Madaktari wasema Zitto alisumbuliwa na kuchafuka tumbo

Rutashubanyuma

JF-Expert Member
Sep 24, 2010
214,583
2,000
Zitto adai amelishwa sumu Saturday, 11 December 2010 21:04

zitto%20kabwe%20hoi.jpg
Fredy Azzah na Fidelis Butahe
MBUNGE wa Kigoma Kaskazini, Zitto Kabwe ambaye jana aliruhusiwa kutoka katika Hospitali ya Aga Khan ya jijini Dar es Salaam alikolazwa kwa matibabu ya tumbo amedai kuwa matatizo hayo aliyapata baada ya kula chakula chenye sumu.

“Namshukuru Mungu naendelea vizuri na nimesharuhusiwa kutoka hospitali, madaktari wameniambia ilikuwa food poisoning (chakula chenye sumu),” alisema Zitto.

Zitto ambaye hakuweza kueleza chakula hicho alikuwa wapi na kina sumu ya aina gani, alisema kuwa baada ya kugundua tatizo hilo, madaktari walimtaka kuwa makini na vyakula anavyokula.

“Sumu gani nimekula na ni wapi, mimi nadhani sio story (habari). Cha msingi kwa sasa naendelea vizuri na nimetakiwa kuwa makini na vyakula ninavyokula,” alisema Zitto.

Hata hivyo, kauli hiyo ya Zitto inapingana na madaktari wake waliosema kuwa mbunge huyo kupitia tiketi ya Chadema, alikuwa anasumbuliwa na mchafuko wa kawaida wa tumbo.

“Alikuwa anasumbuliwa na Gastro enteritis (mchafuko wa tumbo), tatizo hili linaweza kusababishwa na bacteria, virusi katika chakula, au kama chakula hakijapikwa vizuri,” alisema Dk Mustafa Bapumia.

Zitto alilazwa hospitalini hapo tangu Disemba 9 mwaka huu saa 3:00 usiku, baada ya kutoka kwenye mkutano wa ndani wa chama chake uliofanyika Bagamoyo mkoani Pwani ambako alivuliwa cheo cha Naibu Kiongozi wa Kambi ya upinzani bungeni.

Kuhusu hatua ya chama hicho kumvua Zitto wadhifa wake wa unaibu kiongozi wa upinzani bungeni, alisema kwa sasa bado hawezi kuzungumzia suala hilo kwa sababu hajapata taarifa rasmi kutoka chama chake mbali na kusoma suala hilo kwenye vyombo vya habari.

Hata hivyo, alieleza hakuwahi kuomba kupewa wadhifa huo, kwa hiyo endapo watu waliomwona anafaa kufanya kazi na kumpa wadhifa huo, wakiamua kumnyang’anya siyo tatizo kubwa kwake.

“Kwa sasa nadhani suala la afya yangu ndiyo muhimu zaidi. Ngoja kwanza nitoke hapa na afya yangu iimarike na kama kutakuwa kuna sababu ya mimi kuzungumza nitazungumza,” alisema Zitto:

“Lakini ikumbukwe kuwa mimi sikuwahi kuomba wadhifa huu…, kwa hiyo kama watu walionipa wameamua kunibadilishia, mimi sidhani kama kuna tatizo.”

Mwenyekiti wa chama hicho, Freeman Mbowe aliupolizwa na Mwananchi Jumapili juu ya Zitto kuvuliwa uongozi bungeni alisema kuwa chama kitatoa taarifa baadaye.

Katika hatua nyingine Mbunge wa Mpanda Mjini, Said Amur Arfi aliyekuwa amelazwa katika Hospitali ya Aga Khan ya jijini Dar es Salaam, amesafirishwa kwenda India kwa matibabu zaidi.

Arfi aliliambia Mwananchi Jumapili kuwa madaktari waliokuwa wakimtibu wamemwambia kuwa mfuko wake wa nyongo una mawe hivyo anahitaji kufanyiwa upasuaji.

“Nilikuja hapa kwa sababu nilikuwa nasumbuliwa na maumivu makali ya tumbo, nilitoka Mpanda Disemba 2, mwaka huu kuja kwenye semina lakini kutokana na maumivu ya tumbo nilienda Hospitali ya Regency na baada ya kupigwa ultrasound nilielezwa kuwa nina tatizo la uvimbe kwenye maini,” alisema Arfi.

Alisema alivyokwenda katika Hospitali ya Aga Khan alielezwa kuwa ana tatizo jingine la mawe kwenye mfuko wa nyongo na kuwa inabidi afanyiwe upasuaji.

“Naishukuru serikali kupitia ofisi ya Bunge kunipeleka India kwa matitabu zaidi,” alisema Arfi.

Hata hivyo, alisema bado hajaelezwa hospitali anayokwenda kutibiwa na kuwa, taarifa zote hizo anazo muuguzi wa serikali atakayesafiri naye.
Wakati huohuo, Mtangazaji wa Televisheni ya Channel Ten, Cyprian Musiba, anadaiwa kuwekewa sumu kwenye chakula na kufanya alazwe hospitalini kwa matibabu.

Musiba alilazwa katika kituo cha Afya cha Ebrahim Haji kilichopo jijini Dar es Salaam juzi mchana akiwa hajitambui.

Mmoja wa madaktari wa hospitali hiyo, Dk Ramadhani Ali aliliambia Mwananchi Jumapili kuwa Musiba alifikishwa katika hospitali hiyo akiwa anasumbuliwa na tumbo lakini, baada ya kupata matibabu, afya yake iliimarika na jana mchana aliruhusiwa kutoka hospitalini.

“Anaendelea vizuri kwa kweli na amesharuhusiwa” alisema Dk Ali huku akisita kueleza tatizo la lililokuwa linamsumbua Musiba.

Mke wa Musiba ambaye hakujitambulisha alisema kuwa kabla ya Musiba kuruhusiwa mmoja wa madaktari wa HospitaliI hiyo waliwaeleza kuwa Musiba alikula sumu iliyokuwa katika chakula.

“Tumeruhusiwa muda si mrefu ila daktari amesema Musiba alijisikia vibaya kwa kuwa alikuwa amekula sumu iliyokuwa katika chakula,”alisema mke wa Musiba.

Musiba ambaye mara nyingi hutangaza habari za michezo na burudani aliliambia Mwananchi Jumapili kuwa juzi hali yake ilikuwa mbaya na kuongeza kuwa alipelekwa katika hospitali hiyo kwa ajili ya matibabu.

“Hali yangu ilikuwa mbaya sana nilikuwa wa kufa tu ndugu yangu, ila namshukuru mungu naendelea vizuri, ila daktari hapa hospitali amenieleza kuwa nilikula sum,” alisema Musiba.

Habari zaidi zilidai kuwa Musiba alianza kupata matatizo ya tumbo saa kadhaa baada ya kula chakula katika hoteli moja iliyopo karibu na ofisi za Channel Ten.
 
Rutashubanyuma

JF-Expert Member
Sep 24, 2010
214,583
2,000
Fredy Azzah na Fidelis Butahe
MBUNGE wa Kigoma Kaskazini, Zitto Kabwe ambaye jana aliruhusiwa kutoka katika Hospitali ya Aga Khan ya jijini Dar es Salaam alikolazwa kwa matibabu ya tumbo amedai kuwa matatizo hayo aliyapata baada ya kula chakula chenye sumu.

"Namshukuru Mungu naendelea vizuri na nimesharuhusiwa kutoka hospitali, madaktari wameniambia ilikuwa food poisoning (chakula chenye sumu)," alisema Zitto.

Tatizo la madai haya mapya ya Zitto ni kuwa miezi kadhaa iliyopita aliwahi kulazwa Hospitali ya Dodoma na baadaye kupelekwa nje kwa matibabu hayo hayo ya tumbo.........................sasa ataka tuamini ya kuwa kila mara yeye ni mwathirika wa botulism?

I have my theories on the ensuing conspiracies but I will reserve and defer my considerate analysis on Kabwe's excruciating predicaments until some other appropriate day.............................
 
rmb

JF-Expert Member
Nov 1, 2010
223
195
Zitto adai amelishwa sumu Send to a friend Saturday, 11 December 2010 21:05 0diggsdigg

Fredy Azzah na Fidelis Butahe
MBUNGE wa Kigoma Kaskazini, Zitto Kabwe ambaye jana aliruhusiwa kutoka katika Hospitali ya Aga Khan ya jijini Dar es Salaam alikolazwa kwa matibabu ya tumbo amedai kuwa matatizo hayo aliyapata baada ya kula chakula chenye sumu."Namshukuru Mungu naendelea vizuri na nimesharuhusiwa kutoka hospitali, madaktari wameniambia ilikuwa food poisoning (chakula chenye sumu)," alisema Zitto.

Zitto ambaye hakuweza kueleza chakula hicho alikuwa wapi na kina sumu ya aina gani, alisema kuwa baada ya kugundua tatizo hilo, madaktari walimtaka kuwa makini na vyakula anavyokula.

"Sumu gani nimekula na ni wapi, mimi nadhani sio story (habari). Cha msingi kwa sasa naendelea vizuri na nimetakiwa kuwa makini na vyakula ninavyokula," alisema Zitto.

Hata hivyo, kauli hiyo ya Zitto inapingana na madaktari wake waliosema kuwa mbunge huyo kupitia tiketi ya Chadema, alikuwa anasumbuliwa na mchafuko wa kawaida wa tumbo.

"Alikuwa anasumbuliwa na Gastro enteritis (mchafuko wa tumbo), tatizo hili linaweza kusababishwa na bacteria, virusi katika chakula, au kama chakula hakijapikwa vizuri," alisema Dk Mustafa Bapumia.

Zitto alilazwa hospitalini hapo tangu Disemba 9 mwaka huu saa 3:00 usiku, baada ya kutoka kwenye mkutano wa ndani wa chama chake uliofanyika Bagamoyo mkoani Pwani ambako alivuliwa cheo cha Naibu Kiongozi wa Kambi ya upinzani bungeni.

Kuhusu hatua ya chama hicho kumvua Zitto wadhifa wake wa unaibu kiongozi wa upinzani bungeni, alisema kwa sasa bado hawezi kuzungumzia suala hilo kwa sababu hajapata taarifa rasmi kutoka chama chake mbali na kusoma suala hilo kwenye vyombo vya habari.

Hata hivyo, alieleza hakuwahi kuomba kupewa wadhifa huo, kwa hiyo endapo watu waliomwona anafaa kufanya kazi na kumpa wadhifa huo, wakiamua kumnyang'anya siyo tatizo kubwa kwake.

"Kwa sasa nadhani suala la afya yangu ndiyo muhimu zaidi. Ngoja kwanza nitoke hapa na afya yangu iimarike na kama kutakuwa kuna sababu ya mimi kuzungumza nitazungumza," alisema Zitto:

"Lakini ikumbukwe kuwa mimi sikuwahi kuomba wadhifa huu…, kwa hiyo kama watu walionipa wameamua kunibadilishia, mimi sidhani kama kuna tatizo."

Mwenyekiti wa chama hicho, Freeman Mbowe aliupolizwa na Mwananchi Jumapili juu ya Zitto kuvuliwa uongozi bungeni alisema kuwa chama kitatoa taarifa baadaye.

Katika hatua nyingine Mbunge wa Mpanda Mjini, Said Amur Arfi aliyekuwa amelazwa katika Hospitali ya Aga Khan ya jijini Dar es Salaam, amesafirishwa kwenda India kwa matibabu zaidi.

Arfi aliliambia Mwananchi Jumapili kuwa madaktari waliokuwa wakimtibu wamemwambia kuwa mfuko wake wa nyongo una mawe hivyo anahitaji kufanyiwa upasuaji.

"Nilikuja hapa kwa sababu nilikuwa nasumbuliwa na maumivu makali ya tumbo, nilitoka Mpanda Disemba 2, mwaka huu kuja kwenye semina lakini kutokana na maumivu ya tumbo nilienda Hospitali ya Regency na baada ya kupigwa ultrasound nilielezwa kuwa nina tatizo la uvimbe kwenye maini," alisema Arfi.

Alisema alivyokwenda katika Hospitali ya Aga Khan alielezwa kuwa ana tatizo jingine la mawe kwenye mfuko wa nyongo na kuwa inabidi afanyiwe upasuaji.

"Naishukuru serikali kupitia ofisi ya Bunge kunipeleka India kwa matitabu zaidi," alisema Arfi.

Hata hivyo, alisema bado hajaelezwa hospitali anayokwenda kutibiwa na kuwa, taarifa zote hizo anazo muuguzi wa serikali atakayesafiri naye.
Wakati huohuo, Mtangazaji wa Televisheni ya Channel Ten, Cyprian Musiba, anadaiwa kuwekewa sumu kwenye chakula na kufanya alazwe hospitalini kwa matibabu.

Musiba alilazwa katika kituo cha Afya cha Ebrahim Haji kilichopo jijini Dar es Salaam juzi mchana akiwa hajitambui.

Mmoja wa madaktari wa hospitali hiyo, Dk Ramadhani Ali aliliambia Mwananchi Jumapili kuwa Musiba alifikishwa katika hospitali hiyo akiwa anasumbuliwa na tumbo lakini, baada ya kupata matibabu, afya yake iliimarika na jana mchana aliruhusiwa kutoka hospitalini.

"Anaendelea vizuri kwa kweli na amesharuhusiwa" alisema Dk Ali huku akisita kueleza tatizo la lililokuwa linamsumbua Musiba.

Mke wa Musiba ambaye hakujitambulisha alisema kuwa kabla ya Musiba kuruhusiwa mmoja wa madaktari wa HospitaliI hiyo waliwaeleza kuwa Musiba alikula sumu iliyokuwa katika chakula.

"Tumeruhusiwa muda si mrefu ila daktari amesema Musiba alijisikia vibaya kwa kuwa alikuwa amekula sumu iliyokuwa katika chakula,"alisema mke wa Musiba.

Musiba ambaye mara nyingi hutangaza habari za michezo na burudani aliliambia Mwananchi Jumapili kuwa juzi hali yake ilikuwa mbaya na kuongeza kuwa alipelekwa katika hospitali hiyo kwa ajili ya matibabu.

"Hali yangu ilikuwa mbaya sana nilikuwa wa kufa tu ndugu yangu, ila namshukuru mungu naendelea vizuri, ila daktari hapa hospitali amenieleza kuwa nilikula sum," alisema Musiba.

Habari zaidi zilidai kuwa Musiba alianza kupata matatizo ya tumbo saa kadhaa baada ya kula chakula katika hoteli moja iliyopo karibu na ofisi za Channel Ten

Source; Mwananchi

Hii habari ya Zitto mboka imekaa kama udaku jamani!
 
Gama

JF-Expert Member
Jan 9, 2010
12,528
2,000
Wana jf, nimesoma heading kuu ya gazeti la mwananchi inayosema kuwa zito amedai kuwa alipewa sumu huku chanzo hichohicho kikidai kuwa mbunge- arfi amekimbizwa india kwa matibabu. Sijaweza kusoma habari hii kwa undani, tafadhari mwenye habari kamili atujuze. Nawasilisha.
 
Mbogela

JF-Expert Member
Jan 28, 2008
1,378
1,250
shida mwandishi alipoambiwa food poison alidhani inamaanisha zitto alimaanisha amewekewa sumu kwenye chakula. Food poison ni sumu inayotokana na bacteria, alikula chakula kichafu kimsingi alichosema zitto na daktari wake havina utofauti.
 
Nsiande

JF-Expert Member
Jul 27, 2009
1,649
1,195
Muandishi wa habari wa TBC aliyeenda CDM kutafuta habari na kuzikosa kisha ku -roll eyes ! I think she needs a big uandishi ethics overhaul! I would have fired her on the spot..she didn't have to raise her voice with the mzee there! Get a grip girl!
 
rmb

JF-Expert Member
Nov 1, 2010
223
195
Nadhani aliamua kwa makusudi kabisa kupotosha kwa kuweka kichwa cha habari kisichoendana na habari! Gazeti kama Mwananchi nalo linataka kuwa halina tofauti na magazeti ya udaku? Tunaenda wapi?
 
Mzizi wa Mbuyu

JF-Expert Member
May 15, 2009
6,984
2,000
Inabidi awe wazi kueleza nani kamlisha hiyo sumu...ni Jack Zoka naibumkurugenzi wa UwT? Maana wanaweza kumlisha sumu ili asitoe siri za vikao vyao vya jinsi ya kuiua CHADEMA. Lakini pia inawezekana UWT wamemwambia aseme hivyo ili ionekane chadema ndio wamemfanyia hivyo...maana zito haaminiki kama aliweza kuongelea udini kwa maelekezo ya UWT hawezi kusita kuzua tena alimradi tu wamuahidi pesa nzuri.
 
Rutashubanyuma

JF-Expert Member
Sep 24, 2010
214,583
2,000
Zitto akalia kuti kavu
• Dk. Slaa ashangazwa na taarifa

na Bakari Kimwanga

amka2.gif
MBUNGE wa Kigoma Kaskazini na Naibu Katibu Mkuu wa CHADEMA, Zitto Kabwe, hivi sasa yuko katika wakati mgumu na huenda akavuliwa wadhifa wa Unaibu Katibu Mkuu.
Tanzania Daima Jumapili, limedokezwa kuwa kikao cha Kamati Kuu ambayo kilianza jana na kumalizika leo kinaweza kufikia uamuzi huo baada ya wabunge wa chama hicho juzi kuamua kumvua Zitto wadhifa wa Naibu Msemaji wa Kambi ya Upinzani Bungeni.
Wabunge hao walifikia uamuzi huo baada ya Zitto kutofautiana na msimamo wa chama chake ulioamua kususia hotuba ya Rais Kikwete, Novemba 17 alipokuwa akilihutubia Bunge na kulizindua Bunge hilo la 10.
Zitto, aliamua kuzungumza na vyombo vya habari namna alivyopinga hatua ya chama chake na mchakato mzima ulivyokwenda mpaka wakafikia uamuzi wa kususia hotuba hiyo ambapo wabunge wa chama hicho walitoka katika ukumbi wa Bunge wakati Rais Kikwete alipoanza kuhutubia.
Tanzania Daima Jumapili, limedokezwa kuwa baadhi ya wajumbe wa Kamati Kuu huenda wakapendekeza Zitto, ang'olewe kwenye wadhifa huo huku wakijenga hoja kuwa kiongozi huyo amekosa fursa ya kuaminiwa na wabunge wenzake kuwa Naibu Msemaji wa Kambi ya Upinzani Bungeni hivyo hana sifa pia ya kuwa Naibu Katibu Mkuu wa chama.
Hoja inayosimamiwa na baadhi ya wajumbe wa Kamati Kuu ni kuwa kama Zitto, ataendelea na wadhifa wa Naibu Katibu Mkuu kuna uwezekano wa kuibuka kutokuelewana na wabunge wenzake.
Chanzo hicho kimedokeza kuwa wajumbe hao wanaweza kujenga hoja kuwa kwa kuwa hakuaminika katika nafasi ya Nafasi ya Naibu Msemaji wa Kambi ya Upinzani basi haaminiki hata kuwa Naibu Katibu Mkuu.
"Nina imani kuwa Zitto, anaweza kujiuzulu kwa sababu wenzake wameonyesha kutokuwa na imani naye katika nafasi ya Naibu Kiongozi wa Kambi ya Upinzani Bungeni, sasa watakuja na hoja ya kutaka aondolewe na kwenye Nafasi ya Naibu Kati Mkuu," alidokeza mmoja wa wajumbe wa Kamti Kuu.
Juhudi za Tanzania Daima Jumapili, kumpata Zitto kuzungumzia sakata hilo ziligonga mwamba baada ya simu yake ya mkononi kuita bila kupokelewa.
Zitto, ambaye alilazwa katika Hospitali ya Agha Khan, siku tatu zilizopita akiugua ugonjwa wa homa ya matumbo, anaweza asihudhurie katika kikao cha leo kutokana na matatizo yanayomkabili.
Naye Mnadhimu Mkuu wa Kambi ya Upinzani Bungeni, Tundu Lissu, alipoulizwa kuhusu sakata hilo la Zitto, alisema hayuko tayari kulizungumzia kwa kuwa liko juu ya uwezo wake na kikao cha Kamati Kuu ndicho kitakachotoa msimamo wa kiongozi huyo.
Naye Katibu Mkuu wa CHADEMA, Dk. Willbrod Slaa, alisema suala hilo liko mikononi mwa wajumbe wa Kamati Kuu, hivyo hawezi kuingilia majukumu yasiyo yake.
Dk. Slaa, pia alisema kuwa anashangazwa na taarifa zinazodai kuwa Zitto alikula chakula chenye sumu kwenye mkutano wa wabunge wa CHADEMA uliofanyika Bagamoyo siku tatu zilizopita.
Alisema anayepaswa kueleza ugonjwa wa mtu ni dakatari anayemtibu na si chombo cha habari kilichotoa taarifa kuwa Zitto amelishwa sumu.
Dk. Slaa, alisema tangu kuanza kuugua kwa Zitto, mafisadi na wasioitakia mema CHADEMA wamekuwa na harakati za kueneza propaganda za kutaka kuivuruga lakini kamwe kusudio lao halitofanikiwa.
Alisema juzi akiwa ofisi alitumiwa ujumbe mfupi na Zitto, akimtaarifu kuumwa kichwa na baadaye kukimbizwa hospitali kwa mapumziko na kupatiwa matibabu zaidi.
"Unajua hivi sasa sisi tunajua nini kinachoendelea; maofisa Usalama wa Taifa kwa kushirikiana na mafisadi wamekuwa wakitumia mbinu mbalimbali kuisambaratisha CHADEMA kabla ya mwaka 2015, lakini kwa hili sisi tuko makini nalo na agenda ya kuendelea kuwatumikia Watanzania ndiyo tunayoishughulikia sasa na hata kama kuna matatizo huwa tunayamaliza kwa kupitia vikao vyetu kama leo tuko na wajumbe wa Kamati Kuu kwa dharura tukijadili hali ya chama chetu," alisema Dk. Slaa.
Aliongeza kuwa CHADEMA imekuwa ikiandamwa na mafisadi ambao wengine waliwataja kupitia mikutano ya hadhara katika viwanja vya Temeke, Mwembe Yanga, jijini Dar es Salaam.
Katibu mkuu huyo, alitoa wito kwa Watanzania kupuuza magazeti yanayotoa taarifa za uongo unaoenezwa na mafisadi ili kuwatoa Watanzania katika kujadili maslahi ya taifa lao na umaskini unaowakabili.
Hata hivyo alisema katika kujikinga na maovu hayo watapambana na wale mbao hawaitakii mema CHADEMA na kusisitiza kuwa huu ni wakati wa kazi na kuonyesha vitendo hasa kwa kupambana na uovu mbele ya macho ya Watanzania.
Alisema kinachofanyika hivi sasa ni kuipaka matope CHADEMA kwa kupakaziwa matope na kuonekana kuwa haifai mbele ya macho ya jamii kwa ujumla.
"Ndugu yangu hata siku moja usitegemee chombo cha habari ambacho mmiliki wake tulimlipua kwa ufisadi halafu wewe akakuandike vizuri; katu haliwezekani nasi tunajua nini huyo fisadi anachokifanya yeye pamoja na timu yake, CHADEMA iko shwari ila wanataka kutumia mbinu zao za kijasusi kuimaliza hapa hawawezi kabisa," alisema Dk. Slaa.
Katika kikao hicho cha dharura kilichoitishwa chini ya mwenyekiti wake Freeman Mbowe, kinajadili mambo mbalimbali yaliyotokea katika kipindi cha miezi miwili na kupata ufumbuzi wake.
 
Rutashubanyuma

JF-Expert Member
Sep 24, 2010
214,583
2,000
Dk. Slaa aanza mashambulizi
• Asema mafisadi wasubiri kiama chao

na Nuru Yanga

amka2.gif
KATIBU mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) Dk. Willbrod Slaa, amesema kuwapo kwake nje ya Bunge hakumfanyi aache kupambana na mafisadi na vitendo vya kifisadi.
Dk. Slaa, alisema mafisadi wanaodhani kutokuwapo kwake bungeni ndiyo salama yao wanajidanganya kwani ataendeleza mapambano yake aliyoyaanzisha akiwa bungeni nje ya Bunge.
Aliitoa kauli hiyo juzi, alipokuwa akipokea tuzo ya Majimaji iliyotolewa na kituo cha Sheria na Haki za Binadamu (LHRC) kutokana na kazi yake aliyoifanya katika kipindi cha miaka mitano katika Bunge la tisa.
Tuzo hiyo hutolewa na LHRC kama ishara ya kuwakumbuka watu wote waliopigana katika Vita vya Majimaji na hivi sasa wamekuwa wakiitoa kwa watendaji wa mahakama na wabunge wanaofanya vizuri katika shughuli zao za kiutendaji.
Dk. Slaa, alisema wakati akiwa bungeni alikuwa akitimiza wajibu wake wa ibara ya 14 na 15 inayoweka bayana wajibu wa mbunge katika kupiga vita ufisadi na ubadhirifu wa mali za umma.
Alibainisha kuwa mbunge yeyote ambaye hakemei au kuuchukia ufisadi anakiuka ibara hiyo lakini pia hafai kuwa kiongozi.
Alisema kuwa mafisadi kamwe wasitarajie wamepata ahueni kwa yeye (Slaa) kuwa nje ya Bunge bali hivi sasa ndiyo atazidisha kasi ya mapambano ya ufisadi ili kuhakikisha rasilimali za taifa zinatumika ipasavyo.
"Mafisadi wajue hivi sasa ndiyo nitakuwa mkali zaidi, wasitarajie kuwa kutokuwapo bungeni kutanifanya nipunguze kasi ya kupambana nao," alisema.
Alibainisha kuwa amefurahi kupata tuzo hiyo ambayo itachangia wanasiasa wengi kutimiza wajibu wao kwa ukamilifu hasa baada ya kugundua kuna taasisi zinafuatilia kazi wanazozifanya ndani na nje ya Bunge.
Mkurugenzi wa LHRC, Fransis Kiwanga, ambaye alimkabidhi tuzo hiyo Dk. Slaa kwa niaba ya Mwenyekiti wa Bodi Askofu mstaafu Elinaza Sondoro, alisema wamempa tuzo hiyo baada ya kufanya uchunguzi wa kina kwa kupitia mitandao mbalimbali na kutoa dodoso katika maeneo ya vijijini ambapo Dk. Slaa alishinda kwa asilimia mia moja.
Kiwanga, alisema mbali na mitandao pia waliwatumia wafanyakazi wa Bunge ambao walipitia majadiliano ya Bunge (hansard) yaliyoonyesha utendaji kazi wa Dk. Slaa.
Alibainisha kuwa walibaini kuwa Dk. Slaa, alifanya kazi zake kwa kuzingatia sheria na haki za binadamu hasa katika uulizaji maswali ulioibua mijadala mbalimbali ukiwemo ule wa EPA na Richmond.
"Dk Slaa alikuwa akilitetea taifa kwa nguvu zake zote hasa katika uulizaji wake maswali ulioibua mijadala mbalimbali kama ule waraka wa EPA alioutoa bungeni wakati wa hotuba ya bajeti ya Waziri Mkuu wa mwaka 2007," alisema Kiwanga.
Alisema Dk. Slaa wakati akiwa mbunge aliweza kuwasilisha hoja yake binafsi ya kutaka kuundwa kwa kamati teule ya Bunge Agosti 13, 2007 ili kuchunguza matumizi mabaya ya fedha za umma.
Hoja nyingine binafsi aliyoitoa Dk. Slaa ambayo ilikuwa inazingatia haki za binadamu ni ile iliyohusu mkataba wa kufua umeme wa Kampuni ya Richmond ambapo alitaka kuundwa kwa kamati teule ya Bunge kuchunguza mkataba huo.
Kutokana na hoja hiyo, kamati teule iliundwa na ilibainisha kuwapo kwa utata katika mchakato mzima ulioipa ushindi kampuni ya Richmond.
Alisema jambo jingine alilolifanya Dk. Slaa ni kuibua hoja ya mkataba wa serikali kwa kampuni ya Alex Stewarts juu ya kuhakiki mapato yatokanayo na dhahabu.
Aliongeza pia alifanya hivyo pale alipohoji uhalali wa Benki Kuu ya Tanzania (BoT) kulipa deni la kampuni ya Meremeta kiasi cha sh bilioni 155 kinyume na taratibu.
Pia alihoji mikataba ya kampuni ya Mwananchi Gold na Deep Green Finance ambapo Benki Kuu ililipa kiasi cha dola za Kimarekani milioni 5.51 (zaidi ya bilioni 5).
Kuhusu historia ya tuzo ya Majimaji, Kiwanga alisema tuzo hii ni ya pili kutolewa ambapo hutolewa kwa watendaji wa Mahakama na Bunge.
Alisema kuwa tuzo ya kwanza ilitolewa kwa mhimili wa Mahakama ambapo Jaji Mwalusanya alikabidhiwa mwaka 2005.
Naye mjumbe wa bodi ya wakurugenzi wa kituo hicho, Dk. Sengondo Mvungi, alisema Watanzania wanaonewa sana kwa kubebeshwa na watendaji walio mstari wa mbele kutafuna rasilimali za taifa.
Alisema deni linalodaiwa na Shirika la Umeme (TANESCO) ni lile la kampuni ya Dowans ambayo iliifikisha TANESCO katika mahakama ya kimataifa ya biashara kupinga kukatishwa kwa mkataba wa kuzalisha umeme.
Alibainisha kuwa hakuna Mtanzania atakayesimama na kupinga deni hilo hivyo taifa linahitaji watu aina ya Dk. Slaa kupinga uonevu unaofanywa kwa Watanzania.
Dk. Mvungi alisema deni linalotakiwa kulipwa na TANESCO la sh bilioni 185 ni kubwa sana lakini hakuna Mtanzania atakayekuwa na ujasiri wa kusimama na kuhoji na badala yake watakubali kulipa bila ya kujua deni hilo litalipwa kwa kupitia ankara watakazokuwa wakizipata!
"Hili deni la Dowans, ni lazima litalipwa hatuna ujanja, tunahitaji watu wa kukemea uonevu wa aina hii kama anavyofanya Dk. Slaa," alisema Dk. Mvungi.
 
