Madaktari,wananchi na viongozi: Tafakarini haya | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Madaktari,wananchi na viongozi: Tafakarini haya

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by hippocratessocrates, Jul 2, 2012.

 1. h

  hippocratessocrates JF-Expert Member

  #1
  Jul 2, 2012
  Joined: Jul 1, 2012
  Messages: 3,612
  Likes Received: 26
  Trophy Points: 135
  MGOMO WA MADAKTARI: TUTAFAKARI.

  Ni ndefu ila fika mwisho, TAFADHALI.

  Wakati mwingine huwa ninapata shida sana kufikiri ni jinsi gani watanzania tulivyojawa ushabiki, ujinga, upuuziaji wa mambo ya msingi na kuunga mkono matendo maovu na zaidi ya yote kuona kila nia mbaya kwa kila jambo jema linalotokea au kutendwa!!
  1.
  Ushabiki(swala hili linapoangaliwa kimtazamo wa vyama, wakati ni la kitaifa)

  2. Ujinga (kuchangia mada kwa kuangalia matokeo ya jambo na si chanzo cha jambo)

  3. Upuuziaji wa mambo ya msingi (unapoita jambo lina umuhimu lakini unashindwa kulithamini au kufanya juhudi kulitatua)
  4. Huruma kwa vitendo viovu (kushabikia kuteswa kwa mtu yule yule unayemuhitaji akusaidie kuokoa maisha)
  5. Fikra mbaya (kuwa jambo lolote linalodaiwa au kuombwa lina nia mbaya na mwombwaji)
  6. Wivu usio wa maendeleo( Jirani yako asiendelee kwa sababu tu wewe HUTAKI kuendelea)

  MTAZAMO:
  -
  USHABIKI: Jambo hili linapaswa kuangaliwa kwa umoja(kama taifa) na si ubabe, ushabiki wa vyama, elimu, wala udini kama linapotaka kuelekea( kwani kuelekea huko kunafanya watanzania wengi kuangalia lile linalokuja na si chanzo ni nini) bali kwa kutumia busara.
  - UJINGA: “Ujinga” si tusi kama hili neon lichukuliwavyo na watu wengine, ila lina maana ya kutokuwa na ufahamu. Ningeshauri wananchi wasiojua chanzo cha tatizo kujua na kuangalia nini ni chanzo (madai) cha mgomo huu wa madaktari. Lakini kama ni shida kupatikana kwa madai ya madaktari, unaweza kuyasoma hapa;

  i. Kuondolewa kwa viongozi wakuu katika W/Afya kutokana na ushahidi wa uovu wao
  ii. Kuboresha huduma za Afya hospitalini(ongeza vitanda, watumishi, madawa, zana za kazi)
  iii. Kuwapatia watumishi wa sekta ya Afya kadi ya kijani ya Bima.
  iv. Kudai posho ya kuitwa kazini kwa 5%.
  v. Pendekezo la posho ya kufanya kazi katika mazingira hatarishi (30%) AU chanjo
  vi. Pendekezo la posho katika mazingira magumu (30%) AU makazi.

  vii. Pendekezo la mshahara kuwa mil.3.5, (sawa na ongezeko la 70%)


  Katika makubaliano ya serikali na madaktari ombi la kwanza liltekelezwa(kwa ucheleweshwaji), wakati ombi la nne llikipangwa kutekelezwa kwa nusu asilimia pendekezwa hadi pale mazungumzo yatakapokwisha (ambayo haijatekelezwa hivyo ingawa ilisemwa hivyo BUNGENI). Kutokana na madai yaliyobaki kuhitaji pesa “nyingi”. Serikali ilitoa tamko kuwa itashughulikia na madaktari kukubali kurudi kazini na katika bajeti ijayo ya 2013/2014 kuongezwa kwa ajili ya madai hayo muhimu.(ambayo w/Afya imezidi kupunguzwa)


  Ni nani asiyejua umuhimu wa kujikinga na magonjwa(homa ya ini, UKIMWI, kifua kikuu)?leo hii daktari yule yule anayefundisha jamii jinsi ya kujikinga, anapoomba chanjo au fedha ili atafute namna ya kujikinga ni shida?!


  Mazingira ya kijijini na upatikanaji wa huduma unajulikana, ni tofauti na mjini lakini pale madaktari wanapoomba posho iongezeke afike huko katika vijiji katika kutoa elimu(kwani ni moja ya kazi yake) inakuwa shida?

  Si ajabu kukuta mwananchi au kiongozi akilalamika kuwa, “mnadai pesa nyingi”, “wanatuelekeza kwenye maduka yao ya dawa” , “wanachukua dawa za hospitalini”. “wanatuelekeza katika hospitali zao” lakini akisahau kuwa kisheria mshahara wa mwajiriwa unategemea:
  *muda alioutumia akiwa shuleni (ugumu wa masomo),

  *kiwango cha elimu,
  *ugumu wa kazi,
  *na muda wa kufanya kazi.

  Na ndiyo sheria hii hii inayodai madai kama ya kuitwa kazini(call allowance)/katika fani nyingine ikiitwa “overtime” isemayo inapaswa kuwa(5%) kisheria, lakini leo ikidaiwa ni shida?

  Wakati mwingine utasikia wanasema, “wanatuelekeza kwenye maduka yao ya dawa”, “wanachukua dawa za hospitalini”. Lakini wanachanganya na kudhani kila avaae koti jeupe hospitali au duka la dawa ni daktari!! Kama kila ambaye anafanya kazi ikulu ni Rais, muda huu unaosoma makala hii tuna marais wangapi??!


  Nijuavyo mimi pale Muhimbili wodi za watoto, wakina mama mnajua hali ilivyo(wagonjwa watatu kutumia kitanda kimoja, hivyo sijui kama wagonjwa wanakuja kupata matibabu au kupeana magonjwa)! hakuna vitendea kazi wala madawa
  Hivyo ndivyo ilivyo pia katika hospitali ya Bugando na pale KCMC, kule Mbeya ndio hatari zaidi.


  -Leo hii mama mjamzito akija hospitali kujifungua bure(kama ilivyo katika sera) na kuambiwa akanunua pamba, analalamika anaonewa, akidhani madaktari watakula hizo pamba!

  -Watoto wanakufa kwa kukosa madawa na wakiambiwa wakatafute dawa nje(kwa faida yao wenyewe kwani madawa hakuna inakuwa ni kosa)

  -Ukitaka kufanyiwa upasuaji na kuambiwa hakuna damu, ndugu waje kuchangia damu au uchangie gharama, watu wanadhani madaktari wanakunywa damu! Kwani hata kama ndugu wakichangia inabidi kupimwa kutokana na magonjwa, na wakati mwingine wagonjwa hawapewi damu kutokana na damu iliyotolewa na ndugu zao ni chafu(ina magonjwa-na haitakiwi hata kumwambia mgonjwa siri hiyo).

  -Unapokuta mstari mrefu wa kupigwa picha za mionzi(X-ray) na kuambiwa machine hazifanyi kazi, wananchi wanadhani ni madaktari walioharibu machine au kuipeleka hospitali binafsi. Mf Hospitali ya mkoa/rufaa TANGA. Je hospitali za wilaya zina hali gani? Vijini je?

  Madai ya posho, ni pendekezo, hivyo kama serikali inapaswa kuangalia ni kwa kiasi gani inaweza kuongeza posho/mishahara na tatizo kutotokea tena na si kutumia fursa hiyo kuongeza kiasi chochote kisichokuwa na mantiki na kusema imeongezeka!! Wapi kuna shurutisho kwamba bila mil3.5 haturudi kazini, au tunatofautiana katika kusoma na kudadavua?


  Lakini zaidi ni pale kunapokuwa na ushindani kati ya kundi la wasomi ambalo wananchi wenyewe ndio wanawaita, “cream of the nation’ ( waliokuwa wakifanya vizuri sana darasani, hii ikiwa ina maana ya shule za sekondari, na elimu ya juu -sasa kwa umoja wao) na makundi mengine, na wananchi kudhani kundi hili halina maamuzi ya busara au kuchambua mambo ya msingi, madai, madhara, uwezekano wa utekelezaji (HII HAIMAANISHI HAKUNA WENYE BUSARA PIA AU UFAULU WAO HAUKUWA MZURI KWA KUNDI JINGINE isipokuwa kwa kulinganisha na kundi la hao mnaowaita hawana utu)

  Mfano hai:

  Ni sisi madaktari tunaokaa macho ANGALAU masaa 30 kazini kabla ya kukabidhi kwa daktari mwingine,

  Hii ikiwa unapoingia asubuhi unafanya kazi kupita wodini, kwa mgonjwa mmoja mmoja(ukiwa umesimama) hadi mchana, na kisha kwenda kufanya/kusaidia upasuaji(ukidumu kusimama), kwa uzoefu wangu mdogo, upasuaji uliochukua muda mfupi ni masaa 2,lakini ikumbukwe kuwa kwa siku upasuaji unafanyika angalau kwa wagonjwa wanne!!

  Mara baada ya kufanya upasuaji unatakiwa kushinda wodini ukisubiri wagonjwa huku ukijisomea(kuongeza ufahamu wa magonjwa yanayogundulika kila leo pamoja na madawa), hii namaanisha unatakiwa kuwa macho usiku mzima kama vile walinzi wawapo lindoni!!!  Asubuhi ya siku inayofuata, unatakiwa kukabidhi wagonjwa(hii ni kwa kutoa taarifa kwa daktari atakayekuja siku hiyo), taarifa hizi hutolewa kwa kuwapitia wagonjwa wale uliowalaza usiku wakati ukijisomea!!


  - UPUUZIAJI WA MAMBO YA MSINGI: Kuna msemo wa kiingereza unaosema, “Desperate times, take desperate measures” lakini kama hatua zitakazochukuliwa ni za ubabe basi ninahisi tutakuwa tunatofautiana katika kutoa maana ya neno DESPERATE. Sekta ya Afya ni muhimu kama zilivyo sekta nyingine, lakini wakati mwingine ni muhimu zaidi ya nyingine kutokana na kuhusishwa moja kwa moja na uhai wa watu. Hivyo kama ni kutokana na umuhimu huu, inapaswa kuangaliwa matatizo kama ambayo yaliyotokea na ambayo yataendelea kutokea iwapo hayatapatiwa ufumbuzi.
  Leo hii wananchi wengi wanaishi na watumishi wa ndani (housegirl/boy), wengine huwa wanaonewa na kutendewa vibaya hata kama makosa yakiwa ni ya watoto wa mwajiri, lakini ndiye huyu huyu mtumishi wa ndani unayetegemea akupikie chakula!! Chakula kile kile kinachoweza kuondoa uhai wako kwa sumu ya panya inayouzwa mitaani!!!? Inakuwaje ukimuonea hadi na yeye anapoamua liwalo na liwe?
  - KUUNGA MKONO VITENDO VIOVU: Wakati mwingine ninajiuliza hivi hawa ndio wale wale watanzania wasemao wana amani, utu na uzalendo? Inakuwaje kitendo alichofanyiwa Ulimboka Steven(Daktari) kushabikiwa namna hii? Je, hata kama ingekuwa kweli anadai mambo yasiyo na msingi angepewa stahili ile?
  Yuko katika jamii (jumuiya ya madaktari), na kwa watu wengine busara zao(madaktari) inatafsiriwa kana kwamba hawana hisia. Je, wakifanya kazi kwa shingo upande, itakuwaje? Je, unadhani viongozi watakwenda hospitali za serikali au ni mwananchi yule mwenye kutoa maneno mabaya muda huu kurudi katika mikono ya wale aliowaudhi akitegemea uhai wake uwe salama?

  Lakini ni kwanini mwananchi(au kama ilivyokuwa kwa kiongozi Bungeni) aseme kuwa amepata stahili yake?? Je, si serikali inapaswa kulaumiwa kwa kutotoa huduma na si mwajiriwa?

  - FIKRA MBAYA: Watu wanajiuliza hivi madaktari wana utu kweli? Kweli kuacha watu wafe kwa ajili ya “maslahi” yao wenyewe? Watu waliosomeshwa bure na pesa za kodi ya wananchi? Lakini wakisahau kujiuliza madai ya msingi ni yapi na ni nani yuko katika mkataba wa kutibu wananchi wake!  Ukiwa na mtoto mnyenyekevu/muadilifu/mwenye tabia njema na ghafla akabadilika nadhani unapaswa kujiuliza wapi wewe kama mzazi/mlezi hufanyi jitihada au umeondoa nini kwake alichokuwa anakipata.  Lakini katika kujibu maswali ya wananchi (labda kutokana na kutoelewa undani wa jambo hili) Ndiyo, Madaktari tuna utu(kwani nami ni mmoja wao), na hatuwaachi wananchi wafe ila tatizo kubwa ni kutoelewa nani anapaswa kulaumiwa(kwani badala ya wananchi kutoa ushauri na njia mwelekeo wanaendelea kulumbana), hakuna mahali ilipoainishwa kuwa madaktari watawahudumia wananchi ila Serikali itatoa huduma ya Afya kupitia waajiriwa wake (Madaktari).  Ikumbukwe kuwa madai ya madaktari yapo katika sehemu mbili. Sehemu ya kwanza ikiwa ni kutoa huduma kwa wananchi NA huduma kwa mwajiriwa(daktari) ikiwa sehemu ya pili. Inashangaza kuona kuwa wananchi wako tayari kutoona umuhimu wa sehemu ya kwanza(madawa, vitanda, vifaa vya upimaji) na kutounga mkono sehemu ya pili ya madai(kutumia nguvu, akili na uwezo wao wote kupinga PENDEKEZO la posho ikiwa kama dai moja wapo)!!

