Madaktari wamuweka JK kikaangoni! Ni kuhusu uamuzi wa kumfukuza kazi Dr Mponda

Status
Not open for further replies.
siku nilipojua kuwa Mponda ni kihiyo ni pale wakati anasoma makadirio ya bajeti ya wizara yake alipokuwa akitamka CCRBT badala ya CCBRT. na alirudia hivyo zaidi ya mara tatu. Hansard shaidi yangu
 
Kwa JK Dr Mponda na Nkya ni bora zaidi kwake kuliko Watanzania kwahiyo ni bora Watanzania wafe lakin hawa mawazili wabaki madarakani lakini hili si laajabu kama watu wanatoa roho za watu kwa ajili ya ubunge hili litashindikana tumeona Igunga na Arusha.
 
kikwete hana dhamira ya hdati na watanzania...ni mtu mjinga na wa ajabu sana.....hana sifa na wala hastahili kuongoza nchi...anakera sna na kuudhi sana...safari hii ni kuungana na kukataa upuuzi huu wa jakaya na aserikali yake....
 
Whats wrong with this guy m'k'w'e'r'e?
Why he can't improve himself? How
Did we managed to have a sloppy
Like him?

Unaweza kuwa na point ila ungeandika kiswahili tu nadhani ungeeleweka zaidi. Si lazima uandike lugha za watu hata kama hazipandi.
 
mbona chenge aliweza kuachia ngazi kwa ajili ya kauli yake ya 'vijisenti'...inakuwaje hawa incompetent kenge wawili(mponda na nkya) wanashindwa kuachia ngazi?
na kenge waliowezesha jk kusimikwa ikulu kweli ni wa kulaaniwa...!
 
wanza hao madaktari tunawadai mshahara wa mwezi waliokuwa kwenye mgomo maana hawakuufanyia kazi.huo nao ni ufisadi
 
mbona chenge aliweza kuachia ngazi kwa ajili ya kauli yake ya 'vijisenti'...inakuwaje hawa incompetent kenge wawili(mponda na nkya) wanashindwa kuachia ngazi?
na kenge waliowezesha jk kusimikwa ikulu kweli ni wa kulaaniwa...!

hata wewe pia ni kenge mkubwa
 
Lakini JK anayo hofu ya msingi;kama leo madaktari wanaweza kumlazimisha - chini ya tishio la mgomo - kuondoa mawaziri aliowateua yeye mwenyewe ni kitu gani kitazuia makundi mengine mbeleni kudai hivyo hivyo? Walimu, Polisi, wafanyakazi wa utumishi n.k? Kama angeweza kuwaondoa yeye mwenyewe mara moja kabla ya ule mgomo kuwa mkali ingeonekana ni initiative yake; lakini, kama ataamua kufanya hivyo akiwa ameshikiwa bunduki mgongoni - ya mgomo - ataonekana amelazimishwa na hana jinsi na kwa kweli atakuja nahotuba nyingine ya "ajali za kisiasa".
Hata baada ya mgomo kuishi mbona alikuwa na nafasi nzuri tu ya kuwaondoa na wadanganyika wakampa sifa kem kem? Hili alilosuburi ndio sasa ataonekana buza kwani ataonekana anaongoza kwa kutojiamini. Anyaway Kikwete haoni mbele ya pua yake....
 
nachagua kutounga mkono mgomo wa madaktari ili kuokoa maisha ya watanzania wenzangu. Naunga mkono serikali na madaktari waendelee na mazungumzo kufikia muafaka.

Kwa walioshuhudia mateso ya wagonjwa na vifo vya watanzania wenzetu naamini wanaafiki kwamba serikali na madaktari warudi meza ya mazungumzo kabla ya hatua ya kugoma.
Kitu gani unategemea kitazaliwa hapo mezani? Sioni jipya! Nadhani madaktari wanafungua njia kwa wengine kuwa serious next time wakigoma kwa kukataa vikamati vya kuonana na wakubwa ambavyo baadae huishia kuhongwa huku matatizo yakiendelea. Una lipi la kuitetea serikali kwa sloppiness ya hali ya juu inayowaonyesha wwananchi wake? Kipaumbele cha nchi ni hizo safari zake za kijinga? Ni kuhonga wabunge ili wasizuie mambo yasiyo na tija kwa taifa? Mtu kama Ngeleja anadanganya taifa kuwa umeme sasa ni history bado anabaki madarakani ni wa kukaa naye mzungumze? Ahadi za uongo za JK ni za kukalia kuzungumza? Ni heri watu wachache wafe ili taifa lipone kuliko kukaa na nchi iliyokaa na wagonjwa asilimia 99. Hongera madaktari, gomeni na walimu nao wataanza karibuni, polisi nao wako njiani, wafanyakazi wa umma kwa ujumla wao nao vivyo mpaka wakome kuleta solutions za kijinga kwenye mambo serious! Naunga mkono hoja!
 
Kwanza nisema nawaunga mkono madaktari wagome and this time msihache mpaka mnachotaka kipatikane maana wamezoea kuwanyanyasa.

Hao wanaolaumu madaktari hawaitakii hii nchi mema! Serikali inapuuza watz walioiweka madarakani na kuiba raslimali zetu, mawaziri wote wapo kibyashara zaidi ya kazi.

Gomeni wananchi wengi wanawaunga mkono.
 
nadhani hamjawasoma madr. Wao wanajua madai yao yanaweza kushughulikiwa lakini si na akina Mponda na Nkya. Madr wanadai hali bora za huduma kwa wagonjwa, wanadai nyongeza ya posho zao, wanadai kuheshimiwa kwa taaluma yao-tatizo lililopo kwa taaluma zingine zote. Hauoni nchi inaongozwa kiporojjoporojo tu hakuna mtaalamu yeyote anaheshimiwa? Mimi nawaunga mkono madai yao ili kuwe na heshima kwa wataalamu wetu tuliosomesha kwa gharama kubwa. Wakigoma wao na madai yao yakitekelezwa yanafungua mlango kwa wengine kufanya vivyo na hii itawapressurize wakubwa kuweka priorities zao vema ndipo tutakapoona mikataba inarekebishwa na inanufaisha nchi kuliko ilivyo dasa. Utaona kuna kuwajjibishana kwenye nyanja zote na utaona sasa watz wanaanza kufanya kazi na uchumi kukua. Pasipo mashinikizo haya yaenye gharama kubwa JK na serikali yake vitaendelea na usingizi. Akimtoa Nkya na Mponda atakuwa amepata shinikizo la kubadili baraza lake na kuona kuwa kumbe kuweka washikaji hakulipi. Na yeye JK ataanza kuona machungu ya urais na kuacha kuchekacheka ovyo. Asidhani Ikylu ni mahali pa kuuza sura bwana! Umeelewa eeeh?
Kumbe tatizo la madaktari sio posho wala mishahara wala kuboreshewa mazingira ya kazi ,wao wana chuki zao tu na viongozi wa wizara. Ama kweli bongo sasa kila mtu mwanasiasa ,hata madaktari?
 
Kama si Mponda na Nkya wao wanataka nani atatue? Inamaana matatizo ya miaka nenda rudi sekta ya afya yameanza kipindi cha kina Mponda? Ni wapi katika madai yao wametaja kutetea maslahi ya mgonjwa? Haya kama matatizo ya kuheshimiwa taaluma yapo kwa wote ni kwanini hawataki madai yao yaunganishwe na wenzao kwenye sekta moja?


Ndio maana mwl Nyerere wanafunzi wa UDSM walipoandamana miaka ile aliwakaribisha Ikulu vizuri halafu akawakodia mabasi lakini wakazomewa na wananchi njia nzima. Na walipoingia kwenye ajira wakakutana na mazingira magumu hamna kupanda cheo haraka haraka wakati wewe huthamini kidogo unachopewa na taifa.
 
Mimi nilisema hao madaktari wakikubaliwa kila wanachokisema mwisho watasema hatumtaki waziri, na wakikubaliwa watasema hatumtaki waziri mkuu au Rais.

Fukuza wote hao, leta wa cuba na wachina na wahindi, wamejaa kibao.
 
Nakwambia hawa madokta wanapoelekea watataka wapewe helicopter za kuendea kazini. Lakini lesson kwa serikali kujipanga na plan B ,yaani BCP in case hawa jamaa wakigoma maana naona wanatafuta utajiri sasa.
 
nachagua kutounga mkono mgomo wa madaktari ili kuokoa maisha ya watanzania wenzangu. Naunga mkono serikali na madaktari waendelee na mazungumzo kufikia muafaka.

Kwa walioshuhudia mateso ya wagonjwa na vifo vya watanzania wenzetu naamini wanaafiki kwamba serikali na madaktari warudi meza ya mazungumzo kabla ya hatua ya kugoma.
unaonekana unapenda sana warsha na vikao vya harusi... huna point, huna malengo wala hujui maana ya kukamilisha kazi

cr@p!
 
Nakwambia hawa madokta wanapoelekea watataka wapewe helicopter za kuendea kazini. Lakini lesson kwa serikali kujipanga na plan B ,yaani BCP in case hawa jamaa wakigoma maana naona wanatafuta utajiri sasa.

A sign of ill informed dude, who is probably not living in Tanzania, or is part of the caucus that sucks all poor tanzania blood to irrigate their rose gardens
 
Ukweli ni kuwa serikali ya JK ipo kikaangoni kuhusu madai yaliyotolewa jana na madaktari kumpa hadi Jumatano awe ameshawafukuza waziri wa afya Dr. Haji Mponda na naibu wake Lucy Nya kwa madai hao ni wabaya wao na bila kiburi chao labda mgomo ule usingefika pale ulipofikia na tayari waziri mkuu alishatekeleza wajibu wake wa kumfuta kazi katibu mkuu wa wizara hiyo na kumtupia kiporo kilichobaki JK.

Huo unaonekana ni kama mtego endapo rais atatii maagizo hayo baada ya madokta kusema hivyo. Ni bora rais angemfukuza kipindi kile kile Dr. Mponda na naibu wake hali ingekuwa shwari lakini tabia ya kusubiri kupima upepo ndiyo iliyomfikisha hapo JK kupewa shinikizo!

Hivi sasa kauli hiyo ya madokta inajadiliwa na maafisa usalama ili waone jinsi watavyomshauri rais vizuri. Katika majadiliano hayo bado chanzo cha madaktari kufikia hatua ya kutoa shinikizo kama hilo hakijajulikana ni nini hasa? Wachambuzi hao wanachelea kusema isije leo ikawa kwa waziri wa afya na naibu wake kisha rais akawafukuza halafu kesho wakasema tutagoma endapo waziri mkuu hataondolewa madarakani kwani nae ni mchawi katika mgogoro wetu!!!

Hilo ndilo linaloiimuza serikali ya JK.

Mgomo wa madaktari sasa utazidi kuwa shubiri katika wakati huu ambayo mambo hayajatengamaa serikalini kifedha.

Madai ya madaktari ni mengi na karibu yote yanahitaji fedha jambo ambalo linazidi kuongeza ugumu.

Nawasilisha.
 
Status
Not open for further replies.

Similar Discussions

Back
Top Bottom