Madalali kila sekta nchini: Hivi hakuna njia ya kuwakomesha au kuwasimamia? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Madalali kila sekta nchini: Hivi hakuna njia ya kuwakomesha au kuwasimamia?

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Peter Agostino, Dec 21, 2016.

 1. P

  Peter Agostino Member

  #1
  Dec 21, 2016
  Joined: Sep 23, 2016
  Messages: 47
  Likes Received: 44
  Trophy Points: 25
  Huwezi ukajua ubaya na kero za madalali mpaka siku utakapokuwa na shida ya kuuza au kununua kitu ambacho ni sharti kwanza kipitie mikononi mwa madalali. Siyo siku nyingi nilikuwa natokea mkoani Kilimanjaro nikiwa na mzigo ambao ilinibidi kutumia malori au fuso zinazotokea Moshi mjini kuja Dar muda wa jioni kuanzia saa 12.

  Nikiwa njia panda ya Himo na Moshi ilinibidi kusubiri pale kwa ajili ya kupata lori lenye nafasi ya kupakiza mzigo niliokuwa nao. Lakini cha kustaajabisha nilizungukwa na vijana kibao waliojitammbulisha kuwa wao ni madalali ambao kazi yao ni kuwaunganisha wasafiri na malori yanayobeba mizigo kuelekea maeneo mbalimbali toka pale njia panda na walinitaka kupatana nao bei ya kunitafutia usafiri. Kazi kubwa wanayoifanya wao lori linapokuja ni kuliwahi kabla halijasimama na kwenda kuzungumza na dereva wakishaelewana kiasi cha pesa ndipo sasa huja na kupakia mzigo wako.

  Kiasi wanachopatana na wewe huwa karibu mara mbili ya kiasi wanachompa dereva wa lori na ikiwa hutaki basi unaweza ukakesha kituoni. Nilikomaa kuwapa kiasi walichohitaji na kwa kweli nikajikuta saa nne ya usiku inanikutia pale njia panda, kila lori likija walikuwa wanafanya ujanja na kumwambia dereva "huyu jamaa kabeba mzigo wa ishu ondoka hafai". Kwa kweli ilinibidi siku hiyo kuahirisha safari yangu mpaka kesho yake asubuhi nikaja kuondoka na coster. Tena kibaya zaidi vijana wale walishaanza kupanga njama za kunipora kama ningeendelea kukaa pale kituoni, bahati gesti haikuwa mbali nikaingia fasta.

  Sekta nyingi zimejaa madalali na inavyoonekana wanakuwa juu ya sheria hakuna chombo chochote cha kuwasimamia, nashukuru mabasi ya mwendokasi kwa upande wa daladala yamekomesha kabisa kero za wapigadebe ambao ni aina hiyohiyo ya madalali. Lakini bado kuna madalali maeneo mengine mengi kama masokoni, mitaani na hata sekta zingine. Sikatai madalali wana umuhimu wake lakini ninachopinga hapa ni zile dhuluma wanazowafanyia watu kama kwamba hakuna chombo cha kuwasimamia au serikali. Mbona kwa upande wa madalali wa Hisa ambako kuna udhibiti mambo huwa hayaendi kiholela namna hiyo?
   
 2. Humble African

  Humble African JF-Expert Member

  #2
  Dec 21, 2016
  Joined: Jul 28, 2013
  Messages: 3,709
  Likes Received: 7,395
  Trophy Points: 280
  Wanaudhi!
   
 3. bily

  bily JF-Expert Member

  #3
  Dec 21, 2016
  Joined: Apr 5, 2012
  Messages: 8,053
  Likes Received: 4,048
  Trophy Points: 280
  Sasa Kama ngosha kanunua bombardier via madalali sembuse vitu vidogo hivyo hiyo Bongo asee. Bado Boeing madalali kamakawa.
  #bringbackBenAlive
   
 4. B

  Babati JF-Expert Member

  #4
  Dec 21, 2016
  Joined: Aug 7, 2014
  Messages: 31,838
  Likes Received: 25,113
  Trophy Points: 280
  Pole sana mkuu, ndiyo mfumo wetu.
   
 5. P

  Peter Agostino Member

  #5
  Dec 21, 2016
  Joined: Sep 23, 2016
  Messages: 47
  Likes Received: 44
  Trophy Points: 25
  Asante, ila mi naona ni kama vile wanunuaji na wauzazi(tunaohitaji huduma) tunaogopa ama tunakosa ushirikiano, hivi hatuwezi tukaamua kugomea huduma za madalali wadhalimu kama hao wanaodai malipo makubwa mara 2 ya bidhaa/huduma inayodalaliwa? Tutaendelea kuwa kama nyumbu mbele ya simba mpaka lini?
   
 1. This site uses cookies to help personalise content, tailor your experience and to keep you logged in if you register.
  By continuing to use this site, you are consenting to our use of cookies.
  Dismiss Notice
 1. This site uses cookies to help personalise content, tailor your experience and to keep you logged in if you register.
  By continuing to use this site, you are consenting to our use of cookies.
  Dismiss Notice
Loading...