Madaraka Nyerere ataka JK awe na Msimamo; anautaka Urais? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Madaraka Nyerere ataka JK awe na Msimamo; anautaka Urais?

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by BAK, Sep 17, 2009.

 1. BAK

  BAK JF-Expert Member

  #1
  Sep 17, 2009
  Joined: Feb 11, 2007
  Messages: 70,412
  Likes Received: 81,450
  Trophy Points: 280
  Date::9/17/2009Mtoto wa Nyerere ashauri Kikwete aache kutoa muda wa mafisadi kupumuaNa Ramadhan Semtawa
  Mwananchi  MADARAKA Nyerere, mtoto wa kiume wa Baba wa Taifa, Hayati Julius Nyerere, ameonya kuwa kama uongozi wa juu wa nchi hautakuwa na msimamo, vita dhidi ya ufisadi haitakwisha na hali ya umasikini itazidi kuwa mbaya kwa Watanzania wengi.

  Onyo hilo la mtoto huyo wa rais wa serikali ya awamu ya kwanza, limetolewa katika kipindi ambacho taifa liko kwenye maandalizi ya kuadhimisha miaka kumi ya kifo cha muasisi huyo wa taifa itakayokuwa Oktoba 14.

  Mwalimu Nyerere alifariki Oktoba 14, 1999 akiwa Hospitali ya Mtakatifu Thomas nchini Uingereza ambako alikuwa amelazwa.

  Akizungumza jijini Dar es Salaam jana katika mahojiano maalumu na gazeti hili, Madaraka ambaye hupenda kuzungumza kwa upole na umakini, aliweka bayana kwamba, kiongozi wa juu wa nchi, lazima awe na msimamo na ajipambanue kwa marafiki zake wa karibu ili wasimchezee.

  “Kwanza, kabisa ingawa watu wanasema hivi na vile, lakini jambo la msingi kiongozi wa juu wa awe na msimamo, ” alisema Madaraka.

  “Mwalimu (Nyerere), alikuwa akifanya mambo ambayo wengine walikuwa wakikataa, lakini alikuwa ana maamuzi yake kichwani kama kiongozi ambayo alikuwa akiyasisimamia. Hili ni jambo la lazima.”

  Alifafanua kwamba katika vita ya ufisadi kumekuwa na siasa zaidi kuliko vitendo na kwamba ushahidi unaangaliwa kwa mtazamo wa kimahakama zaidi kuliko wa kimazingira.

  Madaraka alisema wakati wa Mwalimu Nyerere, mtu akishukiwa kwamba ni mlarushwa, jambo la kwanza kama ni kiongozi wa serikali lilikuwa ni kung’olewa katika wadhifa wake.

  “Mwalimu... akipata taarifa kwamba, unahusishwa na harufu ya rushwa, jambo la kwanza anakung’oa au anakutaka ujiuzulu na kukwambia wewe utatuharibia serikali,” alisisitiza.

  Madaraka aliongeza kwamba jambo la pili ambalo lilikuwa likifanywa ni mtuhumiwa wa rushwa kuchunguzwa akiwa nje ya kazi na kufikishwa mahakamani.

  “Kwa hiyo, jambo la kwanza kiongozi wa juu wa nchi anapaswa kutumia mamlaka ya kuteua na pia katika kumng’oa mtu ambaye hafai bila kuangalia ni rafiki au la,” alisisitiza.

  Tayari Rais Kikwete ameshaeleza bayana kuwa katika vita hiyo hana rafiki wala ndugu baada ya kuwepo lawama nyingi kuwa serikali inashindwa kuwashughulikia baadhi ya watuhumiwa kwa kuwa ni marafiki zake wa karibu.

  Kikwete pia alisema kuwa mafisadi ni wajanja sana na hivyo inakuwa ni vigumu kuwagundua na kuwafikisha mahakamani.

  Lakini Madaraka alisema wakati mwingine ushahidi wa kimahakama ni mgumu zaidi kuliko wa kimazingira.

