BABU CHONDO
JF-Expert Member
- Jun 6, 2011
- 855
- 139
hii nchi tunaipeleka pabaya sasa,kwanini kila siku migomo na mogogoro hawa ma Dr. tutauuwa wangapi kwa mogomo,athari ya migomo ya migomo kama ni mbaya sana.
Je wagonjwa wetu itakuwaje??Kwa mujibu wa chanzo muhimu katika wizara ya afya, Serikali imejiandaa kuchukua hatu kali kwa madaktari wote waliogoma ifikapo kesho Ikiwa ''Ni pamoja kuwafukuza kazi na utumishi'' baada ya juhudi za Serikali na za Kimahakama ''KUTOHESHIMIWA''. Pamoja na hatua hizo pia taratibu za kuandaa madktari mbadala toka taasisi nyingine za Serikali ikiwa ni pamoja na uwezekano wakupata msaada wa dharura wa Madaktari toka mojawapo ya Nchi za Afrika Mashariki, zinaendelea vizuri. Aidha ulinzi nao unaendelea na utaendelea kuimarishwa katika sehemu na maeneo mbalimbali.
Kauli hii bila shaka ina underline tamko la Serikali leo Bungeni kuwa '' LIWALO NA LIWE''
Hakuna cha kuandaa madaktari mbadala wala kupata msaada wa madaktari kutoka east africa, madaktari/manesi wote
wakiamua kugoma serikali ni lazima inywee...
Mkuu inaonekana ujui nguvu ya dola weye!
Wachina wanaweza kuichukua hospitali nzima na hao wafanyakazi kulipwa na serikali yao ya uchina ,kuna madaktari kama milioni moja hawana kazi nchini China.
Inapokuja ishu ya Job Security wabongo huwa hawaaminiki kabisa, kusalitiana dakika yoyote. Job Security ndio inamfanya Nape anageuka vuvuzela, sitashangaa kama itawafanya madaktari wasitishe mgomo. Hapo Pinda kawatishia njaa madaktari, tuone ubavu wao.
Issue ya madaktari ni ngumu sana kama serikali inadhani kuwafukuza ndio njia muafaka, kabla ya kutekeleza uamuzi huo iende kujifunza hapo Kenya walipotangaza kuwafukuza kazi walifanikiwa kwa kiwango gani? Mwisho wa siku waliwarudisha kazini wote bila masharti yoyote.
Hata uingereza juzi tu madaktari wamegoma na hatukusikia serikali huko ikitangaza kuwafukuza ama kwenda mahakamani. Walikaa kwenye meza ya mazungumzo na kuyamaliza.
Serikali yetu ijifunze kuzungumza na kuwa wakweli kutekeleza makubaliano, vinginevyo migomo hii haitakwisha kamwe hata kama watatumia nguvu nyingi na vitisho kiasi gani.
Watanzania acheni uoga,na hili nalilekeza kwa madaktari wetu,ni hi kama kweli ni madaktari wa ukweli sio kama JK,nawaomba msihofu kwa lolote,na wala msifikiri hakuna maisha nje ya ajira za serikalini,maisha yapo tu na kama ingelikuwa hivyo basi ni watu wngi sana wangelikuwa wameshakufa,ajira zipo kupita kujiajiri au kuajiriwa nje ya serikalini.msiogope juu ya haya maisha na hii ni mwanzo tu kwamba safari ya ukombozi ndio imeeaza,na kwenu niynyi wasomi sitegemei kama mtatishika na kufukuzwa au vyovyote,maaan hawana maana hawa mmemsikia Pinda amesema liwalo na liwe.hiyo ipokeeni na muikabili.
Umoja ni nguvu
Wacha kuota ndoto za jioni wewe! Suluhu nini kila Dr mmoja serikali imlipe milioni 13 kwa mwezi?
dola dhaifu nayo unaiita dola?
LIWALO NA LIWE ni vita kali kati ya Madaktari na Serikali...
Wachina wanaweza kuichukua hospitali nzima na hao wafanyakazi kulipwa na serikali yao ya uchina ,kuna madaktari kama milioni moja hawana kazi nchini China.
kelele za nini mwehu wewe! si usubiri watimize km wanaubavu huo wa kufukuza madk wote! sijui manesi na watalaam wengine unawatoaje kwny mgogoro huu, miaka ya 90 siyo leo!jigoku usiwape moyo bure (hapo pekundu). Hivi unajua kuna madaktari wangapi Tanzania? Halafu unajua kuna private hospitals ngapi Tanzania, na unajua zina uwezo wa kuajiri madaktari wangapi?.
Kama una kumbukumbu nzuri, miaka ya 90 serikali ilistopisha ajiri zote, nadhani uliona madaktari, manesi kibao walivyokuwa wamejaa mitaani bila kazi.
mbona hata mgomo uliopita walisema tunafukuzwa kazi?
Zile billion 300 zingekuwa haziwekezwi Swiss na wajanja nafikiri mishahara isingekuwa tatizo!!
Dr.Chichi kumbe bado hujaona tofauti ya mgomo uliopita na huu wa sasa! Ule wa mwanzo hakukua na amri ya serikali, hivyo serikali ingewafukuza kazi ingebidi iwalipe, which is another burden to the gvt. Safari hii imecheza tricky ambayo wengi wenu hamjaijua, ukifukuzwa hupati chochote maana umedharau amri halali ya mahakama, chezeya dola weye!
Halafu mkuu mjifunze kusoma alama za nyakati. Safari hii hamna back-up ya wananchi, watu wengi hawako upande wenu kwa sababu mmekuwa too demanding and not considerate!
Wacha kuota ndoto za jioni wewe! Suluhu nini kila Dr mmoja serikali imlipe milioni 13 kwa mwezi?