Rutashubanyuma

JF-Expert Member
Sep 24, 2010
214,583
2,000
Pole Zitto, huu ndiyo mrejesho wa wananchi
ban.blank.jpg

Abdul Juma

amka2.gif
MWANAFALSAFA mmoja aliwahi kusema kuwa anao uwezo wa kuihamisha dunia hii na kuipeleka sehemu yoyote ile wanakotakiwa watu, isipokuwa akatoa sharti la kupatiwa eneo la kusimama nje ya hii dunia.
Huyu hataki ukitafsiri kwa mapana dhana yake ni kwamba ana upeo mpana, anajaribu kuwafungua watu akili kuwa huwezi kuwa sehemu ya tatizo kisha ukaondoa tatizo. Ana hamu na uwezo wa kuihamisha dunia lakini naye amekaa humo, anataka atoke kwanza ndipo aweze kuihamisha.
Wiki iliyopita niliandika makala nikijaribu kuelezea vituko vya kisiasa anavyovifanya mwanasiasa kijana na rafiki yangu mkubwa Kabwe Zitto ambaye vile vile ni Mbunge wa Kigoma Kaskazini, Naibu Katibu Mkuu wa CHADEMA na aliyekuwa Naibu Kiongozi wa upinzani bungeni.
Katika makala hayo niliyoyapa kichwa cha habari kilichosomeka "Zitto Anaifahamu Thamani ya Umaarufu?" nilieleza umaarufu wa mwansiasa huyo, jinsi ulivyomjenga na kuaminika kwa wananchi yeye na chama chake.
Lakini kati ya mengi niliyoandika, pia niligusia kuwa katika siasa, hakuna aliye maarufu kuliko chama chake, ila kwa Zitto, lazima tukiri kuwa umaarufu wake umeipaisha CHADEMA na amefanikiwa kujizolea imani zaidi kwa vijana.
Kwamba amekuwa gumzo kitaifa kwa kupiga vita ufisadi. Nikakumbusha alivyosulubiwa na Bunge mwama 2007 kwa kukaa nje miezi minne, alipohoji uhalali wa Waziri wa Nishati na Madini wakati huo, Nazir Karamagi, kusaini mkataba wa mgodi wa Buzwagi nje ya nchi.
Ila kwenye hoja nikasema bila kutafuna maneno kuwa Zitto wa enzi zile si huyu tunayemuona sasa. Leo amegeuka ana sura mbili, hajulikani yuko upande upi. Huyu mbali na kuwa Naibu Katibu Mkuu wa CHADEMA, bado anakwenda kinyume na itikadi zao.
Huyu amekuwa kigeugeu yaani ndumilakuwili. Anataka kumfurahisha kila mtu ili asionekane mbaya, jambo ambalo ni hatari na gumu kutekelezeka.
Zitto ni mpinzani, lakini siku hizi amegeuza siasa zake kujenga urafiki ili kukidhi haja ya maswahiba zake kwenye vyama hasimu vinavyokazana kuibomoa CHADEMA.
Tangu kumalizika kwa uchaguzi ndani ya chama hicho, Zitto amekuwa akitoa kauli zenye utata dhidi ya hali ya mambo ndani ya CHADEMA, zikionyesha anatofautiana na viongozi wenzake na hata wanachama.
Nikafafanua wazi kabisa kuwa mipango ya Zitto ya kuuporomosha umaarufu wake haikuanza sasa, bali ni ya muda mrefu na si ajabu kusikia kuna watu nyuma yake.
Nalisema hilo nikikumbushia hatua yake ya kuibuka kwenye vyombo vya habari mwaka jana, akiishauri serikali inunue ama itaifishe mitambo ya Dowans iliyonunuliwa kifisadi.
Itakumbukwa ni CHADEMA akiwemo na Zitto, ndiyo walikuwa wa kwanza bungeni kupinga mkataba wa kampuni hewa ya kufufua umeme ya Richmond LLC ambayo baada ya kushindwa kazi ikatoa zabuni kwa Dowans.
Nisema kuwa ni jambo la kawaida kutofautiana kimtazamo na hivyo sipingi kabisa hatua ya Zitto kutofautiana na chama chake wakati mwingine, lakini kama kiongozi, maamuzi ya chama hana budi kuyazingatia, kama hataki, anatoka.
Nikamhakikishia yeye na wengine wenye siasa za kizamani kuwa CHADEMA haitadumu milele kwa kumtegemea Zitto, Mbowe, Dk. Willbrod Slaa, John Mnyika, Tundu Lissu pekee. Na ndivyo hivyo haiwezi kufa siku wao wakijitoa ndani ya chama.
Zitto anapaswa kutambua kuwa siasa zake kwa sasa zina walakini, haaminiki tena bali anatatanisha wafuasi wake na wanachama wengine kwa ujumla. Heri kama anaitaka CCM au NCCR bora aende huko. Pamoja na mengi niliyoandika nikahitimisha na, "Tafakari na niachie ujumbe."
Nashukuru sana, wasomaji wote waliosoma makala hiyo, wakatafakari kisha wakanipa ujumbe wa simu, nimepokea maoni mengi sana dhidi ya msimamo wa Zitto. Pengine huu nitauita mrejesho.
Nasema hivyo kwa vile hapo juu nilimejaribu kuonyesha fikra ya mwanafalsa aliyekuwa akitaka kuihamisha dunia, lakini akaomba apewe mahali pa kusimama nje ya dunia. Na Zitto ni sawa na mwanafalsafa yule, atambue kuwa hawezi kuipinga CHADEMA akiwa sehemu ya uongozi.
Kiongozi hapingani na wenzake; wanashauriana na kuelekezana hatimaye wanaweka tofauti zao kando na kuwa kwenye msimamo wa pamoja. Nilipoaandika niliamini ningeeleweka hivyo, lakini Zitto hakunielewa bali alinilaumu kuwa nimeegemea upande mmoja.
Tafakari ya kwanza kabisa kuipata ilikuwa ya Mtanzania aiishie Sweden, akaniambia, "Nimesoma makala yako kuhusu Zitto, hakika huyu kijana anahitaji ushauri nasaha, anakoelekea si kuzuri. Mimi nimekuwa nikishauri ajiondoe CHADEMA, kama ulivyosema kuwa chama hicho hakiwezi kufa yeye akiondoka au viongozi wengine."
Lakini kadiri muda ulivyokwenda, ndivyo maoni yalitolewa mengi na hatimaye Zitto mwenyewe naye alinitumia ujumbe mfupi. Kwa vile sikuwajulisha wahusika kuwa ningechapisha maoni yao, sitawataja majina wala namba zao za simu, walau uone walisema nini baadhi.
Ujumbe wa Zitto ulisomeka hivi: "Salaam. Nimesoma makala yako. Ni nzuri na umejenga hoja. Tatizo umeegemea hoja za upande mmoja kufikia suluhisho lako. Hata siku moja sijawahi kujidaia umaarufu (huu ndio unaowatesa).
