madaktari wetu wanatupeleka wapi?

Kinyau

JF-Expert Member
Nov 24, 2006
910
702
nimesoma kwa masikitiko hii habari kutoka mwananchi. naomba na nyie wanabodi muone uzembe wa wahudumu wetu wa afya.

"Aliyeumia mguu apasuliwa kichwa, wa kichwa apasuliwa mguu.
Na Jackson Odoyo


WAGONJWA wawili waliokuwa wamelazwa katika Taasisi ya Mifupa (MOI) Muhimbili wamefanyiwa upasuaji tofauti na matatizo yaliyokuwa yakiwasumbua.


Wagonjwa hao walifanyiwa upasuaji Novemba Mosi, mwaka huu kwa nyakati tofauti katika taasisi hiyo, ambapo aliyekuwa na matatizo ya mguu alipasuliwa kichwa na wa kichwa akapasuliwa mguu.


Mmoja wa wagonjwa hao Immanuel Didas, aliyeumia goti baada ya kupata ajali ya pikipiki hivi karibuni na kulazwa katika taasisi hiyo, alifanyiwa uchunguzi na madaktari kushauri kwamba afanyiwe upasuaji wa goti hilo.


Hata hivyo katika hali isiyokuwa ya kawaida, wakati wa kumpatia huduma hiyo, madaktari waliohusika walimfanyia upasuaji wa kichwa badala ya goti.


Katika kile kinachoonekana kuchanganyikiwa kwa madaktari hao, mgonjwa mwingine, Immanuel Mgaya ambaye pia alilazwa MOI kwa matatizo ya kichwa na uchunguzi kubaini kuwa anatakiwa kufanyiwa upasuaji wa kichwa, badala yake alifanyiwa upasuaji wa mguu.


Mwandishi wa Mwananchi alizungumza na ndugu wa wagonjwa hao kuhusiana na matatizo yaliyowafika ndugu zao wakati wanapatiwa huduma ya matibabu katika taasisi ambayo waliweka bayana magonywa yaliyokuwa yanawasumbua, lakini wakapata mshangao baada ya kutibiwa tofauti na matatizo yao.


Kaka wa Immanuel Didas, Sisti Marishay alisema mgonjwa wake alikwenda hospitalini hapo kwa matatizo ya goti baada ya kupata ajali ya pikipiki, lakini alipopigwa picha za x-ray hakuwa na matatizo katika mfupa ila kulikuwa na uvimbe kwa ndani ndipo madaktari wakashauri afanyiwe upasuaji ili kuuondoa.


Alisema katika hali ya kusikitisha madaktari hao walimfanyia upasuaji kichwani wakati alikuwa haumwi kichwa.


"Kilicho fanyika ni uzembe wa hali ya juu, kwa sababu mdogo wangu alikuwa anaumwa mguu na sio kichwa, wao wakamfanyia upasuaji wa kichwa na baada ya kutokea tatizo hilo, nilizungumza na Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi hiyo, Profesa Laurent Museru ambaye alikiri kwamba kuna makosa yametokea hivyo wameamua kukaa na kuunda tume ya kuchunguza uzembe huo kisha watatoa taarifa baada ya wiki moja," alisema Marishay.


Marishay alisema kwa sasa hawawezi kuchukua hatua yoyote mpaka watakapo pata majibu ya tume iliyoundwa na taasisi hiyo kuchunguza suala hilo.


Ndugu mwingine wa Didas, Ludani Didas naye alisema kwa sasa hawezi kuzungumzia uzembe huo uliofanywa na madaktari hao kwa sababu mpaka sasa mdogo wake amelazwa katika chumba cha wagonjwa mahututi (ICU).


"Mpaka dakika hii mdogo wangu hajitambui, hawezi kuzungumza chochote na yuko ICU, sasa mimi nitazungumza kitu gani, tusubiri nione hatima ya afya yake ndipo nitazungumzia uzembe huu wa wazi kabisa tena kwa wanyonge," alilalamika.


Naye mama mzazi wa Immanuel Mgaya aliyefanyiwa upasuaji wa mguu badala ya kichwa, Mary Mgina akiwa kwenye Wodi na 17, Sewahaji alimolazwa kijana wake, alisema alifika hospitalini hapo akitokea Njombe, mkoani Iringa wiki iliyopita.


"Tulikuja wiki iliyopita tukitokea Njombe katika Hospitali ya Kibena ambapo walituandikia barua kuja hapa kwa matibabu zaidi ya kichwa kilichoanza kumuuma ghafla siku chache baada ya kuanza mitihani ya kidato cha nne akiwa kwenye chumba cha mtihani," alisema Magina.


Alisema kutokana na tatizo hilo alishindwa kuendelea na mitihani kutokana na kuendelea kuumwa kichwa huku akianguka na kupoteza fahamu, ndipo akahamishiwa MOI ambako baada ya kumchunguza waliamua apasuliwe kichwa ila hawakumweleza ugonjwa unaomsumbua," alisema mama huyo.


Mjomba wa Mgaya, Dick Magina alisema baada ya kufanyiwa upasuaji huo walikabidhiwa mgonjwa aliyefanyiwa upasuaji wa kichwa, lakini hakuwa ndugu yao na walipomkataa walianza kumtafuta na walipompata wakakuta amefanyiwa upasuaji wa mguu na si kichwa.


"Walinikabidhi mgonjwa mwingine tofauti na ndugu yangu nikawakatalia ndipo wakaanza kumtafuta na kumpata akiwa amepasuliwa mguu. Kilicho nishangaza zaidi ni kwamba tangu walipogundua kwamba wamefanya makosa hayo hawajafika kumuona mgonjwa ili wajue anaendeleaje," alisema Mgina na kuongeza;


"Kutokana na uzembe huo uliofanyika tunahitaji matibabu kwa mgonjwa wetu tena kwa gharama zao, pia nimehuzunishwa sana kutokana na makosa yaliyofanyika na hasa kwa wenzetu ambao mgonjwa wao amefanyiwa upasuaji wa kichwa badala ya mguu na hali yake ni mbaya," alisema.


Baadhi ya madaktari na wauguzi wa Muhimbili waliozungumza na mwandishi wa Mwananchi kwa njia ya simu kwa nyakati tofauti jana kwa masharti ya kutoandikwa majina yao gazetini, walidai kuwa uzembe kama huo ni wa kawaida hospitalini hapo.


Walidai kuwa madaktari wengine baada ya upasuaji wanaacha vipande vya pamba, nyembe na hata mikasi ndani ya mwili wa mgonjwa, lakini hufanywa kwa siri na mgonjwa anapofanyiwa upasuaji upya huwa haambiwi sababu ya kumpasua tena.


Baadhi ya wogonjwa waliolazwa katika hospitali hiyo walidai kuwa uzembe kama huo ni wa kawaida kufanyika hospitalini hapo na kudokeza kwamba, hata akina mama wanaojifungua wengine hupewa watoto ambao si wao na wengine huambiwa uwongo kwamba mtoto amefariki muda mfupi baada ya kuzaliwa.


Naye Profesa Museru alikiri kuwepo kwa madai hayo na kusema kwamba, amesikitishwa na tukio hilo na kwamba aliamua kufikisha taarifa hizo wizarani.


Profesa Museru alisema pia wameunda tume ya kuchunguza madai hayo ambayo itaanza kazi leo na kutoa majibu kesho kutwa.


"Ni kweli kuna tukio la aina hiyo hapa hospitalini, lakini kuna taratibu nimeanza kuzichukuwa na sasa hivi ninapozungumza nawe nipo kwenye kikao cha kuunda tume ya kufuatilia na siwezi kukiri au kukataa kuwa ni uzembe, ndiyo maana tunaunda tume ya kuchunguza suala hilo na pia nimeishapeleka taarifa wizarani," alisema Profesa Museru."

by mwananchi
 
inabidi jopo zima wawajibishe na ikiwezekana wafunguliwe mashtaka maana haiingii akilini
 
Thats what we call a https://jamii.app/JFUserGuide up in our goverment hospital...were this Doctors Druck..or in Drugs..am traying to understand them in possive way i cant...how can this be..inamaa hakuna muongozo wa uchunguzi uliofanyika kabla ya wao kuja kufanya operasheni?Poor wagonjwa.
 
yai ni hatari yanayosemwa kuhusu muhimbili ni kweli na nimeyaona mwenyewe, MOI na wodi za wakinamama kuna roho za vifo manesi na ma dr hawawajali wagonjwa na ni wazembe maana hakuna kifungu cha kuwabana wanapofanya uzembe au KUUA KWA KUKUSUDIA. namalizia Muhimbili sio hospitali ya kwenda .....
 
Ni kweli haya ni mambo ya kawaida kwa bongo na sio muhimbili peke yake ni mpaka ikulu kwenyewe,si mliona raisi kapokea mfano wa hundi yenye utata.sio kosa la madaktari bali ni mfumo tulionao ndio wa kuupigia kelele.
 
hali muhimbili inatisha kuna uzembe uliokithiri. Mimi niliwahi kufanyiwa upasuaji wa tumbo pale muhimbili miaka 3 iliyopita,nakumbuka niliwekewa ganzi ya spinal local anasthsesia ambayo hulali kabisa, wakati daktari anakaribia kumaliza umeme ulikatika na wasaidizi wake wakamwachia katochi ka simu ya nokia, I was so scared kuwa ningeshonewa sindano ndani. na hadi natolewa theatre umeme ulikuwa haujarudi. Nilipeleka malalamiko kwa mkurugenzi wa theater operations na wakasema watafuatilia ila nasikia hadi leo bado umeme unatatizo.
Kuna madai mengine kuwa theatre za upasuaji wa kinamama ndio kuna uzembe wa hali ya juu.
sasa sijui wizara husika na uongozi mzima wa muhimbili unafanya nini.
 
""KIHOJA KINGINE CHA MOI""""

Ndugu wa wagonjwa wote mliopata haya madhara kwanza napenda kuwapa pole kwa yale yaliotokea,,kwanza nasikitika kusoma kuna baadhi ya watu wanawa support hawa watu,,(dk),,kisa kingine cha kusikitisha ni kama ifuatavyo nahisi bwana maseru ana kazi kubwa ya kufanya

DADA REGINA LUHANGA NI ALIKUWA MMOJA WA DADA ZETU WALIOPATA AJLI MOMBO MIEZI 2ILIYOPITA,BAHATI MBAYA MUNGU ALMCHUKUA KWANZA YULE ALIEKUWA NAE RAFIKI YAKE WAKIWA WANAENDESHA KUJA DAR ES SALAAM,,
DADA REGINA YEYE ALIPATA MADHARA BAADHI YA SEHEMU IKABIDI APELEKEWE CHARTER NA KAMPUNI ALIOKUKUWA AKIIFANYIA KAZI,,
MUNGU MKUBWA AKAFIKA DAR AKIWA HAI AKAPELEKWA MOJA KWA MOJA HOSPITAL YA MOI,,KUTOKANA NA DK ALIEMCHUNGUZA AKASEMA AMEUMIA KWENYE MABEGA MIGUUNI,,ANAITAJI OPERATION,,MUNGU AKIKUPENDA BASI BINADAMU HATA UFANYEJE,,AKAFANYIWA OPERATION YA KWANZA AKALAZWA ICU,,AKATOKA BAADA YA CKU 3 AKARUDISHWA TENA OPERATION WAMESAHAU KITU KWENYE MGUU,,JAMANI MUNGU AMPE REHEMA ZAKE,,,AKATOKA ,,BAADAEWAKAJA KUREALIZE KWAMBA,,WALIKUWA WANATIBU VITU VINGINE WAKASEMA AMEATHRIKA TUMBONI,WAKASHAURI WAKAMFANYIE X-RAY,,ALIPOANGALIWA AKAKUTWA UTUMBO ULISHAPASUKA SIKU NYINGI NA KUANZA KUOZA ,,JAMANI WALIPOULIZWA KWANINI HAWAKUMFANYIA X-RAY KOTE WANADAI,,HAKUWA ANALALAMIKA KWA TUMBO,,TANZANIA WAPI TUNA KWENDA,,HATIMAE WAKADAI WALIFANYA WAKASHINDWA KUONA KUTOKANA NA DADA ALIKUWA MNENE,,JAMANI KEDE NA SIE WANENE TUKIUMWA TUMBO NDIO TWAFA AU??JAMANI HAWA MOI TUWAAFANYEJE WENGI WANAKUFA KWA UZEMBE HAWASEMI
WAZIRI NAOMBA MLIFANYIE KAZI HUU UZEMBE
 
Africans can't run any viable healthcare system. Any African ran healthcare system is a disaster. It's no wonder people who can afford it go to private hospitals owned by Indians and Europeans. It's not because private hospitals are better funded no! Muhimbili has a bigger budget than many private hospitals but service at private hospitals is 1000 times better. On top of all that many good African doctors tend to flee the country looking for greener pastures. What you are left with is a disaster masquerading as a healthcare system. I feel sorry for the victims!
 
Africans can't run any viable healthcare system. Any African ran healthcare system is a disaster. It's no wonder people who can afford it go to private hospitals owned by Indians and Europeans. It's not because private hospitals are better funded no! Muhimbili has a bigger budget than many private hospitals but service at private hospitals is 1000 times better. On top of all that many good African doctors tend to flee the country looking for greener pastures. What you are left with is a disaster masquerading as a healthcare system. I feel sorry for the victims!
Lack of Standard Operating Procedures!!! The whole System needs thorough scrutiny from the registration process to the time the patient is given the first diagnosis, and further down the operating table. These accidents happen, though they are not new in the medical field they are on many occasion associated with a flaw in the Standard Operating Procedures. The environments involved are dynamic and the chance for an error is always present, but the magnitude of the error which I believe here was more of a combination of two factors:- Human error(from the clerk to the Doctor)and their present Information systemis Whack!!
I hope this wont bring a class action suit against those found guilty of misconduct.
 
walau profesa mwakyusa amewasimamisha kazi hadi uchunguzi utakapokamilika.
 
Inauma sana hii, sana sana, na ni vigumu kuamini kwamba mambo ya kutisha kama haya yanatokea katika hospitali ya kiwango hicho ambayo ni tegemeo kwa matatizo yaliyotajwa.

Hata kama hospitali ikisema itawagharamia matibabu hao iliowaumiza, bado nakosa amani kwani kama matibabu hayo yakifanyika kwenye hospitali hiyo hiyo wanaweza wakawafanyia madudu zaidi. Sasa hivi wagonjwa wale wana hali mbaya zaidi, je tutawaaminije watendaji haohao walioshindwa kuwatibia walipokuwa na hali nafuu? Nasema hivi, mtu kashindwa jambo lilipokuwa bado dogo, sasa limekuwa kubwa zaidi, tuna sababu gani ya kuendelea kumwamini? Yaani huko Bongo tumo kifoni! Tutakimbilia wapi yarabi! Maana hata tukisema washitakiwe hao jamaa, wachukuliwe hatua za kisheria, sawa zitachukuliwa lakini maji yameshamwagika, hayazoleki. Huyo aliyeko huko wanakoita ICU (maskini alikuwa anaumwa GOTI tu!), tumwombee kwa Mwenyezi Mungu amjalie nafuu, lakini je atarudi hali yake ya awali? Maana nasikia wamechokonoa ubongo wake weeeee, walipoona hakuna "kitu" wakafunga mabandeji, lakini fahamu hazikumrudia tena! Na yule aliyekuwa anaumwa kichwa, maradhi yake yako palepale, na zaidi wamemwongezea jeraha mguuni! Jamani! Hata kama si makusudi, hawa jamaa wamefanya kosa by ommission, "kwa kutotimiza wajibu" ndio dhambi yao. Haipaswi kuachwa hivi hivi. Huko kuwasimamisha wahusika kazi hakutaleta maana yoyote kama hazitafanyika jitihada za kuwarejeshea wale wagonjwa hali zao za awali, kuwatibia maradhi waliyokuja nayo, na KUWAFIDIA, ndiyo, wanastahili fidia.

Kama ninayosikia kuwa eti uzembe kama huo ni wa "kawaida" hospitalini hapo, na kwamba eti ni kuwa tu "huwa haitangazwi", nadhani hiki ni kiama. Ni kiama kwa sababu kwanza tunapoteza imani na watu wetu tuliowasomesha kwa gharama kubwa, na hospitali inayogharamiwa kwa asilimia kubwa sana ya bajeti ya wizara husika. Sababu ya pili inayofanya kiama hicho kiwe cha kutisha ni athari za hatua zinazopaswa kuchukuliwa. Je serikali isichukue hatua? Isipotoa adhabu kutakuwa na malalamiko kama haya tuliyonayo sasa hivi na zaidi. Wakitoa adhabu, itabidi wachuunguze wote waliohusika na kosa la sasa na mengine ya namna hiyo, na si ajabu mfumo mzima wa hospitali ukaanguka kwenye hatia. Sasa wapewe adhabu gani? Tukiwafukuza tutakosa wa kututibia (nasikia wako wachache sana hawa jamaa). Najua kuna watakaosema bora tukose wanaotutibu kuliko tuwe nao wanaotuua. Lakini nina uhakika ukitangaza kwamba watu waliowahi kuokolewa maisha yao kupitia mikono ya hawahawa "watuhumiwa" wajitokeze, nina uhakika idadi ya walioponywa itakuwa kubwa kuliko ya waliodhurika. Kumbe ni "uzuri wa ukakasi ndani kipande cha mti", na "chema hakikosi kasoro", huku ma-negativist wakisema "baniani mbaya kiatu chake dawa".

Nasemaje? Tumfukuze kwanza kicheche halafu tukarabati mlango wa banda la kuku uwe imara, ndipo tuanze kumgombeza mtunza kuku wetu kwa kosa la kuweka mlango mbovu bandani ulioruhusu kicheche kuingia. Tukianza kufukuzana na mtunza kuku, vicheche watazidi kuingia, kuku watatawanyika kwa woga, na huko nyikani ndio wataliwa na vicheche zaidi. Namaanisha hivi, hatua zielekezwe katika kurekebisha "MFUMO" uliosababisha hali hii, la sivyo tukiishia tu kutunga adhabu kwa madaktari, makosa yataendelea, wagonjwa watakosa kabisa imani, wataishia kutibiwa mitaani ambako wanaweza kupata matibabu duni zaidi na likawa janga kubwa zaidi. Sisemi hao jamaa waachiwe free ride, no way, lakini isiwe hatua pekee.

Narudia masikitiko yangu, si kawaida yangu kupost hapa response ndefu hivi, lakini hili jambo limeniumiza sana. Mungu awajalie wagonjwa uzima, Amina.
 
Thats what we call a https://jamii.app/JFUserGuide up in our goverment hospital...were this Doctors Druck..or in Drugs..am traying to understand them in possive way i cant...how can this be..inamaa hakuna muongozo wa uchunguzi uliofanyika kabla ya wao kuja kufanya operasheni?Poor wagonjwa.

pinguza jaziba na edit hiyo post yako mkuu buswelu
 
I am very sorry for the concerned patient, I hope they will recover. Errors do occur sometimes unintentionally. No doctor worth his profession would like to make a wrong diagnosis, but in this case I think MOI and the surgeon society should review, if they exist,procedures that has to be followed by doctors before performing an operation. It looks like the concerned doctors had no prior contact with the patients. I was once operated in a hospital abroad the doctor asked my name and explained to me what she was going to perform before I was put into half kaput. Surely if it was not my name and the wrong operation I would have protested. The Tanzania Surgical Association should take the professionl responsibility to ensure that proper theater norms are available in print to all surgeons.
 
Na jana imetangazwa kuwa Emanuel didas ( aliyepasuliwa mguu badala ya kichwa than last monday akapasuliwa kichwa) ameaga dunia. Sijui tuseme ni mapenzi ya Mungu?
Tunasubiri kwa hau ripoti itakayotolewa na prof mwakyusa
 
Kuna makosa mengi sana tu yanafanyika kuna wamama wanafanyiwa operation kuwa wana uvimbe tumboni halafu hakuna kitu.Na siku hizi udaktari siyo wito kabisa yaani watu waenda kusomea udaktari wakiwa hawana kabisa moyo wa kusaidia na matokeo ndiyo haya
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom