Madaktari wote waliogoma kufukuzwa kazi na utumishi!

DATAZ

JF-Expert Member
May 25, 2012
2,448
5,974
Kwa mujibu wa chanzo muhimu katika wizara ya afya, Serikali imejiandaa kuchukua hatu kali kwa madaktari wote waliogoma ifikapo kesho Ikiwa ''Ni pamoja kuwafukuza kazi na utumishi'' baada ya juhudi za Serikali na za Kimahakama ''KUTOHESHIMIWA''.

Pamoja na hatua hizo pia taratibu za kuandaa madktari mbadala toka taasisi nyingine za Serikali ikiwa ni pamoja na uwezekano wakupata msaada wa dharura wa Madaktari toka mojawapo ya Nchi za Afrika Mashariki, zinaendelea vizuri. Aidha ulinzi nao unaendelea na utaendelea kuimarishwa katika sehemu na maeneo mbalimbali.

Kauli hii bila shaka ina underline tamko la Serikali leo Bungeni kuwa '' LIWALO NA LIWE''
 
...baada ya juhudi za Serikali na za Kimahakama KUTOHESHIMIWA Pamoja na hatua hizo pia taratibu za kuandaa madktari mbadala toka taasisi nyingine za Serikali ikiwa ni pamoja na uwezekano wakupata msaada wa dharura wa Madaktari toka mojawapo ya Nchi za Afrika Mashariki, zinaendelea vizuri
mtawalipa sh. Ngapi ndg wewe na serikali yako? Kwenye rangi pana utata na unachokisema.
 
LIWALO NA LIWE ni vita kali kati ya Madaktari na Serikali...
 
Kwa mujibu wa chanzo muhimu katika wizara ya afya, Serikali imejiandaa kuchukua hatu kali kwa madaktari wote waliogoma ifikapo kesho Ikiwa ''Ni pamoja kuwafukuza kazi na utumishi'' baada ya juhudi za Serikali na za Kimahakama ''KUTOHESHIMIWA''. Pamoja na hatua hizo pia taratibu za kuandaa madktari mbadala toka taasisi nyingine za Serikali ikiwa ni pamoja na uwezekano wakupata msaada wa dharura wa Madaktari toka mojawapo ya Nchi za Afrika Mashariki, zinaendelea vizuri. Aidha ulinzi nao unaendelea na utaendelea kuimarishwa katika sehemu na maeneo mbalimbali.

Kauli hii bila shaka ina underline tamko la Serikali leo Bungeni kuwa '' LIWALO NA LIWE''

Wala hiyo sio suluhu ya matatizo ya madaktari,kwani hao wanaotaka kuwaomba kutoka nchi za Afrika Mashariki kwao hakuna wagonjwa? Na wakija huku watafanya kazi bure? Mimi naona serikali ya JK inatulazimisha kuitoa madarakani kwa nguvu. Na katika hili ni lazima iondoke.
 
Wacha kuota ndoto za jioni wewe! Suluhu nini kila Dr mmoja serikali imlipe milioni 13 kwa mwezi?
 
akili yao serikali inafikiri doctor wote ni sawa yaani jk na ulimboka ni sawa? kenya walijaribu wakashindwa madocta sio kitu ya mchezo kama waalimu wanavyochezewa na wao wanachezea elimu ya watoto wa taifa linakuwa la kijinga kama form one hawezi kuandika na kusoma kitabu cha darasa la pili
 
Wachina wanaweza kuichukua hospitali nzima na hao wafanyakazi kulipwa na serikali yao ya uchina ,kuna madaktari kama milioni moja hawana kazi nchini China.
 