  “Mfano leo hii wewe ndugu tulikuwa wote, (anamtaja rafiki yake) tumekuja Maelezo (Idara ya Habari) kuitisha mkutano bila kutoa hata soda, halafu kesho na keshokutwa uwe na gari kama (Range Rover) Vogue, katika mazingira hayo lazima uchunguzwe,” alisisitiza.

  Madaraka alionya kuwa hali ya kutodhibiti ipasavyo mafisadi imesababisha kuongezeka kwa pengo kubwa la masikini na matajiri wachache.

  Makongoro aliweka bayana akisema: “Siku hizi kuna kakundi kadogo (alitumia kidole kusisitiza udogo wake kwa mwisho wa kucha), ambako kana pesa nyingi kweli wakati Watanzania walio wengi ni masikini wa kutupa.

  “Kuna mtu leo hii anaweza kuja na kukuomba Sh1,500 ya kula chakula ukashangaa... hali ni mbaya huku, lakini wengine wana utajiri wa kutisha.”

  Alipoulizwa mtazamo wake kuhusu uongozi wa serikali ya awamu ya nne katika kupambana na ufisadi, alijibu: “Bado safari ni ndefu sana.”

  Madaraka alisema ingawa serikali imekuwa ikichukua hatua, lakini hali bado ni mbaya kwani hakuna sababu kwa nchi kama Tanzania kuwa na umasikini wa kutisha wakati ina utajiri mkubwa.

  Madaraka alisema wakati wa utawala wa baba yake, kulikuwa na uzalendo wa hali ya juu ambao alisema ulitokana na Watanzania karibu wote kuwa sawa na kukosekana matabaka.

  “Wananchi hawakuwa na pesa kweli na viongozi wa juu nao hawakuwa na utajiri; watu walikuwa sawa. Lakini leo hii kuna kakundi kadogo kana utajiri halafu kundi kubwa liko katika umasikini wa kutisha hii ni mbaya,” alisema.

  Kuhusu nia ya Rais Kikwete kuweka sheria ya kuzuia wafanyabiashara kushiriki katika siasa, Madaraka alisema: “Kama ni suala la kutenganisha siasa na biashara, unasema tu hatutaki.
  “Sasa hivi haya mambo ya kuruhusu siasa na biashara ndiyo tunasikia mara kampuni hii ya fulani, kiongozi gani sijui.” Alisema uamuzi wa kutenganisha siasa na biashara ulikuwa msingi mkuu wa Azimio la Arusha la mwaka 1967, kabla ya kuvunjwa mwaka 1990 na kuundwa Azimio la Zanzibar ambalo liliruhusu wanasiasa kufanya biashara.
   
  Last edited by a moderator: Sep 19, 2009
 2. Field Marshall ES

  Field Marshall ES JF-Expert Member

  #2
  Sep 18, 2009
  Joined: Apr 27, 2006
  Messages: 12,659
  Likes Received: 67
  Trophy Points: 0
  - Eti hao viongozi waliong'olewa kwa rushwa na ufisadi under Mwalimu na kufikishwa kwenye sheria, ni kina nani hao mnaweza kuwataja kwa majina tuwajue? Maana mimi nilidhani mambo ya kulindana yalianzia na Mwalimu na sisi sasa tunaiga tu, au?

  Respect.

  FMEs!
   
 3. LazyDog

  LazyDog JF-Expert Member

  #3
  Sep 18, 2009
  Joined: Apr 10, 2008
  Messages: 2,478
  Likes Received: 13
  Trophy Points: 135

  Moja ya misemo nisiyoipenda.
  Very superficial!
   
 4. MziziMkavu

  MziziMkavu JF-Expert Member

  #4
  Sep 19, 2009
  Joined: Feb 3, 2009
  Messages: 39,607
  Likes Received: 4,600
  Trophy Points: 280
  na Hellen Ngoromera


