Maajabu mengine jijini Dar es Salaam, katika pitapita yangu nimekutana na wananchi wanalalamika wanaitaji magari ya maji taka yafike kuwanyonyea vyoo vyao vimejaa na wenye magari wamegoma maana hawana sehemu yakumwaga majitaka maana madampo yamefungwa ghafla, madreva wamedai dampo la tabata lilifungwa na baada ya kufungwa wakawa wanaenda kumwaga Kurasini jana ghafla na dampo la kurasini lilifungwa nakusababisha usumbufu mkubwa kwa wale waliokuwa wameishakuwa na taka kwenye mgari yao. Hapa nimeshindwa kuelewa hawa wahusika wa madambo wanachozingatia katika swala zima la afya. Inamaana wanachi vyoo vinapojaa wafanyeje? au hawa wenye magari wakayamwage wapi!!!! anayefahamu swala zima la haya madambo naomba nieleweshwe. la afya, kurasini lilifungwa