BAK
JF-Expert Member
- Feb 11, 2007
- 124,790
- 288,098
Madalali kutumika kubana mafisadi
Mwandishi Wetu
Daily News; Tuesday,March 25, 2008 @00:02
Serikali yatangaza zabuni, zipo kampuni na watu 1000
SERIKALI imeamua kutumia madalali kukusanya takribani Sh bilioni 200 zilizochotwa na watu na kampuni zipatazo 1,000 kupitia mpango wa Uagizaji wa Bidhaa Nje (CIS) lakini zikatumika kwa matumizi mengine bila kurudishwa, imefahamika.
Kutokana na uamuzi huo Serikali kupitia Wizara ya Fedha na Uchumi tayari imetangaza zabuni yenye lengo la kuwapata madalali hao ambao watakuwa na jukumu la kukusanya fedha hizo ambazo zilitolewa na Serikali ya Japan chini ya mpango wa kusamehe madeni kwa watu na makampuni 916.
Japan ilitoa wakati huo Yen bilioni 16.6 ambazo kwa kiwango cha sasa cha ubadilishanaji cha Yen moja kwa Sh 12 ni sawa na Sh bilioni 199. Zabuni za ukusanyaji wa madeni hayo zinatarajiwa kufunguliwa baadaye wiki hii mjini Dar es Salaam na waombaji wamepewa masharti kadhaa, ikiwamo kuambatanisha dhamana ya Sh milioni mbili.
Kwa mujibu wa tangazo la Serikali, hatua ya kuwatumia madalali inatokana na nia ya Serikali ya kuhakikisha katika mwaka huu wa fedha inakusanya fedha zote zilizochukuliwa chini ya mpango huo miaka kadhaa iliyopita lakini hadi leo hazijarudishwa.
Mpango huo wa CIS ulilenga kuwajengea uwezo wananchi waweze kuagiza bidhaa kutokana na uhaba wa fedha za kigeni ulioikumba nchi wakati huo.
Mabilioni hayo yalichotwa kuanzia miaka ya 1980 mpaka mwaka 1993. Fedha hizo zilitolewa na wahisani mbalimbali chini ya mpango huo CIS ili kuipa uwezo Serikali wa kuimarisha uchumi wake, ikiwamo Japan ambayo imekuwa inatoa misaada mingi kwa Tanzania.
Lengo la wahisani kutoa fedha hizo ilikuwa kuzipatia taasisi, kampuni, viwanda na biashara mbalimbali uwezo wa kuagiza bidhaa na mali ghafi kutoka nje kwa kuwa wakati huo nchi ilikuwa na upungufu mkubwa wa fedha za kigeni.
Hata hivyo wafanyabiashara wengi waliochukua fedha hizo ambazo zilitolewa kama mkopo wa masharti nafuu ambao hauna riba, walishindwa kuagiza bidhaa kutoka nje kama ilivyokusudiwa na serikali badala yake wakazitumia kwa manufaa binafsi.
Hivi karibuni gazeti hili liliripoti kuwa baadhi ya watu waliochota fedha hizo wameanza kuzirejesha baada ya serikali kutishia kuwaanika hadharani iwapo hawatalipa. Katika urejeshwaji huo mfanyabiashara mmoja maarufu wa Dar es Salaam ambaye hakutajwa jina alielezwa na maofisa wa Hazina kwamba alilipa Sh milioni 700.
Mapema mwaka huu Wizara ya Fedha ilitishia kuwaanika hadharani na kuwachukulia hatua za kisheria wakopaji wa CIS kama hawatalipa deni hilo ndani ya kipindi cha miezi mitatu tangu tangazo hilo lianze kutoka kwenye vyombo vya habari.
Miongoni mwa wadaiwa hao wamo wafanyabiashara maarufu nchini, wanasiasa wakiwamo wabunge na baadhi ya maofisa wa serikalini. Gazeti hili lina habari kuwa baadhi ya wadaiwa hao wengine walitumia kampuni bandia kujipatia fedha hizo hali iliyosababisha kushindwa kuagiza bidhaa hizo kama ilivyotarajiwa na Serikali.
Mara kadhaa baadhi ya wafanyabiashara wamewahi kuchunguzwa na taasisi mbalimbali ikiwamo Takukuru juu ya namna walivyochota mabilioni hayo kwa njia ya uongo na kisha kushindwa kuyarejesha serikalini.
Kitendo hicho kilikuwa cha kwanza cha kifisadi kufanyika nchini na tangu wakati huo baadhi ya wafanyabiashara walijineemesha hali inayoaminika iliwafanya waendelee kujichotea fedha nyingine serikalini kwa kutumia mianya mbalimbali na udhaifu wa watendaji.
Kwa mujibu wa masharti yaliyowekwa na Serikali wakati huo wa ukopaji wa CIS, mkopaji akishindwa kulipa kwa kipindi cha miezi 18 tangu achukue mkopo alikuwa analazimika kulipa riba ya asilimia 17.
Fedha zilizokusanywa kutokana na deni hilo zilikuwa zinatarajiwa kutumika kuchangia mapato ya Serikali na miradi maalumu ya maendeleo baada ya makubaliano na wahisani husika.