Kwa mujibu wa chanzo muhimu katika wizara ya afya, Serikali imejiandaa kuchukua hatu kali kwa madaktari wote waliogoma ifikapo kesho Ikiwa ''Ni pamoja kuwafukuza kazi na utumishi'' baada ya juhudi za Serikali na za Kimahakama ''KUTOHESHIMIWA''. Pamoja na hatua hizo pia taratibu za kuandaa madktari mbadala toka taasisi nyingine za Serikali ikiwa ni pamoja na uwezekano wakupata msaada wa dharura wa Madaktari toka mojawapo ya Nchi za Afrika Mashariki, zinaendelea vizuri. Aidha ulinzi nao unaendelea na utaendelea kuimarishwa katika sehemu na maeneo mbalimbali.

Kauli hii bila shaka ina underline tamko la Serikali leo Bungeni kuwa '' LIWALO NA LIWE''
Hakuna cha kuandaa madaktari mbadala wala kupata msaada wa madaktari kutoka east africa, madaktari/manesi wote
wakiamua kugoma serikali ni lazima inywee...
 
Inapokuja ishu ya Job Security wabongo huwa hawaaminiki kabisa, kusalitiana dakika yoyote. Job Security ndio inamfanya Nape anageuka vuvuzela, sitashangaa kama itawafanya madaktari wasitishe mgomo. Hapo Pinda kawatishia njaa madaktari, tuone ubavu wao.
 
Mm nashauri TIMUA wote hii ndo Serikali legelege kwani hawa maDr wapo kisiasa zaidi sio wazalendo na wanasukumwa Chama cha Siasa
Mwl Nyerere aliwachapa viboko kina Sitta UDSM na kuwatimua, akawatimua maPOLISI na RPC
 
Kufukuza madaktari wote sio kazi rahisi kama tunavyodhani...halafu kuwafukuza udaktari sio kuwavua udaktari. Udaktari ni taaluma ambayo mtu anapata baada ya kupitia shuleni kwa muda wa miaka kadhaa...kama wangefanya hivi kwa wakurugenzi wa wilaya na hawa wanaoficha hela kule uswisi mbona Tanzania ingeheshimika.Hili la kufukuza madkatari ni kutesa tu wananchi. By the way daktari sio lawyer au mchumi....tukiwakosa kwa wiki moja tu tutaona cha mtema kuni
 
Hakuna cha kuandaa madaktari mbadala wala kupata msaada wa madaktari kutoka east africa, madaktari/manesi wote
wakiamua kugoma serikali ni lazima inywee...

Tukifukuza wengine tutawapata wapi? Tunaota ndoto za mchana mchana...lets be serious on some issues. Kama wabunge wanapewa wanachodai, why not doctors?
 
Kwa mujibu wa chanzo muhimu katika wizara ya afya, Serikali imejiandaa kuchukua hatu kali kwa madaktari wote waliogoma ifikapo kesho Ikiwa ''Ni pamoja kuwafukuza kazi na utumishi'' baada ya juhudi za Serikali na za Kimahakama ''KUTOHESHIMIWA''. Pamoja na hatua hizo pia taratibu za kuandaa madktari mbadala toka taasisi nyingine za Serikali ikiwa ni pamoja na uwezekano wakupata msaada wa dharura wa Madaktari toka mojawapo ya Nchi za Afrika Mashariki, zinaendelea vizuri. Aidha ulinzi nao unaendelea na utaendelea kuimarishwa katika sehemu na maeneo mbalimbali.

Kauli hii bila shaka ina underline tamko la Serikali leo Bungeni kuwa '' LIWALO NA LIWE''

Madaktari kutoka kenya count them out; maana huko kwao nako kunafukuta mgomo kama huu hapa, hivi vinchi vingine doctor patient ration ni worse than our own here, sasa watume madaktari huku kwao kuungue! mambo ya ajabu kabisa. hapa ndani hakuna reserve pool ya madaktari labda wawafufue wastaafu ili wakaue wagonjwa. Kweli hii ni fire brigade management style, tanzania tunayoitaka iko mbali kweli kweli! god save our souls.
 
Serikali gani iwatimue, kama ni hii ya DHAIFU,lets wait and see,akiwatimua atawatibu yeye kwa udaktari wake wa kumaliza mgogoro kenya? Shame on him!
 
Back
Top Bottom