"Mie ni mtu wa kawaida sana, mtoto wa kimaskini na sijioni maarufu. Endelea kumtafuta Zitto umjue. Zitto ni msemaji wa fikra zake huru bila woga. Umesemea Dowans, umesikia matokeo ya kesi ambapo twalipa mabilioni? Maslahi ya taifa yako wapi? Hata kama humpendi Zitto, msikilize."
Nami katika kumtendea haki Zitto nataka asome walau kwa uchache maoni ya wananchi aone wanamtazamaje kwa sasa. Huyu anasema, "Kwa hali jinsi ilivyotathminika ninyi waandishi mnashughulika zaidi na matukio badala ya kutafiti chanzo.
Kwa namna ulivyoelezea kuhama kwa Kafulila ni wazi kuwa si mfuatiliaji wa mambo yanayofanywa na 'wenye chama'. Punda akichoka hugeuka na kurusha mateke. Zitto kachoshwa na wasiopenda changamoto ndani ya chama chetu."
Mwingine ulisomeka, "Umeandika ukweli kabisa, Zitto hata nia yake ya kutaka kugombea nafasi ya kiongozi wa upinzani bungeni ilikuwa ni kuvuruga chama, hapendi kufuata taratibu."
Yuko aliyesema, "Zitto ni zigo kwa CHADEMA, kabla hawajashika dola hawajui dhana ya uwajibikaji wa pamoja, je wakiishika kina Zitto si watayumbisha baraza la mawaziri? CHADEMA ionyeshe kutokuwa na mzaha na kumwengua, kwani wasipoziba ufa watajenga ukuta."
Msomaji mwingine alisema, "Nilikwisha washauri CHADEMA kuendelea na harakati zao bila Zitto na ikibidi hata bila kuwa na Jimbo la Kigoma Kaskazini. Yaani wamfukuze na uitishwe uchaguzi mdogo na kama wakishindwa sababu Zitto si mgombea wao, basi na iwe hivyo."
Na huyu akaniandikia, "Makala yako imejaa ukweli mtupu, Zitto ni ndumilakuwili na mpenda madaraka, ni mtu wa hatari." Na msomaji mwingine akasema: "Zitto akae chini na wazee wa chama wamshauri na kumpa mifano ya waliomtangulia naamini atabadilika."
Kuna aliyeniambia, "Umeandika na kuhukumu ili kulinda wanasiasa maslahi ndani ya CHADEMA. Tuliokijenga chama kabla yenu na hao kina Zitto tunahuzunika mnavyozamisha jahazi."
Maoni yakawa mengi, mara nikambiwa, "Mimi naona Zitto ana mpango wa kukisaliti chama maana tangu alipoteuliwa kuingia kamati ya madini, amekuwa ni kinyonga. Natoa ushauri kwa chama wampe masharti na asipotii afukuzwe, aende huko anakotaka."
Mitazamo ni mingi, yuko aliyeema, "Ulichoandika kuhusu Zitto ni sahihi lakini mimi nasema pamoja na umaarufu wake wote, hata akiondoka au kufukuzwa bado CHADEMA kitabaki imara, natamani hilo litokee sasa."
Laiti ningeweza kuyachapisha yote, ila Zitto atakuwa amebaini kuwa nilifanya kazi kama mwandishi nikitazama siasa ndani ya chama chake na si kumwonea yeye wala kiongozi yeyote.
Nanukuu ujumbe wa wasomaji kadhaa zaidi nikianza na huyu akisema, "Niko pamoja na wewe, Zitto amekuwa mwana mapinduzi, yaani imekuwa ndani ya Simba kuna Yanga."
"Zitto ameshapata asali ndani ya ile kamati ya madini. Wanasiasa wetu ndivyo walivyo."
Mwingine akasema, "Hivi ni kwa nini wasimuite wakamuulize na kama atabainika wamfukuze kuliko kukiua chama?"
"Nakubaliana na makala yako, kweli tumemchoka Zitto na mambo yake. Tumemsikia wakati wa kampeni jimboni kwake akiwaambia wananchi kuwa 2005 atarudi kama mgombea wa urais. Alijua njama za uporaji wa kura za Dk. Slaa, je chama kitampitisha kugombea? Hatumpendi wala umaarufu wake hautamsaidia."
"Sisi wananchi wa Kigoma tunasema kuwa kama anaona anataka kwenda CCM ili amfurahishe rafiki yake Kikwete ni vema aende atuachie chama chetu kwani Kigoma tumewazoea. Hakuna kiongozi tuliyempenda Kigoma kama Dk. Amani Kabourou lakini njaa yake naye ilimkimbiza tukazoea, sasa sembuse Zitto."
"Zitto amepoteza mwelekeo kila mahali. Yaani huku Kigoma hata akiamua kuondoka na uchaguzi kurudiwa, hapati robo ya kura alizopata uchaguzi wa mwaka huu. Ametuvua nguo watu wa Kigoma."
"Nadhani kama kuna mashabiki wa Zitto, basi hapa Kigoma mimi ni namba moja. Lakini kwa matendo yake hayo watu wa huku tumemkinai mno."
"Ulichomwambia Zitto ni kweli, mkumbushe habari za wkina Dk. Masumbuko Lamwai na umaarufu walioupata wakiwa kambi ya upinzani lakini walipohamia CCM wakapoteza mwelekeo kabisa."
"Zitto ni msaliti wa aina yake, kama anafikiri bila yeye CHADEMA haifiki mbali basi atakuwa anajidanganya nafsi yake mwenyewe, sisi wafuasi wengi wa upinzani ni waelewa na shule inatusaidia ila sijui kama yeye shule ilimkomboa na huo uanaharakati wake kumbe ulikuwa lengo lake kubwa ilikuwa madaraka."
"Mi namshauri Zitto afanye uamuzi wa kweli wa kutubia madhambi yake hayo, ndipo watu tutarudisha imani yetu kwake na atambue kuwa undumilakuwili ni kitu cha hatari. Ajue umaarufu wake umekuja kwa sababu yuko upinzani lakini akiamua kurudi huko CCM ajue amekwisha, hivi karogwa au kawaje jamani?!"
"Zitto kweli kwa sasa hajatulia, kinachonitisha ni nguvu ya mafisadi wanavyoweza kuwanunua hata wale tuliodhani ni watetezi wa wanyonge. Bado tuna kazi nzito ya kupambana na mafisadi."
Nahitimisha na ujumbe huu: "Ni kweli Zitto wa sasa si yule tuliyemfahamu na ubovu wake ulianza pale alipoteuliwa na Rais kuingia kwenye Kamati ya Madini, chama chake kilimkataza yeye akalazimisha.
"Tayari ametangaza kugombea urais 2015. Wakati wa kampeni hakuwahi kutoa neno lolote kuhusu CCM, huyu kwa sasa ni mzigo. Amefikia hatua ya kumhujumu John Mnyika akidai eti aliunga mkono kufukuzwa kwa Kafulila na wenzake."
 
Rutashubanyuma

JF-Expert Member
Sep 24, 2010
214,583
2,000
"Mie ni mtu wa kawaida sana, mtoto wa kimaskini na sijioni maarufu. Endelea kumtafuta Zitto umjue. Zitto ni msemaji wa fikra zake huru bila woga. Umesemea Dowans, umesikia matokeo ya kesi ambapo twalipa mabilioni? Maslahi ya taifa yako wapi? Hata kama humpendi Zitto, msikilize."
Kauli hii ya Zitto inatia mashaka juu ya uwezo wake wa kufikiri kwa sababu hakuna uhusiano wowote ule wa ununuzi wa mitambo chakavu ya DOWANS na ile kesi...................................

TANESCO hawakuwa na ugomvi wowote ule na DOWANS baada ya kumalizika kwa mkataba wao sasa TANESCO ilitoka wapi kukimbilia mahakamani kuizuia DOWANS wasiondoke na mitambo yao?

Waliokuwa na mgogoro na DOWANS walikuwa ni TRA mbona TANESCO hawakuwaacha TRA kuzuia ile mitambo tajwa kwa minajili ya kudai fidia ya kodi yao ya karibu bilioni 9 waliokuwa wanawadai DOWANS?

TANESCO kuzuia mitambo ya DOWANS ulikuwa ni ufisadi ulioihusisha Mahakama Kuu yetu kwa sababu ni uzandiki kwa Mahakama kuafiki hoja za TANESCO wakati DOWANS walikuwa hawajakiuka mkataba wowote ule na TANESCO.......................

Yaelekea hivi sasa ZITTO hatupo kundi moja kwenye vita dhidi ya ufisadi.........mafisadi wamekwisha kumnunua ila sijui kwa bei ipi?
 
superfisadi

JF-Expert Member
May 22, 2009
553
195
Muandishi wa habari wa TBC aliyeenda CDM kutafuta habari na kuzikosa kisha ku -roll eyes ! I think she needs a big uandishi ethics overhaul! I would have fired her on the spot..she didn't have to raise her voice with the mzee there! Get a grip girl!
Anatafuta habari kama mgambo alikosa lugha ya kumshawishi mzee ampe taarifa , ila ameonyesha ni aina gani ya uandishi anafanya .
 
Zak Malang

JF-Expert Member
Dec 30, 2008
5,404
0
Zitto adai amelishwa sumu Saturday, 11 December 2010 21:04

zitto%20kabwe%20hoi.jpg
Fredy Azzah na Fidelis Butahe
MBUNGE wa Kigoma Kaskazini, Zitto Kabwe ambaye jana aliruhusiwa kutoka katika Hospitali ya Aga Khan ya jijini Dar es Salaam alikolazwa kwa matibabu ya tumbo amedai kuwa matatizo hayo aliyapata baada ya kula chakula chenye sumu.

"Namshukuru Mungu naendelea vizuri na nimesharuhusiwa kutoka hospitali, madaktari wameniambia ilikuwa food poisoning (chakula chenye sumu)," alisema Zitto.

Zitto ambaye hakuweza kueleza chakula hicho alikuwa wapi na kina sumu ya aina gani, alisema kuwa baada ya kugundua tatizo hilo, madaktari walimtaka kuwa makini na vyakula anavyokula.

"Sumu gani nimekula na ni wapi, mimi nadhani sio story (habari). Cha msingi kwa sasa naendelea vizuri na nimetakiwa kuwa makini na vyakula ninavyokula," alisema Zitto.

Hata hivyo, kauli hiyo ya Zitto inapingana na madaktari wake waliosema kuwa mbunge huyo kupitia tiketi ya Chadema, alikuwa anasumbuliwa na mchafuko wa kawaida wa tumbo.

"Alikuwa anasumbuliwa na Gastro enteritis (mchafuko wa tumbo), tatizo hili linaweza kusababishwa na bacteria, virusi katika chakula, au kama chakula hakijapikwa vizuri," alisema Dk Mustafa Bapumia.

Zitto alilazwa hospitalini hapo tangu Disemba 9 mwaka huu saa 3:00 usiku, baada ya kutoka kwenye mkutano wa ndani wa chama chake uliofanyika Bagamoyo mkoani Pwani ambako alivuliwa cheo cha Naibu Kiongozi wa Kambi ya upinzani bungeni.

Kuhusu hatua ya chama hicho kumvua Zitto wadhifa wake wa unaibu kiongozi wa upinzani bungeni, alisema kwa sasa bado hawezi kuzungumzia suala hilo kwa sababu hajapata taarifa rasmi kutoka chama chake mbali na kusoma suala hilo kwenye vyombo vya habari.

Hata hivyo, alieleza hakuwahi kuomba kupewa wadhifa huo, kwa hiyo endapo watu waliomwona anafaa kufanya kazi na kumpa wadhifa huo, wakiamua kumnyang'anya siyo tatizo kubwa kwake.

"Kwa sasa nadhani suala la afya yangu ndiyo muhimu zaidi. Ngoja kwanza nitoke hapa na afya yangu iimarike na kama kutakuwa kuna sababu ya mimi kuzungumza nitazungumza," alisema Zitto:

"Lakini ikumbukwe kuwa mimi sikuwahi kuomba wadhifa huu…, kwa hiyo kama watu walionipa wameamua kunibadilishia, mimi sidhani kama kuna tatizo."

Mwenyekiti wa chama hicho, Freeman Mbowe aliupolizwa na Mwananchi Jumapili juu ya Zitto kuvuliwa uongozi bungeni alisema kuwa chama kitatoa taarifa baadaye.

Katika hatua nyingine Mbunge wa Mpanda Mjini, Said Amur Arfi aliyekuwa amelazwa katika Hospitali ya Aga Khan ya jijini Dar es Salaam, amesafirishwa kwenda India kwa matibabu zaidi.

Arfi aliliambia Mwananchi Jumapili kuwa madaktari waliokuwa wakimtibu wamemwambia kuwa mfuko wake wa nyongo una mawe hivyo anahitaji kufanyiwa upasuaji.

