka kumi, na baada ya kushauriana na Tume ya Utumishi waMahakama, kumteua mtu huyo kuwa Jaji wa Mahakama ya Juu.”Hapa Rais anapewa uwezo wa kutengua masharti ya katiba. Hii inaacha nafasi ya Rais kumteua mtu kuwa Jaji wa mahakama ya juu au ya rufani ambaye hana uzoefu kwa kushauriana na tume ya utumishi ambayo ameiteua yeye mwenyewe! Kwa kuruhusu kipengele hiki, Rais anapewa uwezo wa kutengua masharti ya katiba. Kumbuka hii ni katiba ya wananchi wote lakini Rais anapewa uwezo wa kutengua uamuzi wa wananchiNAPENDEKEZA HII TUME YA UTUMISHI WA MAHAKAMA IWE HURU NA RAIS ASIPEWE NAFASI YA KUTENGUA MASHARTI YA KATIBA. Kama ni lazima kutengua masharti basi wa kumruhusu kufanya hivyo si tume aliyoichagua mwenyewe bali Bunge ambalo limechaguliwa na wananchi kwa madhumuni ya kurekebisha katiba kwani katiba ni ya wananchi.Ukitaka maoni yangu zaidi tembelea thread hii hapa: https://www.jamiiforums.com/katiba-mpya/464510-rasimu-ina-matatizo-mengi-yarekebishwe-haraka.html
 

Forum statistics

Threads 1,272,335
Members 489,924
Posts 30,448,060