Madaktari Wapigana Hospitalini, Mtoto Afariki | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Madaktari Wapigana Hospitalini, Mtoto Afariki

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Pdidy, Feb 27, 2010.

 1. Pdidy

  Pdidy JF-Expert Member

  #1
  Feb 27, 2010
  Joined: Nov 22, 2007
  Messages: 36,031
  Likes Received: 6,831
  Trophy Points: 280
  Madaktari Wapigana Hospitalini, Mtoto Afariki


  Dr Sinomar Ricardo alidundana na daktari mwenzie badala ya kumhudumia mwanamke mjamzito Saturday, February 27, 2010 1:59 AM
  Madaktari wawili wa nchini Brazili walitwangana makonde kwa zaidi ya nusu saa badala ya kumhudumia mwanamke mjamzito aliyekuwa akiwasubiria wamalize kupigana ili wamzalishe.
  Madaktari wawili wa nchini Brazili waliacha kazi ya kumzalisha mwanamke na kuanza kutwangana makonde mbele ya mwanamke mjamzito aliyetakiwa kuzalishwa kwa njia ya operesheni.

  Mwanamke aliyejulikana kwa jina la Gislaine Santana, 32, aliingia kwenye leba na kusubiria kuzalishwa kwa njia ya operesheni wakati ngumi zilipozuka ghafla kati ya madaktari wawili ambao walitakiwa kumfanyia operesheni hiyo.

  Kwa mujibu wa gazeti la Folha de Sao Paulo la Brazili, madaktari hao walitwangana makonde mazito na kugaragazana kwenye sakafu za wadi ya uzazi huku mwanamke huyo mjamzito akipiga kelele akitaka waache kupigana.

  Daktari wa tatu alikuja dakika 90 baada ya tukio hilo na kumzalisha mwanamke huyo lakini mtoto wa kike aliyezaliwa alikuwa ameishafariki.

  "Sitaki kusema chochote, lakini mpaka mke wangu anaingilia leba, mtoto wangu alikuwa bado yu hai na mwenye afya njema", alisema mume wa mwanamke huyo.

  Mamlaka husika za nchini Brazili zimewafukuza kazi madaktari wote wawili waliodundana na wameanzisha uchunguzi kuhusiana na kifo cha mtoto huyo.
   
 1. This site uses cookies to help personalise content, tailor your experience and to keep you logged in if you register.
  By continuing to use this site, you are consenting to our use of cookies.
  Dismiss Notice
 1. This site uses cookies to help personalise content, tailor your experience and to keep you logged in if you register.
  By continuing to use this site, you are consenting to our use of cookies.
  Dismiss Notice
Loading...