Madaktari watimuliwa | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Madaktari watimuliwa

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by BAK, Nov 20, 2007.

 1. BAK

  BAK JF-Expert Member

  #1
  Nov 20, 2007
  Joined: Feb 11, 2007
  Messages: 70,461
  Likes Received: 81,711
  Trophy Points: 280
  Madaktari watimuliwa
  SAKATA LA MOI

  na Lucy Ngowi
  Tanzania daima

  SAKATA la upasuaji tata katika Taasisi ya Mifupa na Tiba Muhimbili (MOI), limechukua sura mpya baada ya mgonjwa aliyefanyiwa upasuaji wa mguu badala ya kichwa, kufanyiwa upasuaji mwingine jana na madaktari wawili zaidi kusimamishwa kazi.
  Chanzo chetu cha habari kimeeleza kuwa upasuaji wa pili wa Emmanuel Mgaya, sasa wa kichwa, ulianza saa nne asubuhi jana na hadi saa 10 alasiri, alikuwa bado yupo katika chumba cha upasuaji.

  Novemba mosi, mwaka huu, Mgaya alifanyiwa upasuaji wa mguu badala ya kichwa na Emmanuel Didas, aliyekuwa afanyiwe upasuaji wa kichwa, alifanyiwa wa mguu.

  Katika hatua nyingine, chanzo chetu cha habari kilieleza kuwa madaktari wengine wawili wamesimamishwa kazi na kufanya idadi ya madaktari waliosimamishwa kazi kuhusiana na sakata hilo kufikia wanne.

  Kwa mujibu ya chanzo hicho, madaktari hao (majina tunayo), wamesimamishwa kazi kutokana na kumwingiza Didas kinyemela kwenye chumba cha upasuaji, bila kulipia.

  “Madaktari hawa wawili wamesimamishwa kazi kutokana na kumwingiza kinyemela kwenye chumba cha upasuaji, mgonjwa aliyekuwa afanyiwe upasuaji wa mguu, lakini akafanyiwa upasuaji wa kichwa. Inasemekana mgonjwa huyo alikuwa hajalipia, hivyo wakati wakifanya ujanja huo wakabadilisha vyumba vya wagonjwa,” kilieleza chanzo chetu cha habari.

  Chanzo hicho cha habari kimeeleza kuwa kunatarajiwa kufanyika mabadiliko makubwa ya uongozi katika taasisi hiyo, hasa katika kitengo cha upasuaji, kabla ya Desemba 4, mwaka huu.

  “Mabadiliko hayo yatafanywa na Mkurugenzi wa MOI, hivyo hatutakuwa na imani naye kwa kuwa tunasikia anawaweka watu alio karibu nao,” kilisema chanzo cha habari.

  Kwa mujibu wa chanzo hicho, wafanyakazi wa taasisi hiyo waliiomba serikali iunde tume huru katika suala la upasuaji tata, kwa kuwa tume iliyoundwa hawakuwa na imani nayo, bila mafanikio.

  “Tumeomba tume huru ili tueleze matatizo yetu, lakini serikali haikutaka kutusikiliza…tunasubiri matokeo…tupo tayari kuandamana kwa amani,” kilisema chanzo chetu.

  Chanzo kinasema hata matokeo yatakayotolewa na serikali ya upasuaji tata hayatakuwa na maana, na kusisitiza kuwa wao wanaomba tume huru katika tatizo hilo lililojitokeza kwa kuwa kuna mambo mengi yamefichika likiwamo la ubadhirifu wa fedha katika taasisi hiyo.

  Chanzo hicho kimesema kuwa kuna taarifa kuwa Baraza la Madaktari limeshauriwa na tume iliyoundwa kuangalia adhabu ya kuwapa madaktari waliohusishwa katika tukio hilo, pia kuangalia suala la vyumba vya upasuaji kwa maelezo kuwa ni vidogo.

  Katika sakata hilo, uongozi wa juu wa taasisi hiyo umehusishwa katika sakata hilo lililotokea Novemba mosi, mwaka huu, na kutakiwa kujiuzulu ili kuimarisha huduma zilizozorota katika taasisi hiyo.

  Ilielezwa kuwa taasisi hiyo imegawanyika na kuwa na makundi mawili yaliyosababishwa na uongozi wa juu kwa kutoa upendeleo wa vyeo hata kwa wale wasiostahili. Hata hivyo, jambo hilo limekanushwa na madaktari wa taasisi hiyo, baada ya kikao cha dharura kuitishwa katika taasisi hiyo.
   
 2. Maarifa

  Maarifa JF-Expert Member

  #2
  Nov 21, 2007
  Joined: Nov 23, 2006
  Messages: 2,880
  Likes Received: 1,049
  Trophy Points: 280
  Ni lini umesikia Tanzania mtu anajiuzulu kwa kuwa accountable? Hilo halipo Ubabaishaji na rushwa kila pahala. Jamani mpaka kufukia kuwabomoa watu vichwa kisa matatizo ya kazi ni unaccpetable. Ni kwa nini wasimamishwe? was expecting wawe kwa pilato.
   
Loading...