Madaktari Waukata Mguu wa Kushoto Badala ya Mguu wa Kulia | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Madaktari Waukata Mguu wa Kushoto Badala ya Mguu wa Kulia

Discussion in 'JF Doctor' started by Gudboy, Jan 28, 2010.

 1. Gudboy

  Gudboy JF-Expert Member

  #1
  Jan 28, 2010
  Joined: Aug 14, 2009
  Messages: 799
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 33
  Madaktari nchini Peru bila kutarajia waliukata mguu wenye afya badala ya mguu uliotakiwa kukatwa wenye maambukizi na walipogundua kosa lao waliumalizia kuukata mguu uliobaki hivyo kumwacha mgonjwa akiwa amepoteza miguu yake yote miwili.</SPAN>
  Madaktari nchini Peru walijichanganya na kuukata mguu wa kushoto wa mwanaume mwenye umri wa miaka 86 badala ya kuukata mguu wake wa kulia ambao ulikuwa na maambukizi.

  Mwanaume huyo alitakiwa kukatwa mguu wake wa kulia ili kuzuia maambukizi katika mguu wake kusambaa mwilini mwake.

  "Nilishtuka sana niliponyanyua shuka na kuona madaktari wameukata mguu wake wa kushoto badala ya mguu wa kulia", alisema binti wa mwanaume huyo, Carmen Villanueva.

  Carmen alisema kuwa madaktari katika mji wa Callao walikuwa wakimpatia matibabu baba yake tangia januri 4 mwaka huu kutokana na maambukizi aliyokuwa nayo katika mguu wake wa kulia.

  Baada ya hali yake kuwa mbaya sana siku ya jumamosi, waliamua kufanya operesheni ya dharura kuukata mguu huo ili kuzuia maambukizi kusambaa mwilini mwake.

  Baada ya kugundua makosa yao, madaktari waliamua kumfanyia operesheni nyingine mwanaume huyo siku iliyofuatia na kuukata mguu wake wa kulia uliotakikana kukatwa tangia awali na kumwacha mwanaume huyo akiwa amepoteza miguu yake yote miwili bila kutegemea.

  Hospitali ya Sabogal Hospital ilisema imewasimamisha kazi kwa muda madaktari waliofanya operesheni hizo huku uchunguzi wa tukio hilo ukiendelea.

  Waziri wa afya wa Peru, Oscar Ugarte alithibitisha tukio hilo na kusema "Bila shaka wanastahili kuadhibiwa.. ni tukio la kusikitisha na tumeanzisha uchunguzi".

  Familia ya mwanaume huyo imepanga kufungua
  kesi mahakamani kuwashataki madaktari hao.
  </SPAN>
  Source: Nifahamishe.com
   
 2. Lekanjobe Kubinika

  Lekanjobe Kubinika JF-Expert Member

  #2
  Jan 28, 2010
  Joined: Dec 6, 2006
  Messages: 3,067
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 135
  Duuuu! Nilifikiri mambo haya yanatokea hospitali ya Moi tu!!!!!!

  Leka
   
 3. elimumali

  elimumali Senior Member

  #3
  Jan 29, 2010
  Joined: Jan 13, 2010
  Messages: 149
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35
  Namuombea afueni mgonjwa huyu, Mwenyezi Mungu afanye miujiza yake amponye, ampunguzie maumivu na hapo baadaye apate miguu ya bandia imsaidie. Namuombea maisha marefu AMEN.

  Wahusika wa makosa hasa wanastahili adhabu KALI itakayokumbukwa na dunia nzima, ili iwe fundisho kwa wanadamu wote wazembe.
   
 4. Mahai

  Mahai JF-Expert Member

  #4
  Jan 29, 2010
  Joined: Jan 14, 2010
  Messages: 351
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 35
  I am speechless. Hao madaktari wasisimamishwe kazi kwa muda, wanyang'anywe na leseni wasiwe madaktari tena katika maisha yao yote na huyo baba Mungu ampe moyo wa ujasiri wa kukabiliana na unexpected disability aliyopewa na hao madaktari.
   
Loading...