Madaraka ni kileo ukiyatumia vibaya yanalevya

Lord OSAGYEFO

JF-Expert Member
Feb 19, 2021
1,369
2,000
Hakika Viongozi wetu Madaraka mliyonayo ni kama Kileo mnapozidisha lazima milele hebu yatumieni kwa kiasi.Mlio wengi Mmeapa kwa kutumia VITABU VITAKATIFU na Kumtaja MUNGU kuwa AWASAIDIE inakuwaje Mnatesa Watu?

Mnaua, Mnapora mali na Wake au Waume Zao? Mnawaonea, Kuwabambikizia Kesi na Kuwafunga bila hatia? Mnavunja Katiba kwa Makusudi kwa Majivuno ya Madaraka? Angalia Mfano wa Kileo cha Madaraka Kilipomfikisha Aliyekuwa DC wa Hai SABAYA. Hakika Ukikiuka KIAPO ulichoapa kwa Kumtaja MUNGU lazima MUNGU atakuadhibu.

JamiiForums2073931459.jpg
 

kalonji

JF-Expert Member
Feb 17, 2021
6,198
2,000
Ili kuiondolea nchi laan ya umwagaji damu na maovu yafaa wote walioshiriki uovu wawajibishwe.Nyumba yafaa isafishwe yote kabisa.
 

kalonji

JF-Expert Member
Feb 17, 2021
6,198
2,000
Angalau waislamu umuogopa Mungu kwenye nadharia ya uongozi wamejitosheleza uogopa kuumiza watu kesho watalipa.
 

kalonji

JF-Expert Member
Feb 17, 2021
6,198
2,000
Kanuni za kuongoza watu ni mbili epuka hivi usilete laana kwenye uzao wako.

1.Usimwage damu ya mtu.

2.Usimwage machozi ya mtu.

Ukifanya hivi kesho haupo laana ubakia kwenye uzao wako.Jiulize why baadhi ya familia za wazazi wao waliwahi kuwa viongozi azifanani.
Ni kwa sababu baba zao walimwaga machozi na damu za watu.
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom