Madaktari wasema Zitto alisumbuliwa na kuchafuka tumbo

Na ni gazeti la RA -- Mtanzania -- tu ndilo linalopiga debe kwa nguvu kwamba alitiliwa sumu! Hivi anafikiri Watz wote bado mambumbumbu?

wacha urongo kasome na 'Tanzania Daima B' mwananchi
 
Mhhh ama kweli kitu usichokijua ni kama usiku wa giza. Kwa mwandishi neno FOOD POISON ni SUMU NDANI YA CHAKULA. Ni kweli kuwa ni sumu, lakini mwandishi alichotakiwa kujua ni aina gani ya sumu, Imeingiaje ndani ya chakula??? Nafikiri kama angalikuwa ni INVESTIGATIVE JOURNALIST angemuuliza daktari alomtibu Zitto, kama issue ni sumu ndani ya chakula Je mmeripoti ofisi ya Mkemia mkuu ili kujua ni aina gani ya sumu???. Hapo nafikiri Dr Angemwelewesha kuwa ni sumu inayotokana na wadudu (Microbes) aweza kuwa Bacteria au Virus, baada ya ku-contaminate chakula ana achia traces za enzymes ndani ya chakula hicho, na mtu akila hicho chakula hizo enzymes toka kwa microbes husababisha mlaji kuumwa tumbo, kichwa, na huanza kuharisha na pia kutapika. Mnaweza mkala watu wengi chakula hicho lakini si lazima wote waliokula chakula hicho wapate matatizo hayo. Hii inatokana na watu kuwa na viwango tofauti vya kinga mwilini dhidi ya aina hiyo ya sumu au poison. Ni yule tu mwenye kinga dhaifu ndio hu-react haraka saana. Mfano mzuri wote twawaona vichaa wakila majalalani au wale wazoa taka wakila ndizi huku wakizoa taka, lakkini husikii wakilazwa kama Mheshimiwa ZK. Kikubwa hapa Zitto asifikirie kuwa kuna watu wanataka kumuua, la hasha, yeye kama Muislamu nafikiri anaelewa fika kuwa ni ALLAH pekee mwenye uwezo wa kumwondoa mja siku na wakati wowote ule alioupanga. ZK ajue kuwa yeye si wa kwanza kuumwa food poison, watu wanaugua kila siku je nao wamewekewa sumu???
 
Na waandishi wetu Fredy Azzah na Fidelis Butahe
MBUNGE wa Kigoma Kaskazini, Zitto Kabwe ambaye jana aliruhusiwa kutoka katika Hospitali ya Aga Khan ya jijini Dar es Salaam alikolazwa kwa matibabu ya tumbo amedai kuwa matatizo hayo aliyapata baada ya kula chakula chenye sumu."Namshukuru Mungu naendelea vizuri na nimesharuhusiwa kutoka hospitali, madaktari wameniambia ilikuwa food poisoning (chakula chenye sumu)," alisema Zitto.

Zitto ambaye hakuweza kueleza chakula hicho alikuwa wapi na kina sumu ya aina gani, alisema kuwa baada ya kugundua tatizo hilo, madaktari walimtaka kuwa makini na vyakula anavyokula.

"Sumu gani nimekula na ni wapi, mimi nadhani sio story (habari). Cha msingi kwa sasa naendelea vizuri na nimetakiwa kuwa makini na vyakula ninavyokula," alisema Zitto.

Hata hivyo, kauli hiyo ya Zitto inapingana na madaktari wake waliosema kuwa mbunge huyo kupitia tiketi ya Chadema, alikuwa anasumbuliwa na mchafuko wa kawaida wa tumbo.

"Alikuwa anasumbuliwa na Gastro enteritis (mchafuko wa tumbo), tatizo hili linaweza kusababishwa na bacteria, virusi katika chakula, au kama chakula hakijapikwa vizuri," alisema Dk Mustafa Bapumia.

Zitto alilazwa hospitalini hapo tangu Disemba 9 mwaka huu saa 3:00 usiku, baada ya kutoka kwenye mkutano wa ndani wa chama chake uliofanyika Bagamoyo mkoani Pwani ambako alivuliwa cheo cha Naibu Kiongozi wa Kambi ya upinzani bungeni.

Kuhusu hatua ya chama hicho kumvua Zitto wadhifa wake wa unaibu kiongozi wa upinzani bungeni, alisema kwa sasa bado hawezi kuzungumzia suala hilo kwa sababu hajapata taarifa rasmi kutoka chama chake mbali na kusoma suala hilo kwenye vyombo vya habari.

Hata hivyo, alieleza hakuwahi kuomba kupewa wadhifa huo, kwa hiyo endapo watu waliomwona anafaa kufanya kazi na kumpa wadhifa huo, wakiamua kumnyang'anya siyo tatizo kubwa kwake.

"Kwa sasa nadhani suala la afya yangu ndiyo muhimu zaidi. Ngoja kwanza nitoke hapa na afya yangu iimarike na kama kutakuwa kuna sababu ya mimi kuzungumza nitazungumza," alisema Zitto:

"Lakini ikumbukwe kuwa mimi sikuwahi kuomba wadhifa huu…, kwa hiyo kama watu walionipa wameamua kunibadilishia, mimi sidhani kama kuna tatizo."

Mwenyekiti wa chama hicho, Freeman Mbowe aliupolizwa na Mwananchi Jumapili juu ya Zitto kuvuliwa uongozi bungeni alisema kuwa chama kitatoa taarifa baadaye.

Source : Mwananchi
 
Mhhh ama kweli kitu usichokijua ni kama usiku wa giza. Kwa mwandishi neno FOOD POISON ni SUMU NDANI YA CHAKULA. Ni kweli kuwa ni sumu, lakini mwandishi alichotakiwa kujua ni aina gani ya sumu, Imeingiaje ndani ya chakula??? Nafikiri kama angalikuwa ni INVESTIGATIVE JOURNALIST angemuuliza daktari alomtubu Zitto, kama issue ni sumu ndani ya chakula Je mmelipoti ofisi ya Mkemia mkuu ili kujua ni aina gani ya sumu???. Hapo nafikiri Dr Angemwelewesha kuwa ni sumu inayotokana na wadudu (Microbes) aweza kuwa Bacteria au Virus, baada ya ku-contaminate chakula ana achia traces za enzymes ndani ya chakula hicho, na mtu akila hicho chakula hizo enzymes toka kwa microbes husababisha mlaji kuumwa tumbo, kichwa, na huanza kuharisha na pia kutapika. Mnaweza mkala watu wengi chakula hicho lakini si lazima wote waliokula chakula hicho wapate matatizo hayo. Hii inatokana na watu kuwa na viwango tofauti vya kinga mwilini dhidi ya aina hiyo ya sumu au poison. Ni yule tu mwenye kinga dhaifu ndio hu-react haraka saana. Mfano mzuri wote twawaona vichaa wakila majalalani au wale wazoa taka wakila ndizi huku wakizoa taka, lakkini husikii wakilazwa kama Mheshimiwa ZK. Kikubwa hapa Zitto asifikirie kuwa kuna watu wanataka kumuua, la hasha, yeye kama Muislamu nafikiri anaelewa fika kuwa ni ALLAH pekee mwenye uwezo wa kumwondoa mja siku na wakati wowote ule alioupanga. ZK ajue kuwa yeye si wa kwanza kuumwa food poison, watu wanaugua kila siku je nao wamewekewa sumu???

Mzee unatumia busara kujadili mtu ambaye ana chembe ya busara. Tatizo la Zitto anataka kuingiza siasa kwenye sayansi, huyu mtu anataka kusikia kile anachotaka kusikia tuu. Mimi nadhani hapo nilipobold hapo juu ndio kwenye majibu. Unakumbuka ile kesi ya Nchimbi , Zitto na yule aliyekuwa mbunge machachari wa kike wa CCM (Amina Chifupa) . Nadhani tukianzia hapo tutapata majibu yote...
 
Hatudanganyiki !! CDM hawahangaiki na yeye pia maneno mengi yule kijana kama kapewa vipesa mahali basi vimemzingua anaogopa. CDM msimsikilize tuangalie shughuri za kulikomboa taifa
 
Hivi jameni, food poisoning ndio kulishwa sumu? Nasikia mheshimiwa alikuwa ana harisha sana. Pengine hii inatokana na kula chakula kichafu, magonjwa ya tumbo au hata kipindupindu. Ingekuwa kalishwa sumu matokeo yangekuwa mengine.
 
Alichosema ni food poisoning jana alipohojiwa na TBC. Na hii inaweza kusababishwa na mo's kama C. botulinum, E.coli na wengine wa aina hiyo kwenye chakula. May b aulizwe alikula wapi hiko chakula maana mostly wanapatikana kwenye vipolo ambavyo si well reheated
 
Na waandishi wetu Fredy Azzah na Fidelis Butahe
MBUNGE wa Kigoma Kaskazini, Zitto Kabwe ambaye jana aliruhusiwa kutoka katika Hospitali ya Aga Khan ya jijini Dar es Salaam alikolazwa kwa matibabu ya tumbo amedai kuwa matatizo hayo aliyapata baada ya kula chakula chenye sumu."Namshukuru Mungu naendelea vizuri na nimesharuhusiwa kutoka hospitali, madaktari wameniambia ilikuwa food poisoning (chakula chenye sumu)," alisema Zitto.

Zitto ambaye hakuweza kueleza chakula hicho alikuwa wapi na kina sumu ya aina gani, alisema kuwa baada ya kugundua tatizo hilo, madaktari walimtaka kuwa makini na vyakula anavyokula.

"Sumu gani nimekula na ni wapi, mimi nadhani sio story (habari). Cha msingi kwa sasa naendelea vizuri na nimetakiwa kuwa makini na vyakula ninavyokula," alisema Zitto.

Hata hivyo, kauli hiyo ya Zitto inapingana na madaktari wake waliosema kuwa mbunge huyo kupitia tiketi ya Chadema, alikuwa anasumbuliwa na mchafuko wa kawaida wa tumbo.

"Alikuwa anasumbuliwa na Gastro enteritis (mchafuko wa tumbo), tatizo hili linaweza kusababishwa na bacteria, virusi katika chakula, au kama chakula hakijapikwa vizuri," alisema Dk Mustafa Bapumia.

Zitto alilazwa hospitalini hapo tangu Disemba 9 mwaka huu saa 3:00 usiku, baada ya kutoka kwenye mkutano wa ndani wa chama chake uliofanyika Bagamoyo mkoani Pwani ambako alivuliwa cheo cha Naibu Kiongozi wa Kambi ya upinzani bungeni.

Kuhusu hatua ya chama hicho kumvua Zitto wadhifa wake wa unaibu kiongozi wa upinzani bungeni, alisema kwa sasa bado hawezi kuzungumzia suala hilo kwa sababu hajapata taarifa rasmi kutoka chama chake mbali na kusoma suala hilo kwenye vyombo vya habari.

Hata hivyo, alieleza hakuwahi kuomba kupewa wadhifa huo, kwa hiyo endapo watu waliomwona anafaa kufanya kazi na kumpa wadhifa huo, wakiamua kumnyang'anya siyo tatizo kubwa kwake.

"Kwa sasa nadhani suala la afya yangu ndiyo muhimu zaidi. Ngoja kwanza nitoke hapa na afya yangu iimarike na kama kutakuwa kuna sababu ya mimi kuzungumza nitazungumza," alisema Zitto:

"Lakini ikumbukwe kuwa mimi sikuwahi kuomba wadhifa huu…, kwa hiyo kama watu walionipa wameamua kunibadilishia, mimi sidhani kama kuna tatizo."

Mwenyekiti wa chama hicho, Freeman Mbowe aliupolizwa na Mwananchi Jumapili juu ya Zitto kuvuliwa uongozi bungeni alisema kuwa chama kitatoa taarifa baadaye.

Source : Mwananchi

Waandishi wetu nao!!!??? Food poisoning si lazima uwe umewekewa sumu.

Waende SUA au TFD wakatafute maana ya food poisoning ndo waje waandike.

Pia huku kwenye mahoteli muwe mnakuwa makini na vyakula vyao. vingine havihifadhiwi vizuri hivyo vinaathiriwa na bacteria na fungus.
 
Akawaulize akina RA wanaomfadhili kukivuruga CDM. Mods toa hii, inarudiwarudiwa tu.
 
"Sumu gani nimekula na ni wapi, mimi nadhani sio story (habari). Cha msingi kwa sasa naendelea vizuri na nimetakiwa kuwa makini na vyakula ninavyokula," alisema Zitto.???????????????

Hata hivyo, kauli hiyo ya Zitto inapingana na madaktari wake waliosema kuwa mbunge huyo kupitia tiketi ya Chadema, alikuwa anasumbuliwa na mchafuko wa kawaida wa tumbo.??????????????

"Alikuwa anasumbuliwa na Gastro enteritis (mchafuko wa tumbo), tatizo hili linaweza kusababishwa na bacteria, virusi katika chakula, au kama chakula hakijapikwa vizuri," alisema Dk Mustafa Bapumia!!

Hii habari inaonekana kuwa ya kuunga unga ambapo mgonjwa tayari anatuhumu kula sumu halafu hawezi kusema kala hiyo sumu wapi? Hapa kuna witch hunting!

sikumsikia lakini kama alitumia neno 'food poison' hakumaanisha ametegwa sumu, hiyo kitu inajitengenezaga baada ya msosi kukaa muda mrefu au kama msosi umeanza kuharibika, hutokea naturally, ni njia Mungu anatumia kuwafanya watu wale msosi fresh :)
 
Food Poisoning
n.
  1. An acute, often severe gastrointestinal disorder characterized by vomiting and diarrhea and caused by eating food contaminated with bacteria, especially bacteria of the genus Salmonella, or the toxins they produce.
  2. Poisoning caused by ingesting substances, such as certain mushrooms, that contain natural toxins.
 
Mambo ya KPR, sikujua kijana anapenda kuchakachua KPR, yawezekana ilikuwa kwenye breakfast yake alipokuwa akijipendelea KPR na chai... Tunamtakia Afya Njema....

HOJA yangu ni hii, kuumwa aumwe Profesa akiwa kijiweni akiumwa mwanasiasa ni dili tayari... Hata kama ni ugonjwa wa kawaida linaweza kutumika kujipatia au kujijengea maslahi binafsi au ya wengine... wanasiasa hawaaminiki ... wakati mwingine umaarufu ukipungua wanaweza hata kujilaza ICU kugain simpathy... simaanishi mheshimiwa amefanya hivyo la ila namaanisha tujue tu kila hoja inabidi umakini sio kuhisi
 
Inabidi awe wazi kueleza nani kamlisha hiyo sumu...ni Jack Zoka naibumkurugenzi wa UwT? Maana wanaweza kumlisha sumu ili asitoe siri za vikao vyao vya jinsi ya kuiua CHADEMA. Lakini pia inawezekana UWT wamemwambia aseme hivyo ili ionekane chadema ndio wamemfanyia hivyo...maana zito haaminiki kama aliweza kuongelea udini kwa maelekezo ya UWT hawezi kusita kuzua tena alimradi tu wamuahidi pesa nzuri.

Naye huyu mnaona ni mali si aende tu akawachukue watoto wake aliowatelekeza kule Chitungwiza. Jamaaa ni loafer moja tu sawa na Mwizi.
 
Food poisoning kwa mtu mmoja tu? Je chakula kilipikwa cha Zito pekee? Mmmmmm! tuombe mungu chedema tusianze kujimaliza.
 
Hawa waandishi wetu feki sana...tangu lini Food Poisoning ni LAZIMA mtu uwe UMEKULA chakula chenye sumu??
Food poisoning au kitaalam "Gatro Enteritis" ni hali inayowatokea watu wengi wanapokula kitu chenye contamination.Sidhani kuna binadamu ambaye katika maisha yake hajawahi kupatwa na hali hii. Najaribu kuwaza, endapo watu wote wangekuwa na fikra za kuuawa kwa kutiliwa sumu basi tungeshashtakiana majumbani humo, migahawani, maofisini n.k maana mara nyingi hali hii hutokea baada ya kula chakula.

Ni upotofu kukimbilia kutoa tafsiri ya kutaka kulishwa sumu wakati " sumu" unaila mwenyewe kwenye chakula chako. "Food poisoning" ni terminology inayotumika kwe wepesi kuelezea kisichokubalika tumboni na hivyo kutolewa kwa ama kutapika au kuharisha.
 
Back
Top Bottom