  Kwa wafanyakazi, wengi(kama sio wote) kabla ya kupewa ajira mliulizwa pendekezo la mshahara wako uwe kiasi gani, na ilipoleta utata mlijadiliana na mwajiri wako, kwa wengine ilipokuwa shida mliacha nafasi hizo na kwenda sehemu nyingine. Je, utofauti huo uko wapi katika sekta ya Afya?


  Kama watu wanadhani bado madaktari wanasomeshwa bure kama inavyodaiwa, wawaulize wadogo zetu walioko vyuoni HKMU,IMTU, WBUCHS, KCMC, nk. Takribani miaka miwili iliyopita wanafunzi wa IMTU waligoma kwa sababu ya ada yao kuongezwa sana, sasa sijui kusomeshwa huku kunakoongelewa kunatoka wapi!  -WIVU USIO WA MAENDELEO: Wakati mwingine najiuliza kwa nini watanzania tuna akili ya namnahii! Kwa kuwa jirani yako anatembea kwa miguu, na wewe uendelee kutembea kwa miguu kilomita kadhaa kwenda sokoni ingawa una uwezo wa kununua baiskeli!! Kwa kuwa walimu hawagomi(labda ni kutokana na kuridhishwa na mazingira ya kazi) na madaktari wasigome? Kwa mfano dai la posho, haina maana kupinga watu kufanya hivyo wakati wanazo sababu za msingi!! Watu wanapinga mgomo kwa kusema “kama mkiongezewa pesa na sisi si itaongezeka” sasa unadhani tutaishije?. Sasa unajiuliza, je hii ndio sababu ya msingi ya kuzuia mgomo? Ni dhambi watumishi wa kada nyingine wakiongezewa mshahara? Wanajua utaoongezeka kweli, lakini kwasababu ya kujua hawataweza kusimama kwa umoja hadi mwisho ndiyo iwe tatizo kwa sekta nyingine wakiamua kwa umoja wao kutoachana? Wivu ni mzuri, lakini uwe wa maendeleo. Au Serikali inadhani kwa vitisho ndiyo itaaharibu umoja wetu madaktari?


  Nadhani yahitaji ziada kubwa, kutatua mgogoro wa wale uliowachagua wakiwa bora katika bora huko mashuleni

  MWISHO:


  Kwa kumalizia tungejiuliza hao madaktari(kama si watu wa kusaidia madaktari-Paramedics) kutoka Iran watakuwa na ukaribu na wananchi kuliko madaktari wa nyumbani? Je, uwiano wa daktari mmoja kwa wagonjwa wa Iran tunaujua? Je, watakuja na misaada ya vifaa na madawa na mazingira bora? Je, gharama za wakalimani isingefaa kuboresha huduma za Afya na kulipwa madaktari wa hapa? Je, ni mzazi/mlezi gani atamshauri mtoto wake kusomea utabibu? Je, hili ndilo litakalokuwa suluhisho kwa migomo katika sekta nyingine?

  Nchi kutegemea misaada kwa 60% ya bajeti yake na kukaidi agizo la Wamarekani na kukubaliana na wa-Iran kama wengi mjuavyo tayari, haituweki katika kukosa misaada(maana ndiyo tuitegemeayo)! Kama hiyo haitoshi Je, hatuingizwi katika orodha ya nchi chache zinazotoa ushirika katika nchi zinazo tuhumiwa kuwa na uhusiano wa kigaidi? Tatizo hili halipelekei kuwa na matatizo mawili makubwa(yaani tatizo la sasa ambalo halijatatuliwa na hilo jipya tunalolikaribisha la kimataifa?