"Nilikuja hapa kwa sababu nilikuwa nasumbuliwa na maumivu makali ya tumbo, nilitoka Mpanda Disemba 2, mwaka huu kuja kwenye semina lakini kutokana na maumivu ya tumbo nilienda Hospitali ya Regency na baada ya kupigwa ultrasound nilielezwa kuwa nina tatizo la uvimbe kwenye maini," alisema Arfi.

Alisema alivyokwenda katika Hospitali ya Aga Khan alielezwa kuwa ana tatizo jingine la mawe kwenye mfuko wa nyongo na kuwa inabidi afanyiwe upasuaji.

"Naishukuru serikali kupitia ofisi ya Bunge kunipeleka India kwa matitabu zaidi," alisema Arfi.

Hata hivyo, alisema bado hajaelezwa hospitali anayokwenda kutibiwa na kuwa, taarifa zote hizo anazo muuguzi wa serikali atakayesafiri naye.
Wakati huohuo, Mtangazaji wa Televisheni ya Channel Ten, Cyprian Musiba, anadaiwa kuwekewa sumu kwenye chakula na kufanya alazwe hospitalini kwa matibabu.

Musiba alilazwa katika kituo cha Afya cha Ebrahim Haji kilichopo jijini Dar es Salaam juzi mchana akiwa hajitambui.

Mmoja wa madaktari wa hospitali hiyo, Dk Ramadhani Ali aliliambia Mwananchi Jumapili kuwa Musiba alifikishwa katika hospitali hiyo akiwa anasumbuliwa na tumbo lakini, baada ya kupata matibabu, afya yake iliimarika na jana mchana aliruhusiwa kutoka hospitalini.

"Anaendelea vizuri kwa kweli na amesharuhusiwa" alisema Dk Ali huku akisita kueleza tatizo la lililokuwa linamsumbua Musiba.

Mke wa Musiba ambaye hakujitambulisha alisema kuwa kabla ya Musiba kuruhusiwa mmoja wa madaktari wa HospitaliI hiyo waliwaeleza kuwa Musiba alikula sumu iliyokuwa katika chakula.

"Tumeruhusiwa muda si mrefu ila daktari amesema Musiba alijisikia vibaya kwa kuwa alikuwa amekula sumu iliyokuwa katika chakula,"alisema mke wa Musiba.

Musiba ambaye mara nyingi hutangaza habari za michezo na burudani aliliambia Mwananchi Jumapili kuwa juzi hali yake ilikuwa mbaya na kuongeza kuwa alipelekwa katika hospitali hiyo kwa ajili ya matibabu.

"Hali yangu ilikuwa mbaya sana nilikuwa wa kufa tu ndugu yangu, ila namshukuru mungu naendelea vizuri, ila daktari hapa hospitali amenieleza kuwa nilikula sum," alisema Musiba.

Habari zaidi zilidai kuwa Musiba alianza kupata matatizo ya tumbo saa kadhaa baada ya kula chakula katika hoteli moja iliyopo karibu na ofisi za Channel Ten.

Kwenye red: Huyu jamaa mbona anatusumbua sana akili zetu? nilishawahi kusema humu ndani kwamba huenda he has a screw loose! Na sitashangaa baadaye tukasikia kwamba akina RA walijaribu kuwahonga madaktari wa Aga Khan ili waseme alikula sumu na kukuta trace ya hiyo sumi katika vipimo walivyomchukua!
 
S. S. Phares

JF-Expert Member
Nov 27, 2006
2,141
1,195
Hawa waandishi wetu feki sana...tangu lini Food Poisoning ni LAZIMA mtu uwe UMEKULA chakula chenye sumu??
 
Zak Malang

JF-Expert Member
Dec 30, 2008
5,404
0
Kwenye red: Huyu jamaa mbona anatusumbua sana akili zetu? nilishawahi kusema humu ndani kwamba huenda he has a screw loose! Na sitashangaa baadaye tukasikia kwamba akina RA walijaribu kuwahonga madaktari wa Aga Khan ili waseme alikula sumu na kukuta trace ya hiyo sumi katika vipimo walivyomchukua!

Na ni gazeti la RA -- Mtanzania -- tu ndilo linalopiga debe kwa nguvu kwamba alitiliwa sumu! Hivi anafikiri Watz wote bado mambumbumbu?
 
ifolako

Member
Nov 8, 2010
98
0
Kauli hii ya Zitto inatia mashaka juu ya uwezo wake wa kufikiri kwa sababu hakuna uhusiano wowote ule wa ununuzi wa mitambo chakavu ya DOWANS na ile kesi...................................

TANESCO hawakuwa na ugomvi wowote ule na DOWANS baada ya kumalizika kwa mkataba wao sasa TANESCO ilitoka wapi kukimbilia mahakamani kuizuia DOWANS wasiondoke na mitambo yao?

Waliokuwa na mgogoro na DOWANS walikuwa ni TRA mbona TANESCO hawakuwaacha TRA kuzuia ile mitambo tajwa kwa minajili ya kudai fidia ya kodi yao ya karibu bilioni 9 waliokuwa wanawadai DOWANS?

TANESCO kuzuia mitambo ya DOWANS ulikuwa ni ufisadi ulioihusisha Mahakama Kuu yetu kwa sababu ni uzandiki kwa Mahakama kuafiki hoja za TANESCO wakati DOWANS walikuwa hawajakiuka mkataba wowote ule na TANESCO.......................

Yaelekea hivi sasa ZITTO hatupo kundi moja kwenye vita dhidi ya ufisadi.........mafisadi wamekwisha kumnunua ila sijui kwa bei ipi?

Ruta-Shuba-Nyuma!
 
Zak Malang

JF-Expert Member
Dec 30, 2008
5,404
0
Mafisadi wanataka kufanya walichomfanyia Chacha Wangwe na Zitto alivyokuwa akili ndogo anaingia kichwa kichwa! Tungekuwa na vyombo vya upelelezi makini ambavyo havijaingiliwa na mafisadi, wangejua ni nani alihusika kumuuwa Wangwe. Badala yake walikaa kimya na kuridhika na mwenendo wa vyombo vya habari vya mafisadi vilivyokuwa vinajaribu kuonyesha kwamba viongozi wa juu wa Chadema ndiyo wahusika!!!

Jamani hakuna mtu wa kumkalisha Zitto na kumueleza anachokifanya ni hatari kwake?
 
Nduka

JF-Expert Member
Dec 3, 2008
8,555
2,000
Inabidi awe wazi kueleza nani kamlisha hiyo sumu...ni Jack Zoka naibumkurugenzi wa UwT? Maana wanaweza kumlisha sumu ili asitoe siri za vikao vyao vya jinsi ya kuiua CHADEMA. Lakini pia inawezekana UWT wamemwambia aseme hivyo ili ionekane chadema ndio wamemfanyia hivyo...maana zito haaminiki kama aliweza kuongelea udini kwa maelekezo ya UWT hawezi kusita kuzua tena alimradi tu wamuahidi pesa nzuri.

Kwani yeye pia ni mzee wa CDM au yeye na chongo wanauhusiano? UWT hawana maslahi wala ugomvi na Zitto ila CDM na Mbowe wana ugomvi hivyo wana motive ya kumu eliminate, nadhani hawajajua kuwa sumu haiwezi kumuua huyu Muha wamesahau walikwishajaribu mara ya kwanza?
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom