Madaktari waonya kuhusu ulaji ''keki na peremende kazini''

Kurzweil

JF-Expert Member
May 25, 2011
6,622
8,397
Madaktari wa meno wameshtumu utamaduni wa kazini wakisema ugawanyaji wa keki na peremende unachangia matatizo ya kiafya.

Idara ya afya ya meno imesema kuwa watu wanafaa kupunguza ulaji wa keki na biskuti kazini kwa sababu vyakula hivyo vinawafanya kunenepa kupitia kiasi mbali na afya mbaya ya mdomo.

Profesa Nigel Hunt amesema kuwa wafanyikazi wanahitaji kubadilisha utamaduni wa kazini.

Ili kuweza kupunguza ulaji wa vyakula vyenye sukari wafanyikazi wameshauriwa kutumia vyakula hivyo kama chakula cha mchana mbali na kuvificha .

Profesa Hunt ,muhadhiri wa chuo kikuu cha Royal College of surgeons ,alisema kuwa huenda wasimamizi wa afisi hizo wanataka kuwazawadi wafanyikazi, wafanyikazi kutaka kusherehekea ama mtu anayeleta zawadi afisini baada ya likizo hatua inayosababisha vyakula vya sukari nyingi kuingia afisini.

Lakini amesema kuwa hilo linaathiri afya ya wafanyikazi na ni muhimu kufanya uamuzi wa mwaka mpya wa kukabiliana na utamaduni wa vyakula vya sukari.

''Ijapokuwa peremende hizo huenda zikawa na maana ,zinachangia unenepaji wa kupitia kiasi pamoja na afya mbaya ya mdomo,''aliongezea.

Tunahitaji kubadili utamaduni katika afisi zetu ambao unashawishi ulaji wa vyakula vya afya na unawasaidia wafanyikazi kutotumia vyakula vya sukari kama vile, keki, peremende na biskuti.

Chanzo: BBC
======

JAMII LEO
 
Jana tu nimeng'oa jino langu la mwisho lile la chini, ilikuwa ni shughuli pevu, maana nilipigwa spana, pliers na drill za umeme utafikiri gari, nashukuru Mungu lilitoka. Sili tena ice cream, keki, biskuti wala majuisi ya ajabu ajabu, nimekoma
 
Back
Top Bottom