chakii
JF-Expert Member
- Sep 15, 2013
- 20,392
- 24,963
Kilio cha hali ngumu ya maisha kwa Januari kimeendelea kupamba moto na safari hii kimewafikia madalali wa nyumba ambao walikuwa wakitengeneza pesa chekwa hususani mwanzoni mwa mwaka.
Tofauti na ilivyokuwa miaka mingine, inadaiwa kuwa biashara ya nyumba za kupangamwaka huu imedorora kutokanana kukosekana kwa wateja.
Mwananchi ilizungumza na wenye nyumba na madalali kadhaa wa jiji la Dar es Salaam, Mbeya, Tanga na Iringa ambao walieleza kuwa hali imekuwa tofauti kwa mwaka huu na sababu kubwa ikitajwa kuwa ni hali ngumu ya maisha.
Madalali hao walilalamika kuwa hali hiyo imesababisha maisha kuwa magumu kutokana na kutegemea kazi hiyo kuwaingizia kipato.Mmoja wa madalali hao, Juma Kinole ambaye anafanya shughuli zake Tabata, alisema mwaka huu umeanza vibaya kwao na mambo yatakuwa mabaya zaidi endapo hali itaendelea kuwa hivyo.
Dalali huyo alieleza kuwa, awali alikuwa akipangisha nyumba mbili hadi tatu kwa siku lakini sasa hivi anaweza kumaliza wikibila kupata mteja.“Wateja wengi walikuwa ‘nyumba ndogo’ (vimada) na ndiyo walikuwa wanatupa kazi lakini sasa mambo yanaonekana kuwa tofauti.
Hakuna wateja, inawezekana waliokuwa wanawapangishia wamejitoa kutokana na hali ngumu ya maisha.”Kinole alisema kwa kiasi kikubwa hali hiyo imewasababisha watu waliokuwa wakijenga kuhamia hata kabla ya nyumba zao kukamilika.“Mtu anaona bora ahamie kwenye banda lake hata kama halijaisha ili kukwepa kodi.
Ukitembea sasa hivi nyumba nyingi hazina wapangaji kilio kikubwa kimekuwa pesa.”Kando na hilo, Kinole alisema wapo wapangaji ambao wamehama nyumba kubwa na kwenda kupanga chumba au vyumba viwili kwa lengo la kupunguza gharama za kodi.
Kauli hiyo inaungwa mkono na dalali wa Ubungo, Salum Saleheanayeeleza kuwa kuna idadi kubwa ya nyumba ziko wazi hazina wapangaji na nyingine zikitakiwa kuuzwa.“Nyumba zimekuwa nyingi hakuna wateja.
Yaani nyumba ya kupanga inaweza kukaa muda mrefu bila kupata mpangaji hali haikuwa hivi. Hatakwa nyumba zinazouzwa mambo yamekuwa magumu, watu wanatangaza kuuza lakini hakuna wateja.”Bei ya kupanga katika nyumba zilizopo Tabata Segerea zimeendelea kushuka.
Zilizokuwa zikipangishwa kwa Sh200,000 zimeshuka hadi kati ya Sh170,000 na Sh150,000 kwa mwezi.
Baadhi ya wapangaji ambao walimudu kupanga nyumba nzima wameanza kupunguza matumizi kwa kuhamia katika vyumba vichache ili kuendana na hali ya kiuchumi.
Mkazi wa Tabata Segerea aliyejitambulisha kwa jina moja la Winnie alisema amelazimika kuhamia katika nyumba ya rafikiyake baada ya kukubaliana ili walipe nyumba ya pamoja ya Sh250,000 kwa mwezi akihama katika nyumba ya Sh400,000 aliyokuwa akilipiwa na mpenzi wake.
“Tunaishi marafiki watatu, wote tulikuwa tukilipiwa na marafiki zetu wa kiume lakini wote kwa sasa wamesema hawana fedha na kodi zimeisha, imebidi tukubaliane kuchangishana fedha na kupanga angalau nyumba aliyokuwa akiishi mwenzetu kwa gharama ya chini ili maisha yaendelee,” alisema Winnie.
Chanzo: Mwananchi Online