  KARIBUNI MADAKTARI WAPYA, WASTAAFU KWA MOYO MWEUPE PEEE!

  MUNGU ibariki Tanzania,

  MUNGU mbariki Daktari Ulimboka Steven (The Tanzanian Father of Medicine)

  MUNGU tubariki madaktari.
   
 2. mtotowamjini

  mtotowamjini JF-Expert Member

  #2
  Jul 2, 2012
  Joined: Apr 23, 2012
  Messages: 4,540
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 0
  JK ashasema hela haipo so kama hamtaki kazi msepe, so hakuna haja ya kuendelea kulalamika tena hapa
   
 3. Zanta

  Zanta JF-Expert Member

  #3
  Jul 2, 2012
  Joined: Apr 4, 2011
  Messages: 2,017
  Likes Received: 70
  Trophy Points: 145
  Kua mkweli tu ndugu shida yenu saana ni hapo kwenye RED (7m)
   
 4. M

  Msendekwa JF-Expert Member

  #4
  Jul 2, 2012
  Joined: Mar 11, 2012
  Messages: 440
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35
  Ndiyo ni hapo kwenye 3.5M, na sio 7m km Dhaifu alivyopotosha, na wanastahili.
  Na kitaeleweka tu.
  Tangu ln dhaifu akachimba mkwara ukawa kweli?
  Au anadhani ana deal na TUCTA aliowaita mbayuwayu wakanywea?
   
 5. h

  hippocratessocrates JF-Expert Member

  #5
  Jul 2, 2012
  Joined: Jul 1, 2012
  Messages: 3,612
  Likes Received: 26
  Trophy Points: 135
  Sometimes it's better to keep quiet and people to think may be you are a fool, than to talk and remove all doubts.

  Kuna utofauti mkubwa kati ya KUTOELEWA na KUTOTAKA KUELEWA!!
  tofauti ni kwamba asiyetaka kuelewa "not only he i accept he is at the mud, but he also LIKE being there!"

  Fuatilia kujua madai ya madaktari ni yapi, na serikali kupitia vyombo vya habari(ikiwa ni gharama nyingine) kuweka madai yao, wakidhani kwa kupotosha wananchi watasahau/kuogopa,wakidhani madaktari wanategemea support ya wananchi wenye uwezo mdogo kupambanua mambo(kama mwanasiasa)..these people have brains, we use brains.
   
 6. M

  Mukalabamu Member

  #6
  Jul 2, 2012
  Joined: Oct 22, 2008
  Messages: 53
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 15
  well narated,anayetaka kuelewa ameelewa asiyetaka basi kanyaga twende,hakuna atakayedai haki yenu bali nyie wenyewe,wala support ya hao wanaohongwa tisheti na kapelo za ccm sidhani kama mnawahitaji katika mapambano yenu,hata siku moja sijawahi kusikia mwananchi akilalamika kuwa mazingira ya kazi ya udaktari ni magumu!alaliaye kitanda ndiye anayejua kunguni wake
   
 7. h

  hippocratessocrates JF-Expert Member

  #7
  Jul 2, 2012
  Joined: Jul 1, 2012
  Messages: 3,612
  Likes Received: 26
  Trophy Points: 135
  The hottest people in HELL will be for those who n greay time of advesary like this, they maintaon their neutrality...
  Just pick your side either politics or profession! neither both nor none.
   
 8. BPM

  BPM JF-Expert Member

  #8
  Jul 2, 2012
  Joined: Mar 10, 2011
  Messages: 2,766
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 135
  Asnte kwa mchanganuo , wa kuelewa ataele na hata wale wadhaifu walau watapata mwanga
   
 9. Njilembera

  Njilembera JF-Expert Member

  #9
  Jul 2, 2012
  Joined: May 10, 2008
  Messages: 1,424
  Likes Received: 154
  Trophy Points: 160
  Duh ilikuwa refu lakini yenye busara na mantiki! Asiyeelewa ni mbumbu na tena ni mdhaifu.
   
 10. h

  hippocratessocrates JF-Expert Member

  #10
  Jul 2, 2012
  Joined: Jul 1, 2012
  Messages: 3,612
  Likes Received: 26
  Trophy Points: 135
  Really TBC?!sometines i wonder if even the TBC news reporters and other workers watch that channel at their homes!
   
 11. h

  hippocratessocrates JF-Expert Member

  #11
  Jul 2, 2012
  Joined: Jul 1, 2012
  Messages: 3,612
  Likes Received: 26
  Trophy Points: 135
  TBC!!Mtapata laana
   
 12. Tetty

  Tetty JF-Expert Member

  #12
  Jul 2, 2012
  Joined: Jan 6, 2012
  Messages: 25,560
  Likes Received: 16,530
  Trophy Points: 280
  Sijui wadnganyika tumetiwa pamba kichwani badala ya ubongo!Ni kweli tunapenda kulalamika pembeni kuwa mazingira ya hospitali mabaya,lakini wakigoma madaktari kwa ajili ya hiyo haki ya mdanganyika huyu kupata haki ya msingi ya huduma za afya tunawatukana,kuwadhalilisha na hata kuwajeruhi.Kuna siku viongozi wetu watajibu kwa muumba wao.Watawala for once wamuogope Mungu,watende haki.Tanzania ni ya kwetu sote siyo ya wanaccm nafamilia zao.
   
 13. U

  Undertaker New Member

  #13
  Jul 2, 2012
  Joined: May 1, 2011
  Messages: 2
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Nimekusoma dr,haki haipatikani bila kupambana Mungu atawasaidia.Nashaanga watu wanaodai ma dr wahitaji pesa nyingi, mnasahau jamaa wanaosinzia na kushabikia mambo ya kipumbavu mjengoni lakin wanaBelipwa pesa nyingi hakuna anayesema.Huu ni muda wa mabadiliko.
   
 14. S

  SANING'O LOSHILU Senior Member

  #14
  Jul 2, 2012
  Joined: May 19, 2012
  Messages: 144
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Hakuna hoja za msingi mlizonazo sasa hivi manake migomo yenu ipo kimaslahi zaidi then mnawadanganya wasiojua kuwa mnawapigania watanzania, sasa baba ridhi kasema rudi kazini hutaki acha sasa wewe ingiza kiburi uone
   
 15. Mkirua

  Mkirua JF-Expert Member

  #15
  Jul 2, 2012
  Joined: Sep 9, 2010
  Messages: 5,667
  Likes Received: 24
  Trophy Points: 135
  Acha kulia nilisema tangu mgomo wa mwanzo na sasa naendelea kusema mmeshaambiwa kuwa nendeni huko wanakolipa hizo mnazozitaka sijawahi kuona watu walio na roho mbaya kama ninyi wauwaji wakubwa .... mpo tayari kuwatoa ndugu zenu watanzania wenzenu kafara kwa ajili ya kudai milioni 3...to hell...hukulazimishwa kusomea hiyo kazi kama vipi acha kuliko kuwa na mizigo tukidhani binadamu...ninyi huyo ulimboka ndo mlidhani wa maana sio?? pelekeni9 basi na watanzania wanaokufa kwa ujinga wenu south afrika.
   
 16. TZ biashara

  TZ biashara JF-Expert Member

  #16
  Jul 3, 2012
  Joined: Mar 9, 2012
  Messages: 523
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 0
  Nimejaribu kuisoma kwa makini na kuelewa shida mnazopata ila sijaweza kukufahamu ktk rangi nyekundu ni kama unajaribu kuwaconvince watu na vitu vya kulazimisha au kulazimishwa.Madaktari nyinyi ni watu muhimu kwakweli wala haina ubishi.Nikweli wizara ya afya inabidi iangalie hili suala hasa la vitendea kazi ni moja ya vitu muhimu.Na kama unataka suport kutoka nje ni vizuri kujielezea shida ziazostahili kurekebishwa lakini usiingize mambo ambayo yanaweza yakakushushia hadhi yako.Kwani masuala ya ugaidi wakati mwingine hujui yupi gaidi hapa duniani.Mimi nadhani gaidi ni yule anaeua au muuaji na sijawahi kusikia Iran inafanya mauaji.Anyway good luck
   
 17. h

  hippocratessocrates JF-Expert Member

  #17
  Jul 3, 2012
  Joined: Jul 1, 2012
  Messages: 3,612
  Likes Received: 26
  Trophy Points: 135
  you have very good point Tzbiashara but the problem i see is that US cant and wont understand that (though you and i know that we dont harbour terrorists)
   
 18. M

  Mkojo Member

  #18
  Jul 3, 2012
  Joined: Jul 3, 2012
  Messages: 32
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Jina la mtoa mada ni aina ya dawa?
   
Loading...