Tetesi: Madaraka ni dhamana ya muda mfupi sana. Je, Lukuvi kumpiku Majaliwa?

Yote hiyo kwa kuwa na sisi tunapinga kila kitu, watabadilika tuu kama na sisi tunaweza kuona kuna kizuri wanakifanya.

Chuki huzaa chuki, wema huzaa wema. Ukiniona mimi ni mjinga na kweli ni mjinga ukiniambia na ukasisitiza mimi ni mjina , haitotokea nikapata nafasi ya kutafakari werevu wako. Nitakachoangalia ni dharau ulionayo kuhusu mimi.

CCM hawahitaji kura zetu bali sisi tunahitaji kura zao.
Hakuna kitu CCM itajifundisha kutoka kwetu ila sisi tuna mengi ya kujifundisha kutoka kwao.

Baada ya matokeo ya Uchaguzi mkuu huu, Chadema inatakiwa kuwa na sobriety kwa uchambuzi wa kina na marejeo karibu maeneo yote kichana , kiuongozi,mahusiana na vyama vingine ndani na nje ya nchi, kuset political goals, kuset electoral policies. Na kutengeneza strategy na ku achieve our goals hata ikiamanisha tuwe na overall changes.
 
Kwa taarifa yako ni kwamba kwenye uchaguzi huu hakuna kura yoyote iliyopigwa na wananchi iliyohesabiwa , matokeo ya kila jimbo yalipangwa wiki 2 kabla ya uchaguzi , Kwa mfano , Jimbo la Hai matokeo yalitangazwa usiku wa manane huku hata masanduku mengine ya kura yakiwa hayajafika kwenye majumuisho , Masanduku yalikamilika kufikishwa kwenye kituo cha majumuisho saa 2 asubuhi , huku tayari matokeo yakiwa yametangazwa .

Jimbo la Temeke karibu vituo vyote vya kupigia kura ilibandikwa kuwa Lissu kapata kura 19 , vituo vyote ni 19 tu , sasa hata kama huna akili timamu hata hili hukuliona ? ilitajwa wiki moja kabla ya uchaguzi kwamba Tume ilimuandalia Magufuli kura mil 12 , hakuna aliyekanusha , na ikawa hivyo hivyo , haya yote hukuyaona ? Nafahamu unachotaka tukifanye ili ujue hatukuridhika , na bila shaka utakipata , Stay Tuned
Mkuu inaonekana unao ushahidi na uthibitisho wa kutosha, vipi ushafungua kesi ngapi mpaka sasahivi mahakamani zinazohusiana na zoezi zima la uchaguzi?

Haya ngoja nifkrie kuwa hutaki kutumia sheria kupata haki yako, vipi ushaandamana mikoa mingapi mpaka sasahivi kupinga Matokeo?

Kila la kheri Mkuu ngoja Mimi Ni stay tuned kama ulivyosema kusoma nyuzi zako za kulialia baada ya zoezi la uchaguzi kuisha.
 
Nimeuliza ili kupata majibu baada ya tetesi kunifikia, naomba mwenye kujua zaidi atueleweshe.

Na wala haishangazi, hii ni kwa vile uongozi ni kama mbio za kupokezana vijiti, anayeanza siyo anayemaliza.
Sasa wewe kinakuuma nini? Kwani kuna mtu kazaliwa kuwa waziri mkuu pekeake? Chandimu bwana mnaboa mno!
 
Kati ya mimi na wewe unayetumia VPN ku like nyuzi za Magufuli mtu aliyefungia mitandao nani kanyooka ? kwa taarifa yako sisi hatujawahi kukata tamaa na hatutakuja kukata tamaa hadi ccm ing'olewe kwa halali ama kwa haramu
Lakini hili la kuzima mitandao karibia wiki ya pili sasa tunaenda sio haki kabisa watu waungane kwa hili bila kujali chama hii inaumiza biashara za watu na haki ya kupata habari. Sio sawa kabisa tunarudishana miaka 20 nyuma mambo ya kizamani kulazimishana kusoma habari wanazo zipenda wakubwa tu mambo ya magazeti ya Mzalendo na Uhuru ndiko mnatupeleka. Biashara za watu hasara kubwa kwanini tuishi na VPN utasema tuko N.Korea. uchaguzi umeisha mtu kisha apishwa uwoga unatoka wapi wakati tumechaguliwa na almost 85% nchi yote kijani mpaka Pemba mapenzi makubwa, hofu inatoka wapi.
 
Kama ni hivyo ni kwanini wanafanya uchaguzi kupotezea watu muda na pesa. Watu hawalali majumbani mwao wakifanya kampeni kumbe mshindi anajulikana.
Don't warry it will go down in history fisiemu walikipata cha mtema kuni mwaka huu na huo ni ushindi mkubwa kwa cdm.....
cdm watabaki kuwa wafalme wasio na mataji.
 
Nimeuliza ili kupata majibu baada ya tetesi kunifikia, naomba mwenye kujua zaidi atueleweshe.

Na wala haishangazi, hii ni kwa vile uongozi ni kama mbio za kupokezana vijiti, anayeanza siyo anayemaliza.
Ni vizuri umekubali yaishe. Karibu tuungane kujenga nchi yetu na kufuatilia safu ya Mheshimiwa Rais Magufuli. Umeanza vyema, usirudi nyuma na achana na mambo ya CHADEMA. Maendeleo hayana vyama.
 
Lakn mkuu ulidai Lissu asipoapishwa bas ndo mwisho wa tz, vip mbna thread zako zinaonyesha tz inasonga mbele?
Usikenyue sana meno bado mapema, yajayo ni Usiku wa kiza...usishangae mkaanza kuchapana AK-47 wenyewe kwa wenyewe huko Lumumba maana kwa Sasa hatakuepo Lissu wa kupigwa risasi
 
Mkuu inaonekana unao ushahidi na uthibitisho wa kutosha, vipi ushafungua kesi ngapi mpaka sasahivi mahakamani zinazohusiana na zoezi zima la uchaguzi?

Haya ngoja nifkrie kuwa hutaki kutumia sheria kupata haki yako, vipi ushaandamana mikoa mingapi mpaka sasahivi kupinga Matokeo?

Kila la kheri Mkuu ngoja Mimi Ni stay tuned kama ulivyosema kusoma nyuzi zako za kulialia baada ya zoezi la uchaguzi kuisha.
Foolish, Clueless idiot
 
Hakuna waziri mkuu aliewahi kuwa Rais Tanzania

Ukiteuliwa uwaziri mkuu maana yake hutakuja kuwa Rais na hutoshi kuwa Rais
Rejea historia vizuri Mkuu, maana kumbukumbu zinaonyesha kuwa J.k. Nyere ndiye Waziri Mkuu wa kwanza wa Tanganyika na bado alikuja kuwa Rais wa nchi hii
 
WAZIRI MKUU NI UMMY MWALIMU.

WAZIRI MKUU NI UMMY MWALIMU.

WAZIRI MKUU NI UMMY MWALIMU.

Nimeandika mara tatu kuonyesha nina uhakika.

Mods msifute hii post.
 
Back
Top Bottom