  MTOTO wa Baba wa Taifa, hayati Mwalimu Julius Nyerere, Godfrey Madaraka Nyerere, amesema atajitosa kuwania uongozi wa nchi endapo ataona mambo hayaendi vizuri, na kama watajitokeza watu wasio na sifa kuliongoza taifa.
  Madaraka ambaye ni mtoto wa sita kati ya saba wa Baba wa Taifa, alitoa kauli hiyo jana jijini Dar es Salaam alipoulizwa swali na mmoja wa wanahabari, kama ana nia ya kuwania uongozi, hasa katika kipindi hiki cha kuelekea Uchaguzi Mkuu, unaotarajiwa kufanyika mwakani na wa mwaka 2015.
  Mtoto huyo wa Baba wa Taifa, alikuwa akizungumza na waandishi wa habari kuhusu azma yake ya kutaka kupanda Mlima Kilimanjaro, akiambatana na mtoto wa aliyekuwa Rais wa Uganda, hayati Iddi Amini, aitwaye Jaffar Amin.
  Bila kutaja nafasi ya uongozi anayokusudia, Madaraka alisema zamani alipokuwa anaulizwa swali kama hilo, jibu lake huwa hapana, lakini wakati huu hujibu kuwa atagombea iwapo ataona mambo yanaenda mrama na kama watajitokeza wagombea wababaishaji na wasio na sifa.
  “Zamani mtu akiniuliza swali kama nitawania uongozi, nilikuwa namjibu kuwa sina nia kabisa ya kuwania uongozi, lakini hivi sasa mtu akiniuliza swali hilo nitamjibu hivi, itategemea na mazingira yaliyopo, mfano ikiwa katika eneo ninaloishi nitaona watu ninaowafahamu kwamba hawana uwezo wa kuongoza wanajitokeza kuwania uongozi, nitashawishika kujitosa kwa sababu naamini kuwa nitaweza.
  “Hata wewe ukiwa katika eneo lako, ukiona mambo hayaendi vizuri na uwezo wa kuongoza unao, utafanya nini? Basi na mimi hilo ndilo jibu langu,” alisema Madaraka.
  Akizungumzia kuhusu azma yake ya kupanda Mlima Kilimanjaro akishirikiana na Jaffar Amin, Madaraka alisema wanatarajia kutumia siku nane kukamilisha zoezi hilo la kupanda mlima huo, ambalo litaanza Oktoba 29 hadi Novemba 6.
  “Mimi kwa kushirikiana na Jaffar tutapanda Mlima Kilimanjaro kwa siku nane, lengo la kufanya hivyo ni kuchangisha fedha kwa ajili ya watoto yatima wa Kituo cha Community Alive, kilichopo Musoma. Jaffar aliamua kuungana na mimi katika zoezi hilo kwa kuwa nilimweleza nia hiyo Aprili, mwaka huu alipokuja Butiama, naye alikubaliana nami na kuamua kuniunga mkono,” alisema Madaraka.
  Alibainisha kuwa, dhumuni lingine la kupanda mlima huo ni kuadhimisha miaka 10 ya kifo cha Mwalimu Nyerere ambaye alifariki Oktoba 14 mwaka 1999.
  “Nimeona nitumie siku hizo kumuenzi Baba wa Taifa kwani katika maadhimisho mengi, tumekuwa tukikaa sehemu na kukutana kwa kumbukumbu, kisha kila mmoja kuondoka, lakini kupanda kwangu mlima ule ni ishara ya kumuenzi Baba wa Taifa,” alisema Madaraka.
  Alisema Jaffar anatarajiwa kuwasili nchini Oktoba 25, kisha kukaa jijini Dar es Salaam kwa siku mbili, kabla ya kuelekea mkoani Kilimanjaro kupanda mlima huo.
  Alipoulizwa nani atakuwa mgeni rasmi katika tukio hilo la kupanda Mlima Kilimanjaro kwa watoto hao wa maraisa wa zamani, alisema shughuli hiyo haitakuwa rasmi, hivyo hakutakuwa na mgeni rasmi.
  Alibainisha kuwa, kilichomsukuma kutaka kupanda mlima huo mwaka huu ni kuweka kumbukumbu ili aweze kuwaonyesha watoto wake kabla theluji ya Mlima Kilimanjaro haijaisha, kwani aliwahi kuwasikia wataalamu wakisema baada ya miaka 20, theluji ya mlima huo itakuwa imekwisha.
  “Mwaka jana nilipanda mlima huo, lakini sikufika kileleni, lengo la kufanya hivyo lilikuwa kuchangisha fedha za kujengea mabweni katika Shule ya Sekondari ya Wasichana ya Chief Edward Wanzagi, iliyopo mkoani Mara na tulifanikiwa kukusanya zaidi ya sh milioni 20.
  “Mwaka huu nikifanikiwa kufika kileleni, nitakuwa nikifanya zoezi hilo kila mwaka kwa kuhamasisha masuala tofauti. Mwaka jana nilipanda mlima huo ili kuchangia shule na mwaka huu ni yatima, hakuna lengo katika kuchangia jambo hili, hivyo naomba wadau wajitokeze kuniunga mkono,” alisema Madaraka.
  Alipoulizwa kama suala hilo halihusiana na masuala ya kisiasa na kwa nini asirasimishe, Madaraka alisema hawezi kurasimisha shughuli hiyo kabla hajatafakari kwanza.
  “Suala hili halihusiani na masuala ya kisiasa na sitaki kulirasimisha kwani nikifanya hivyo itabidi kuunda chombo fulani, halafu mwisho wa siku nia ya jambo lenyewe itapotea.
  “Kwa sasa nina hofu ya kuanzisha chombo kwa sababu, unaweza kuondoa azma ya kitu ulicholenga, nahitaji kufikiria kwanza kabla sijarasimisha suala hili,” alisema Madaraka.
  Pamoja na mambo mengine, mtoto huyo wa Nyerere alisema kwa sasa anaishi Butiama na lengo lake ni kuunda chombo cha kukuza na kuendeleza utalii katika Kanda ya Ziwa.
  http://www.freemedia.co.tz/daima/habari.php?id=8707
   
 5. S

  Son of Alaska JF-Expert Member

  #5
  Sep 19, 2009
  Joined: Jun 2, 2008
  Messages: 2,813
  Likes Received: 102
  Trophy Points: 0
  catch him in his blog,BUTIAMA AND BEYOND.jamaa ana sense of humour kali sana
   
 6. K

  Kinyikani Member

  #6
  Sep 19, 2009
  Joined: Dec 5, 2006
  Messages: 65
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 0
  yeye mwenyewe ni fisadi usidanganye watu wewe.
   
 7. Next Level

  Next Level JF-Expert Member

  #7
  Sep 19, 2009
  Joined: Nov 17, 2008
  Messages: 3,159
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 135
  Tunabahati mbaya.....we can't get another ''JK Nyerere''
   
 8. M

  Mwanaluguma Member

  #8
  Sep 19, 2009
  Joined: Aug 23, 2008
  Messages: 64
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0  Anzisha taasisi ufanikishe vizuri shughuli hiza,usipuuzie ushauri huo muhimu wa bure.Ya urais mmmmmmm!!!!
   
 9. S

  S.M.P2503 JF-Expert Member

  #9
  Sep 19, 2009
  Joined: Nov 25, 2008
  Messages: 463
  Likes Received: 21
  Trophy Points: 35
  Anaonekana kuwa presidential material ingawaje bado anasuasua... sijui anamwogopa nani, JK au CCM?

  Kama anataka kuikomboa nchi kwa stairi ya kinyerere basi hana budi kuyavulia maji nguo... najua anajua kwamba Nchi haiendeshwi vizuri ndo maana alisema kuna kakundi kadogo ni katajili kupindukia na kengine maskini wa kutupwa...

  Chonde-chonde madaraka, TANGAZA nia yako mapema ujulikane maana ukiwa na nia, penye njia utapaona tu.. acha kuuma na kupuliza... Njoo uwakomboe watanzania kwa fikra za baba yako... Moderator tafadhali mfikishie ujumbe huu...
   
 10. jmushi1

  jmushi1 JF-Expert Member

  #10
  Sep 19, 2009
  Joined: Nov 2, 2007
  Messages: 17,550
  Likes Received: 1,895
  Trophy Points: 280
  Mkuu hapo pa moderator umeniacha sina mbavu hapa.
  Kuna mtu mwenye hizo link za hizo blogs zenye interviews zake?
   
Loading...